Matokeo ya kidato cha pili mwaka 2017 yalitangazwa tarehe 8/1/2017. Matokeo hayo yanaonesha ufaulu mzuri kwa shule za binafsi kuliko shule za umma kwani kati ya shule kumi zilizofanya vizuri Tanzania, zote ni za binafsi.
Hata hivyo kwa shule zilizofanya mitihani ya masomo ya biashara inaonesha somo la commerce limefanya vibaya kuliko ilivyotarajiwa. Kwenye shule nyingine commerce imefanya vibaya kuliko hata hesabu na fizikia. Matokeo ya commerce yameendelea kuwa mabovu kwa mfululizo wa miaka kadhaa kwa kidato cha pili na cha nne.
Kwa mtazamo wangu, Kwanini tusitangaze matokeo ya somo hili kama janga la taifa ili kama inawezekana tulete mjadala wa kitaifa? Maana kama tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda, inabidi pia tutengeneze watu makini kwenye biashara ili kuiwezesha Tanzania kuuza bidhaa zitakazozalishwa na viwanda vyetu ndani na nje ya nchi.
Ni wazo langu tu kwamba kama tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda inabidi tutengeneze uwiano mzuri kati ya masomo ya biashara na sayansi maana kuongeza uzalishaji kunahitaji sana kupanua masoko yetu ya nje na ndani ili viwanda vistawi.