Je, siri ya China kupunguza umaskini ni nini? Ni kwa jinsi gani ‘kijiji cha kwanza cha China katika kupambana na umaskini’ kilivyofanikiwa?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Je, siri ya China kupunguza umaskini ni nini?

------Ni kwa jinsi gani ‘kijiji cha kwanza cha China katika kupambana na umaskini’ kilivyofanikiwa?


Na Hassan Zhou

1617933103947.png


Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China hivi karibuni ilitangaza waraka uitwao “Kupunguza Umaskini: Uzoefu na Mchango wa China”. Waraka huo umeeleza jinsi Chama cha Kikomunisti cha China CPC kilivyoongozana na watu wa China kupambana na umaskini katika miaka 100 iliyopita, haswa baada ya mkutano mkuu wa 18 wa CPC, kutokana na juhudi kubwa zilizodumu miaka minane, mwishoni mwa mwaka jana, China ilikuwa imetimiza lengo kuu la kutokomeza umaskini uliokithiri kama ilivyopanga, na kwamba katika kiwango cha sasa ambacho ni juu ya kile cha Benki ya Dunia, watu karibu milioni 100 waishio vijijini wameondokana na umaskini. Je, siri ya China ni nini? Wacha tuangalie jinsi familia kadhaa za kichina zilivyofanikiwa kuondokana na umaskini, ili upate jibu la siri.

Juhudi za kuondokana na umaskini katika sehemu za vijijini China zilianzia miaka zaidi ya 30 iliyopita katika kijiji kimoja kiitwacho Chixi, kusini mashariki mwa China.

Chixi ilikuwa ni kijiji cha mlimani, wakazi wengi wakiwa ni wa makabila madogo madogo. Zamani, maisha ya wanakijiji hao yalikuwa magumu kiasi cha “suruani moja kuvaliwa na mtu yeyote akitoka”. Mwaka 1984, hali hii iliripotiwa kwenye gazeti na kuanza kufuatiliwa na serikali.

4444.jpg


wageni kutoka Afrika wakitembelea kijiji cha Chixi

Njia za kijiji cha Chixi za kuondokana na umaskini zinaweza kujumuishwa kama “kuchangia damu”, “kubadilisha damu” na “kutengeneza damu”, kilikabiliwa na changamoto, lakini hatimaye kimefanikiwa. Katika miaka kumi ya mwanzo, serikali ilitumia njia ya “kuchangia damu” yaani kupeleka pesa, miti na mbuzi katika kijiji hicho. Kutokana na udongo kuwa mgumu sana, miti na mbuzi hawakuweza kuishi. Lakini waswahili husema “kujikwaa si kuanguka, bali ni kusonga mbele”. Kushindwa huku kuliwapa watu wazo moja kuwa, kazi ya kupambana na umaskini inatakiwa kufanywa kwa mujibu wa hali ilivyo, na wala sio kuiga moja kwa moja.

Mwaka 1994, serikali ya huko ilichukua hatua ya ujasiri kama ya “kubadilisha damu”, na kuwahamishia wanakijiji hao kwenye eneo moja lenye mazingira mazuri. Mwanzoni, wengi wao walikataa kuondoka kwenye makazi yao waliyoishi mababu zao mlimani, lakini baada ya kuona wenzao kuhamia kwenye nyumba yenye ghorofa mbili kutoka nyumba ya nyasi na udongo bila ya kulipia hata senti moja, walikubali.

5555.jpg


mkazi wa kijiji cha Chixi akiwa ameshika chombo cha jadi cha kuvuta sigara huku akitabasamu

6666.jpg


wanakijiji wakivuna majani ya chai

Wakati huohuo, kijiji cha Chixi kiliamua wazo la kupambana na umaskini kwa “kutumia ipasavyo rasilimali zilizopo”. Japo maeneo ya kilimo ni madogo, lakini hali ya hewa ya unyevunyevu na hali ya udongo milimani inafaa zaidi kwa kilimo cha chai. Kuanzia hapo, mpango wa “kutengeneza damu” uliohusisha kilimo cha chai ulianza katika kijiji cha Chixi. Sasa kijiji hicho kimekuwa na mlolongo mzima wa kilimo cha chai. Mwaka 2019, mapato yanayoweza kutumiwa na mtu mmoja mmoja katika kijiji hicho yalifikia dola elfu 3, ni theluthi moja zaidi ya wastani wa mapato hayo ya wanakijiji mmoja mmoja nchini China.

Historia ya kijiji cha Chixi katika kuondokana na umaskini kwa miongo mitatu ni mfano mmoja hai wa vita dhidi ya umaskini hapa China. Methali ya Kiswahili inasema, kauli nzuri ni bora kuliko mali. Natarajia kuwa mifano mitano niliyoelezea yanaweza kukupa wazo jipya katika kupambana na umaskini. Wachina husema “sifa za kipekee za mazingira ya mahali fulani zinawapa wakazi wake sifa maalum”, natumai kuwa mazingira unayoishi yanakupa sifa zinazokuwezesha kimaisha.



Ikiwa una swali ama maoni kuhusu makala hii, unaweza kunitumia barua pepe katika anuani hapa chini.

64909787@qq.com

Pia unaweza kunifuatilia kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook: @yoyoasema
 
Back
Top Bottom