Je, Serikali imehalalisha trafiki kupokea rushwa?

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,737
Mimi ni mtumiaji Sana wa usafiri wa haice mkoa wa Arusha.

Nimekuwa nashuhudia kila wakati nikiwa natumia usafiri huo kuona trafiki wakipokea rushwa Kama watoza ushuru wa sokoni, bila kificho chochote.

Hasa maeneo ya friends cona, sasa na madereva wamezoea na kuona kwamba huo ni wajibu wao, akipigwa mkono tu konda anashuka na 1000 mpaka 5000, na hii ni kwasababu ya kosa la kupakia abiria pasipo na kituo.

Siungi mkono haice kupakia bila utaratibu, ila kuna vituo vimejengwa sehemu isiyostahili kabisa kwani abiria itamlizimu atembee Hadi m 300 kwa kusonga barabara ili aingie sokoni kutoka kituoni au asonge barabara m3 ili afike kituoni,

Je, Serikali ni kwamba haioni kuwa aliye vunja Sheria naye anaadhibiwa kwa Sheria kuvunjwa?
 
Hoja kama hizi hazina wachangiaji, ila kila mkoa na wilaya TZ hii ni kati ya tozo za kawaida kabisa.

Nadhani ni utekelezaji wa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.

Nothing to change. Hata baada ya kuandika uzi huu mradi huu utaendelea na hata wewe najua unatoa! This is bongoland
 
Back
Top Bottom