bruno twemanye
JF-Expert Member
- May 18, 2015
- 801
- 388
Sijui mimi
Matatizo ya foleni mashimo barabarani mifereji michafu wanafunzi kukosa usafiri nakadhalika, ni makubwa katika jiji la Dar kuliko SHISHA.
Sinui hii kitu.. Tena kama ipo nionje maana hata taasisi ya tfda wapo kimyaaa... Je inatokana na mchicha?Habari wanajamvi,
Hivi sasa kuna mazongezonge yanaendelea kuhusu shisha. Huu mjadala wa shisha ni mpana na mrefu sana. Wakati hayo mazongezonge yakiendelea hebu ngoja tuulizane hivi shisha ni madawa ya kulevya au ni kweli shisha ina madhara makubwa kuliko bange au sigara? Mbona ilikuwa inavutwa hadharani? Hivi ni kiwango gani cha kilevi kilichoko kwenye shisha ambacho kinaruhusiwa au kisichoruhusiwa?
Mbona katika orodha ya madawa ya kulevya iliyo katika Sheria Kuu ya Madawa Na Uzuiaji Wa Usafirishaji Wa Madawa Haramu shisha haijaorodheshwa?
Kuna kipindi Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani ya mwili na mfumo wa hewa, Meshack Shimwela alisema madhara ya shisha ni kama yale yanayosababishwa na uvutaji wa sigara pengine na zaidi kutokana na kilevi hicho kuwa na tumbaku nyingi.
Mwanzoni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitangaza kupiga marufuku uvutaji wa shisha katika maeneo yote ya Jiji la Dar sambamba na hilo agizo lipo agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alivitaka Vyombo vya Dola nchini kuwachukulia hatua kali za kisheria watu watakaobainika kujihusisha na Matumizi ya Shisha.
Juzi hapa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema atamwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda iwapo hatasimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya dawa za kulevya aina ya shisha.
Hatua hiyo inatokana na kauli ya Makonda kuwatuhumu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi Suzan Kaganda, kulegalega kusimamia suala hilo huku akihofia wanaweza kuwa wamehongwa na watu waliotaka kumhonga lakini akakataa.
Binafsi ningeomba Mamlaka ya Chakula, Dawa na Lishe itufahamishe kama kweli hii shisha ni kilevi. Naona kama kuna jambo linalohusu matumizi ya shisha halijaeleweka vizuri na wahusika ambao ni TFDA, polisi na Mamlaka zingine.
Hizi taasisi zinaonekana zinafahamu kwamba kuna ombwe fulani katika kutekelezaji agizo la uzuiaji wa matumizi ya shisha na hawajatoa tamko lolote ila wameachiwa polisi wakamate watu. Hao polisi nafikiri wanajiuliza kama iwapo wanayo mamlaka ya kukamata kitu kisichojulikana wala kuelezwa kwamba ni madawa ya kulevya kwa mujibu wa sheria.
Vile vile nafikiri polisi wanajiuliza iwapo ukimkamata mtu na kumfikisha mahakamani pasi kuwepo kwa sheria itakuwa imetenda haki?
.................................
..........................
Point ya msingi ni hii hapa kiafya kama itatumika kwa mtu zaidi ya mmoja ile pipe yake HEPATITS,INFLUENZA,TUBERCLOSIS,INFLUENZA,H.PYLOL na magonjwa mengne hyo ndio point ya msingi hakuna kingne zaidi ya hicho
Kuna MTU anasema eti wewe ndio Paul Makonda MWENYEWEHata mahotelini tunachangia sahani, vikombe, nyuma na vijiko! Cha msingi no kanuni gani za usafi zinatumika!!!?