Hivi..ni kwamba hao wakuu wengine hawana magari yao binafsi ya kufanya hayo?
Leo hii Halima Dendegu, Jordan Rugimbana ama Anna Mghwira akifanya haya kwenye magari yao binafsi (Passo, Rav 4 au Kluger) watasalimika?
Zzk aliposema "Malimbukeni na Washamba" aliwahusu watu wa "Jamii hii"?
Tangu usichana wao na maisha yao yote Fenella Mukangara na Janeth Mbene wamekulia kwenye familia zilizo bora (Ni moja ya wanasiasa/ viongozi waliotoka familia za ushuani kabla na hata baada ya kuolewa) walikua wakiendesha na kutumia magari ya kifahari! Lakini walipopata dhamana ama nafasi za uongozi hawaku wahi wala kuthubutu kufanya mbwembwe hizi tunazo zishuhudia kipindi hiki!
Ni mara baada ya kukosa nafasi ya uwakilishi jimbo la Kibamba (Fenella) amekua akiendesha Range Rover hadharani tena yeye mwenyewe na hata baada ya kukatwa ubunge EAC..
Ama ndio wanaiga lifestyle ya sampuli za viongozi wa Equtorial Guinnea, Congo Brazaville, Cameroon na hata Gambia? Name it!
Si kwamba namuonea wivu! LA hasha..kuna kitu kinakosekana hasa cha uongozi!
Unatoa taswira gani kwa mwananchi anae tembea kwa miguu kwa kukosa nauli toka msasani mpaka mbezi beach kwenda lindoni ?
This is not fair jamani..uswahili huu ukiufanya kimya kimya nani atakuuliza?
Tuna mijitu mishamba ya hovyo na milimbukeni inayojali social status bila kujali hali na maisha ya wanyonge!
Eti tuwaombee..! Tuwaombee nini? Kuomba omba bila kua specific ni uwendawazimu..mnachosha mnakera na kukatisha tamaa!