Je, Shisha ni nini? Madhara yake ni yepi?

sasa hyo shisha kuna wengine wanaongeza na marijuana weeee,mi nilijaribu cku moja tulikua kwny party kumbe walichanganya na hiyo bangee,kesho yake wakanipigia simu kuniambia,nilichoka nimekoma!
 
Hatari aisee hiyo, kwaiyo umeshawai kula mjani? passion lady
sasa hyo shisha kuna wengine wanaongeza na marijuana weeee,mi nilijaribu cku moja tulikua kwny party kumbe walichanganya na hiyo bangee,kesho yake wakanipigia simu kuniambia,nilichoka nimekoma!
 
Last edited by a moderator:
Iv hygene (haijini) ya ule mpira ikoje?

Swali la msingi sana, watumiaji tunaomba mtupe briefing ya usafi na afya ya huo mpira. Kuna mtu ametaja 'filter' au kichujo, na kila mtu hupewa kichujo chake binafsi, sio? Je waandaaji wanajiridhisha vipi usafi wa mrija na usalama wake dhidi ya maambukizi ya vimelea vya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya hewa?
 
‘SHISHA' marufuku kutumiwa ndani ya Tanzania na Kenya

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepiga marufuku matumizi ya uvutaji tumbaku ijulikanayo kama ‘Shisha' kutokana na madhara yanayotokana na kilevi hicho ambapo athari kubwa huwa ni kwa mtu asiyetumia kilevi hicho kwani anaweza kuugua saratani ya mapafu kwa urahisi, tofauti na mtumiaji.

Akizungumza na FikraPevu leo Julai 21, 2014 Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Steven Kebwe, amesema baada ya serikali kufanya tathmini juu ya matumizi ya kilevi hicho imegundua madhara makubwa yanayowapata watumiaji na kuwa serikali inawataka watumiaji wa kilevi hicho kuacha kukitumia haraka iwezekanavyo, baada ya kushamiri kwa matumizi kwa kilevi hicho nchini.

"Kwa uhalisia ni dawa mojawapo ya kulevya na inachanganywa na vitu vingi mno vinavyoathiri mwili wa binadamu, na hata wengine wanaweka Bangi, Tumbaku na Cocaine ambapo vitu kama hivi haviruhusiwi na tulishaliongelea Bungeni suala hili mwaka huu" aliiambia FikraPevu.

Amesema watu watakaopatikana na hatia ya kutumia kilevi hicho kuanzia sasa hadharani, watapambana na mkono wa sheria kwani wamekuwa mtumiaji wa kilevi hicho hapati madhara makubwa kama mtu asiyetumia kilevi hicho.
Aidha, madhara ya matumizi ya shisha yanategemeana na chembechembe za mwili wa mtumiaji au anayeathiriwa na moshi wake; ulevi huu ubainika kuwateka vijana hasa wa jiji la Dar es Salaam na taarifa za kitaalamu zinaonyesha kuwa ulevi huu una athari za kiafya kwa watumiaji.

Kuibuka kwa ghafla watumiaji wa kilevi hicho Dar es Salaam

FikraPevu imebaini kuwa, utumiaji mkubwa wa aina hiyo ya kilevi umeibuka ghafla nchini na kuwateka vijana hususani wa jiji la Dar es Salaam, ambapo watengenezaji hutumia chombo maalumu chenye bomba la kutolea moshi, ambacho huwekwa tumbaku, maji na moto. Waandaaji wa Shisha huweka ladha kadhaa kama vile vanila, strawberry, mint, chocolate au kahawa ili kuwavutia wavutaji.

Watumiaji wamesema tumbaku hiyo huwekwa katika chombo hicho na kuunguzwa kwa moto, kisha moshi wa tumbaku hupita kwenye maji na huingia kwenye bomba, kisha watumiaji huanza kuvuta.

Maeneo maarufu yanayotajwa kuwa Shisha huuzwa kwa wingi ni Mwananyamala, Kinondoni, Ufukwe wa Coco, Sinza Barabara ya Shekilango na maeneo kadhaa ya mighahawa mitaa ya mjini ambako vijana hupendelea kujivinjari kwa nyakati tofauti na kuwa kutumia kilevi hicho kwa siku nzima ni shilingi 10,000 (ingawa gharama hizi huweza kuongezeka sehemu za migahawa).

Shirika la Afya Duniani

Taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaeleza kuwa, mkupuo mmoja wa shisha una kemikali hai 4,800 na kwamba kemikali hizo husababisha saratani ya mapafu, maradhi ya moyo na maradhi ya mfumo wa upumuaji na kuwa kiasi cha uvutaji wa shisha kwa saa moja ni sawa na kuvuta takribani sigara 100 hadi 200.

Shirika hilo limesema licha ya kuwa watengenezaji na wavutaji wa shisha kudai kuwa haina madhara kwa sababu huchanganywa na maji, lakini bado madhara yake ni makubwa na kuwa watumiaji wanatakiwa kutambua madhara ya kilevi hicho, badala ya kuchukulia kuwa ni mtindo wa maisha tu au starehe isiyo na madhara.

Kenya nayo yasisitiza ni marufuku kutumia kilevi hicho

Uvutaji wa kilevi nchini Kenya unaendelea kukuwa kwa kasi na kuwateka vijana wengi ambapo serikali ya Kenya kupitia idara husika imeamua kuchukua hatua za kupiga marufuku na kuweka sheria mpya.

Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na onyo kutoka kwa wataalamu wa afya nchini humo walioeleza kuwa kilevi hicho kina athari kubwa zaidi ya uvutaji wa sigara, ambapo nchini humo shisha ndio mtindo mpya wa vijana wanaotumia kujiburudisha katika vilabu vya burudani Wake kwa Waume.

Kwa taarifa zaidi soma FikraPevu.com
 
wameona zinatishia hisa za TCC tu, wacha nimwambie cute b alisokote bonge la benge tuvutee
 
Last edited by a moderator:
Hii kitu ni hatari kuliko Sigara,kuna wengine wanavuta Shisha na hawavuti Sigara!

Shisha ilianzia Misri miaka mingi sana na ni maarufu sana Midle east yote

iliwahi kupigwa marufuku katika nchi fulani ya Gulf,lakini watumiaji wake wakalalamika kwanini Shisha ipigwe marufuku wakati Sigara ruksa kuvuta?! Ilibidi Serikali iruhusu tu watu kuendelea kuvuta

Lakini kila kwenye mgahawa wa Shisha kuna tangazo linalo elezea kuwa Shisha ni hatari kwa Afya yako.
 
sasa hyo shisha kuna wengine wanaongeza na marijuana weeee,mi nilijaribu cku moja tulikua kwny party kumbe walichanganya na hiyo bangee,kesho yake wakanipigia simu kuniambia,nilichoka nimekoma!

inavutia
 
Mmh... Kwa muono wangu sigara ni hatari kuliko shisha... Tazama tu mbinu ya uchujaji moshi

Shisha ni hatari zaidi Mkuu,tena ile paipu inaongeza risk ya kuambukizana magonjwa kama TB
 
Picha za mitungi ya kuvutia shisha
 
Attachments

  • 1432150485733.jpg
    1432150485733.jpg
    43 KB · Views: 239
  • 1432150501397.jpg
    1432150501397.jpg
    16.3 KB · Views: 219
Jina SHISHA limetokana na Kifaa hicho Shisha kufananishwa na Zile Pampu za kwenye vituo vya kuuzia mafuta "Petroleum Station" ambapo Pampu hizo waarabu huziita Shisha..

Shisha ni HATARI KWA AFYA nashauri watumiaji waache mara moja na wale wasiotumia usijaribu eti kuvuta mara moja ni rahisi sana kulizowea to be addicted.
 
Back
Top Bottom