Je, Serikali ipitishe sheria itakayotoa Uhuru wa Kujitoa uhai?

Megalodon

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
2,238
4,059
Kwa sheria za Tanzania, jaribio lolote la kutaka kujiua ni JINAI, na ukinusurika, unaingia kwenye vyombo vya dola na kushitakiwa.

Hii inapingana na uhuru wa mtu binafsi (Autonomy) kujiamulia maisha yake.

Euthanasia (Mercy Killing) ambayo ni Voluntarily, muhusika mwenyewe kwa msaada wa watu wa Afya, aidha kwa kutumia dawa, lethal injection au kukatiwa Oxygen in a peaceful way anaridhia kufa.

Tumeshuhudia baadhi ya wa TZ, kujipiga risasi, kujitundika kamba au kupanda gorofani na kujiachia. Hii ni aina mbaya ya Euthanasia ambayo wakati mwingine mtu hafi na kubaki kilema kibaya au kubaki kwenye damage kwa muda mrefu.

Kwa kutambua uhuru wa kujitoa uhai, Serikali kupitia bunge tukufu, je inahaja ya kupitia na kupitisha Sheria itakayotoa Uhuru wa kujitoa uhai ili hata wagonjwa walio kwenye terminal stages , wawe assisted suicide badala ya kuendelea kuishi kwenye maumivu makali yasiyo na tiba kama vile kansa, Aids stage 4 or debilitating damage .

Nawasilisha
 
Tunapoelekea huko utasema hata mwanaume kuingiliwa kinyume na maumbile ni haki yake!

Haki zina mipaka braza, hilo hata hao watetezi wa haki za binafamu wanalijua. Kila kitu kina kiasi..kikipitiliza kunakuwa ni tatizo. Ikumbukwe kwenye haki pia kuna utamaduni,Mila,desturi na madili ya jamii. Ndio maana hakuna makubaliano zaidi ya Kidunia kuhusu uhalali wa maazimio ya haki za binadamu ukiondoa yale yaliyopitishwa na waasisi/wanachama wachache wa nchi za Magharibi mwaka 1948.
 
Tunapoelekea huko utasema hata mwanaume kuingiliwa kinyume na maumbile ni haki yake!

Haki zina mipaka braza, hilo hata hao watetezi wa haki za binafamu wanalijua. Kila kitu kina kiasi..kikipitiliza kunakuwa ni tatizo

Nchi za Ulaya na America na India

Assisted Suicide ni common practice

Kwa Tanzania, tunaweza kuweka hiyo sharia with terms
 
Hakuna sehemu wanaruhusu kujiua bali kuna sehemu kutokana na mazingira mfano mtu yupo kwenye mashine kwa muda mrefu au ana maumivu makali kwa kibali unaweza kufanya hivyo yaani anayefanya hivyo itaonekana kwamba hajaua...,

By the way kama unataka kujiua si utakuwa umekufa sasa nani atakushitaki..., kama umeshindwa kutekeleza hilo jambo unataka tukupe zawadi ? Kwa kukusaidia huenda tukakupa kifungo kingine cha kupelekwa kwenye uangalizi wa afya ya akili....

Tuna mambo mengi ya kufuatilia kama nchi haya mengine ni ya kupotezea wewe kama unataka kuondoa uhai wako hakikisha kwanza umemaliza majukumu yako (usituachie wananzengo kutunza familia yako) jipeleke sehemu chimba kabisa kaburi utakapozikwa na acha pesa za funeral services... alafu Rest in Peace
 
Fanya Research zako vizuri. Soma kwa bidii
 
Mbona unawasemea watu

Tuna tuna,
Akili yako isiwe kwenye sandwich basi mkuu

Let it free
 
Nchi za Ulaya na America na India

Assisted Suicide ni common practice

Kwa Tanzania, tunaweza kuweka hiyo sharia with terms
Kwa Mila, utamaduni na madili yao wako sahihi kwetu bado yanakinzana na Mila zetu. Kwa mfano kuna baadhi ya makabila mtu aliyejiua hazikwi kwenye makaburi ya ukoo na tena hakuna kuweka matanga au watu kulipa. Maiti yake haipewi heshima. Jamii yetu inatafsiri vibaya kitendo Cha mtu kujiua ni kama laana au udhaifu.
 
Mbona unawasemea watu

Tuna tuna,
Akili yako isiwe kwenye sandwich basi mkuu

Let it free
Unadhani katika utungaji wa Sheria na Ufuatiliaji wa mambo kama Taifa kuna Mlipa Kodi yoyote ambaye hausiki ?.., Kwahio sababu pesa yangu inaklusanywa kwenye mambo kama haya kwahio mimi ni Mdau
 
Back
Top Bottom