ThaGreatman
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 708
- 1,465
Nianze kwa kukupongeza Mh.Rais,kwa majukumu mengi uliyonayo ya kulijenga taifa hili masikini, si kazi ndogo!
Mh.Rais,natambua fika kwamba andiko langu hili laweza kujadiliwa kwa namna tofauti na watu tofauti tofauti,(ubinadamu asilia). Wafanyakazi walio wengi hawaelewi na hata sisi wengine hatuelewi sintofahamu hii katika utumishi wa umma,unasababishwa na nini haswa?Ni mwaka wa NNE sasa watumishi stahiki zao za kisheria hazitekelezwi,(hakuna ongezeko la mishahara,wala kupandishwa vyeo,au madaraja kama ilivyozoeleka kuitwa), hivi tatizo ni kwamba hatuna fedha?au umeamua kukomoa watumishi wa umma kwa makusudi?
Kuna wakati ziliwahi kusikika tetesi kwamba,"watumishi wa umma walio wengi,walimuunga mkono mshindani wako mkubwa katika uchaguzi wa 2015" na hivyo ulikuwa hasira nao kweli kweli kwa kuwa hawakuonyesha ushirikiano (sina hakika kama kauli hii ilikuwa na ukweli au lah!), lakini yote kwa yote, ni kwamba watumishi wa umma wanakiona cha mtema kuni!
Kama hisia za kuunga mkono Lowassa ndo chanzo kikuu cha kuwakausha juani watumishi wa umma,ni matumaini ya watumishi walio wengi sasa kwamba wataanza kuneemeka angalau kwa kuongezewa mishahara na kupandishwa madaraja yao,ili kukabiliana na mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya shilingi, kwa sababu waliyemuunga mkono sasa amerejea na kukuunga mkono,kwa maana nyingine watumishi sasa watakuwa waungaji mkono wazuri wa juhudi zako!
Kibaya zaidi ni kwamba hata sheria za utumishi wa umma sasa zinang'ata upande mmoja tu,(wa mtumishi),akienda kinyume na sheria na au kanuni za utumishi wa umma,kama zilivyorekebishwa mwaka 2002,anakiona cha mtema kuni,lakini sheria hiyo hiyo iliyompa wajibu mwajiri imepuuzwa na hakuna tatizo kabisa!(sheria imebaki na jicho moja pekee).
Mh.Rais,kwa heshima kubwa kabisa,tunaomba utazame kundi la watumishi wa umma,hao ndiyo wanawezesha maisha ya wengine kwenda sawa sawa!(angalau kwa kutupatia visenti kupitia biashara zetu ndogo ndogo na shughuli za ujenzi).
Watumishi wamejaa vinyongo ambavyo nadhani,2020 vinaweza kuleta changamoto sana kwenye kujinadi mbele yao!!!