Matatizo ya foleni mashimo barabarani mifereji michafu wanafunzi kukosa usafiri nakadhalika, ni makubwa katika jiji la Dar kuliko SHISHA.
SHISHA NI TATIZO KUBWA KULIKO UNAVYOFIKIRIA
Uvutaji wa shisha au hookah umekuwa kama fasheni hasa kwa vijana wanaoinukia.
Wengi wanadhani kuwa shisha ni salama zaidi ya sigara na kwa imani hiyo, hata kina dada nao wamejiingiza
kwa wingi kwenye 'fasheni hiyo'.
Wengi wanadhani kuvuta moshi wa sigara yaliyopita kwenye maji ni salama zaidi ya sigara/cigar za kawaida.
Dhana hii imejengeka kutokana na imani kuwa kwa vile moshi wa sigara na vikorombwezo vingine huchujwa na maji kabla kuvutwa kwa mdomo ni salama.
Vijana wanavutiwa sana na fasheni hii kutokana na uhamasishaji ambao unafanyika dunia nzima kuhusu athari za uvutaji wa sigari pamoja na bidhaa za tumbaku. Hivyo na kuwafanya waamini kuwa shisha ni mbadala mzuri wa uvutaji wa sigara/cigar lakini ukweli ni kuwa uvutaji wa shisha ni hatari zaidi ya sigara za kawaida.
Ukweli ni kwamba mvutaji wa shisa huvuta moshi zaidi kulika mvutaji wa sigara kwani muda unaotumika kwenye shisha ni mwingi zaidi kuliko ule unaotumiwa na mvuta sigara wa kawaida.
Shirika la Afya dunia linaarifu kuwa kuvuta shisa kwa muda wa saa moja ni sawa na mtu anayevuta sigara 100 kwa mpigo. Ingawa moshi wa shisa huchujwa na maji lakini mabaki ya moshi huo bado yanakuwa na kiwango kikubwa cha kemikali zinazosababisha cancer na matatizo ya moyo.
Kwa ufupi moshi wa shisha unaviwango vifuatavyo:-
1. carcinogenic tar x 36 zaidi;
2. carbon monoxide x 15 zaidi
3.kiwango kikubwa cha lead, nickel na arsenic
4.kiwango kikubwa cha hydrogen cyanide na sumu nyingine
5. kiwango kikubwa cha nicotine ambacho hukufanya kuwa teja wa shisha
Kama tuna wahamasisha vijana wetu kutokana na madhara ya ukimwi pamoja na madawa ya kulevya basi kwa mijini inapaswa tuhamasishe vijana wetu kuhusu athari za shisha pamoja na viroba [mada hii nitaitolea maelezo yake wakati ujao]