Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta jana alizima hoja ya Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa (Chadema) kuhusu tuhuma dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha, kuingilia mchakato wa zabuni ya uchapishaji wa vitambulisho vya taifa.
Akielezea kwa nini alichukua hatua hiyo Spika amedai Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama imemshauri kuwa ni busara mradi huo usichelewe, uachwe uendelee hadi mwisho na kama hapo baadaye itaonekana kuna tatizo, kamati itarejea kuijadili.
Tatizo ni kwamba kulingana na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, ushauri kama huo haukutolewa na wao kama kamati. Inasadikiwa kuwa kamati iliyomshauri Spika kuchukua hatua hiyo ni kamati ya wabunge wa CCM chini ya Waziri Mkuu.
wabunge wa CCM walikuwa wakitafuta msimamo wa pamoja wa namna na kumdhibiti Dk. Slaa atapowasilisha hoja binafsi inayotaka maelezo ya serikali kuhusu hatua ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha, kuingilia mkachato wa utengenezaji wa vitambulisho vya taifa.
Lengo kuu ya hii kamati ya Wabunge wa CCM inaonekana ni kujaribu kumlinda na kumwokoa mhusika na kashfa ambayo ingemwandama. Je hii haithibishi ule woga wa wengi wetu kuwa wabunge wetu wako pale kwa maslahi ya CCM na si wananchi wala taifa?
Je, ni adhabu gani inafaa apewe Spika ikithibitika kadanganya bunge.