Je, sisi bado ni watumwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, sisi bado ni watumwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mundali, Sep 16, 2010.

 1. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Katika mchakato huu wa uchaguzi, mgombe wa chama cha mapinduzi amesikika akitoa ahadi kemkem, kule atawapa meli, wengine maji ya kudumu na kadhalika.
  Kinachonishangaza ni kwamba utekelezaji wa ahadi zake unategemea wafadhili zaidi kuliko ubunifu wa vyanzo vya mapato vya ndani. Hali hii haina tofauti na mvulana anaemuahidi rafiki yake wa kike mkufu wa dhahabu akitegemea kuomba fedha kwa baba.

  JK hayo ni mawazo ya kitumwa, amka ndugu yetu hakuna mjomba toka nje atakayewapa maji watanzania bila kuwachuna. Nakumbuka msemo wako "ukitaka kula sharti nawe uliwe" angalia usije ukaliwa wewe na ukaishia kunawa tu.

  JK japo ubunifu kidogo tu, misamaha ya kodi inazidi makusanyo! Huoni haya mabo?

  Ati elimu bure haiwezekani, bila aibu wewe na kinana mnatamka maneno hayo. Mnaweza kuwaonesha watanzania risiti mlizolipiwa ada na wazazi wenu? Mbona ninyi mlisoma tena si bure tu, na posho za kununulia sabuni na kadhalika mlipewa, bila kusahau usafiri bure kutoka na kwenda mashuleni. Mnafikiri wadanganyika wamesahau "TRC warranties".
  Tena hata hamumwogopi Mungu ati Slaa anawadanganya wananchi, hapo nani hasa mwongo? Nyerere alitoa wapi pesa ya kuwasomesha bure JK?
  Mmeshindwa kaeni pembeni waacheni wanaoweza waongoze!
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  JK hawezi kuamka ndugu. JK ameingia urais akiwa usingizini. Sasa ndo amelala fofofo. Ndo maana kila akizinduka anadanganywa kisha anaendelea na usingizi.

  Muhimu tumpunzishe mwaka huu ili aendelee na usingizi wake. Hakika hakuna atakayemsumbua hata alale masaa 24.

  Jitahidi kuwahamasisha watu tusaidiane kumpa JK muda wa kulala zaidi.

  Kura zote kwa Chadema
   
 3. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Nimesoma kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu hadi Masters bure. Shuleni tulipewa warranties za TRC kwenda na kurudi wakati wa likizo, chuo kikuu tulipewa nauli ya kwenda na kurudi wakati wa likizo, malazi, chakula, vitabu bure na isitoshe kila mwezi tulikuwa tunapewa boom. Huo ni wakati ambapo rasilimali nyingi za Tanzania zilikuwa bado kuanza kutumika tofauti na wakati huu. By the way nilianza darasa la kwanza miaka ya 1980,s na chuo kikuu 1980,s na hapo nilisoma na wengi ambao kwa sasa wapo kwenye uongozi wa nchi na nje ya nchi. Sote tulisoma bure!
   
 4. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ama kweli "hakika mtu mwenye akili akijua kwamba una akili akakuambia jambo la kipumbavu na wewe ukalikubali atakudharau" na "ukiwa na kipande cha almasi, akaja tapeli na kipande cha chupa akakwambia mbadilishane na wewe ukakubali tena huku ukichekelea, unakuwa zuzu tu".
  Enyi wana wa kilimanjaro, JK amewaahidi kuzungusha barabara za lami kwenye mlima wooote wa kilimanjaro, nanyi mmemshangilia kweli. Mwenzenu anawaona mazuzu tu! Kama kweli ni mtekelezaji wa ahadi, kawaulizeni watu wa kusini, kile kipande cha kilometa 60 alizoacha Mkapa kimewekwa lami? Kawaulizeni watu wa Singida kile kipande alichoacha mkapa kaweka lami? Na maeneo mengi tu. Huyo hasemi kweli, ndio sababu hata Tendwa alisema ahadi alizotoa ni uzushi mtupu.
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mbona unakwenda mbali? aliahidi nini kwao wilayani bagamoyo na amewafanyia nini?
   
 6. m

  mjukuu2009 Member

  #6
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kweli kaka.
   
 7. S

  Safre JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Eeeh! Hadi bagamoyo amewadanganya? Nyumban?kuwa serious mkubwa
   
Loading...