Je, Sokoine alikufa kwa ajali ya gari, Au aliuawa kwa kupigwa risasi 18 kifuani?

Wanaokumbuka vizuri waatujulishe. Gari alilokuwa anatumia Sokoine siku ile alipopata ajali lilikuwa Mercedes Benz au Land Rover?
 
Hivi huyo Dumisan Dube raia wa afrika kusini wanayesema alimgonga na gari alifanywa nini?
 


Mkuu ilikuwa ajali kama ajali nyingine tu. Nisiache kukuwekea hii hapa:

 
Hii story umeunga vipande vya hadithi ulizosimuliwa toka sehemu mbali mbali na wewe ukatudanganya hapa tukuone unajua ukweli.
Story ya awali kabisa ya kifo cha Sokoine ilihusu uchawi na kwamba alirogwa na kupelekwa Gamboshi na Kawawa na genge lake la akina Mzee Msuya. Kwamba kilichozikwa ni gogo tu.
Awali tukiwa watoto tuliamini sana huu ujinga, hadi siku nilipokutana uso kwa Uso na dereva wa Mercedes Benz aliyekuwa akiendesha gari ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine. Hakuna hata moja uliloeleza linaloshabihiana na ukweli. Na usiniambie eti alichosema dereva yule kilipangwa na system. Watu wa Musoma Mjini wanamfahamu huyu jamaa maana amefanya kazi ofisi ya RSO Mara zaidi ya miaka 7 ambako alihamia akitokea Rukwa na amefariki miaka chini ya 5 iliyopita. Nyerere hawezi na asingeweza kufanya ufisadi wa kitoto kama huu. Wazushi kama wewe waliwahi kusema Nyerere ana mashamba ya Miwa Cuba, lakini Leo tunaona kina Makongoro wanakubali kuajiriwa na miaka 62. Tafuteni Kiki nyingine lakini hii haitusombi.
 
Hivi huyo Dumisan Dube raia wa afrika kusini wanayesema alimgonga na gari alifanywa nini?

Alifikishwa mahakamani akafungwa miaka 13. Lakini baada ya kina Mandela kuchukua nchi, kibinadamu alirejeshwa kwao.

Nyerere alikuwa mtu sana hata katika kukikubali kifo cha swahiba wake Sokoine ki hivi:

 
Nyerere aliyeweza kupiga simu benki kuu na kuagiza apewe fedha anazotaka kwa sababu za "usalama wa taifa" alihitaji kuuza meli ili aibe hela za umma?

Ushawahi kufika kwa Nyerere ukaona alivyoishi?
Ujinga ndo umeanzia hapo.. yaani nyerere aibe hela kwa kuuza meli tena aliyoinunua yeye mwenyewe!?? Halafu sokoine alikuwa na ukubwa gani wakati alikuwa mteule wa nyerere?? Hii ni moja ya hekaya za kitoto mnoo!!
 
Ujinga ndo umeanzia hapo.. yaani nyerere aibe hela kwa kuuza meli tena aliyoinunua yeye mwenyewe!?? Halafu sokoine alikuwa na ukubwa gani wakati alikuwa mteule wa nyerere?? Hii ni moja ya hekaya za kitoto mnoo!!
Nimesikitika sana, Nyerere, mtu aliyeweza kutuibia alivyotaka kama Mobutu alivyoiba Congo, lakini kwa uadilifu mkubwa akaishi maisha simple tu, kwa muktadha wa kiongozi wa taifa, leo hii amekuja kusingiziwa wizi kijinga hivi.

Nyerere ana makosa mengi, kifalsafa, kisiasa, lakini hili la wizi bado sijaliona.

Alipofariki Nyerere, alikuja Mama Gracia Machel, mke wake Mandela, mwanzo kabisa, akitaka kuwa karibu na mjane Mama Maria Nyerere msibani.

Basi yule Mama akapelekwa Msasani kwa Nyerere.

Alipofika Msasani, alivyopaona pako simple vile, na jina la Nyerere alivyolijua limevuma dunia nzima miaka na miaka kwamba Nyerere ni bonge la giant katika siasa za dunia, yule Mama akaona bila shaka hapa si kwa Nyerere, hii ni government guest house tu nimeletwa kupumzika kabla ya kufika kwa Nyerere.

Mama Gracia Machel akasema jamani nipelekeni kwa Nyerere nataka kufika mara moja nikae na Mama Maria, msinicheleweshe.

Watu wakamwambia Mama mbona umeshafika kwa Nyerere ndiyo hapa.

Yule Mama alivyopaona pako simple ilikuwa kama hajaamini hapo ndiyo kwa Nyerere.

Nyumba ya Butiama ya Nyerere aliyojengewa na jeshi ndani kuna viti vya plastiki. Vile viti wanavyoweka watu kukalia nje kwenye bar kunywa pombe, viko ndani Wazanaki wanakalia. Kama vile si nyumbani kwa rais.

Sasa mtu kama huyo aibe hela afanyie nini?
 
Kwa maisha aliyoishi Nyerere baada ya kustaafu. Na hata aina ya maisha ya familia yake baada ya kifo chake, sioni base yotote ya kudai Nyerere alikuwa fisadi.

Linganisha familia ya Jomo Kenyatta wa Kenya na ya Nyerere. Familia ya Kenyatta ni matajiri sana hata kwa macho ya nyama tu iko wazi kabisa. But familia ya Nyerere hata ukifika pale Butiama wako kawaida sana kimaisha.
 
Hata kama aliuwawa na Nyerere secret police,tukijua sasa hv haiwezi kutusaidia kitu,wote waliohusika wameishakufa,
Ni kawaida,ukijifsnya kieleele zaidi ya Raisi,lazima utulizwe,ilitokea kwa Robert Ouko wa Kenya,George Saitoti wa Kenya,
Ni system duniani kote
 
“Of course I found 18 bullets in his chest when I was doing postmortem” haya ni maneno yalitamkwa kwenye Bar moja jijini Dar es Salaam na Dr. Shaba (surgeon) daktari bingwa wa maswala ya upasuaji;

A single bullet is enough to totally eliminate the intented target!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…