Je, Serikali imebadili Magari ya Wakuu wa Mikoa?

Gari la RC DSM ni range rover, ameanza kulitumia Meck Sadick, please msiwe watunwa kulalamika
 
Habari wanaJF,

Katika peruzi peruzi yangu mitandaoni nimekutana picha iliyonishangaza baada ya kuona Gari aina ya Range Rover ikiwa na Plate Number inayoashiria kuwa anapaswa kuitumia Mkuu wa Mkoa RC DSM yaani RC(Regional Commissioner) DSM(Dar es Salaam).




Je, ni wakuu wa mikoa wote wanatumia Magari haya?

Je, kama si mali ya Serikali inawezekana Watu binafsi kutumia Magari yenye Plate Number zinazofanana na za viongozi wa umma?

Kama ni mali ya Mkuu wa Mkoa, Je ni sawa kutumia Plate Number yenye hadhi ya Uongozi wa Umma katika magari binafsi?

Jitihada zote za kumshusha Makonda zimeshindikana.Kwa nini zimenishindikana na kwa kuwa ana nguzo kubwa nyuma yake.
Je tunafaidika nini kuendelea kumfuatilia wakati hakuna tunachoweza kufanya dhidi yake?
Haya ni maisha tu na yatapita kama ya kina Gurumo,Sefue na wengine.
Tuangalie mengine.
 
Hilo gari lilimpokea Makonda Alipokwenda Zanzibar, hapo ni Unguja alipofanya ziara ya kimafunzo Mkoa mjini Maghribi Unguja, Makonda hakwenda na gari huko hilo aliandaliwa na mwenyeji wake, wazandiki endeleeni kuumia najua viungulia vya wivu lkn ndio hivyo tena kama kwenye ukooo wenu mna nyota ya punda mtabeba mizigo mpaka kiama..Wazandiki mtakufa mwaka huu
 
Yana mwisho....na mwisho wake huwa mbaya....subiri Sizo atoke pale kwa hiari au shari au kutwaliwa uone maisha yatavyo badilika.....from Vogue to Kalandinga.....! Time will tell
Endelea kuomba dua mbaya lkn ujue wewe ndio utakufa njaa
 
Hoja yangu ni kuwa. Kelele nyingi kuhusu RC huyo zilianza baada ya kutuhumu watu kwa madawa. Whether utekelezaji wake ulikua butu au la. Hivyo inawezekana wanaomlalamikia ni wanufaika.
tujiulize,alichokifanya ni sawa?mimi niliona tangu mwanzo hakuwa na mamlaka yoyote ya kufanya alichokifanya.alichotakiwa kufanya kama alikuwa na ushahidi ilikuwa ni kuwapeleka mahakamani.mwisho wa siku kazi wamepewa wahusika hausikii mtu kutaka sifa kwa kuwachafua wengine.
 
209b66574b1b21485b9d14315f94bdcf.jpg


Hivi..ni kwamba hao wakuu wengine hawana magari yao binafsi ya kufanya hayo?

Leo hii Halima Dendegu, Jordan Rugimbana ama Anna Mghwira akifanya haya kwenye magari yao binafsi (Passo, Rav 4 au Kluger) watasalimika?

Zzk aliposema "Malimbukeni na Washamba" aliwahusu watu wa "Jamii hii"?

Tangu usichana wao na maisha yao yote Fenella Mukangara na Janeth Mbene wamekulia kwenye familia zilizo bora (Ni moja ya wanasiasa/ viongozi waliotoka familia za ushuani kabla na hata baada ya kuolewa) walikua wakiendesha na kutumia magari ya kifahari! Lakini walipopata dhamana ama nafasi za uongozi hawaku wahi wala kuthubutu kufanya mbwembwe hizi tunazo zishuhudia kipindi hiki!

Ni mara baada ya kukosa nafasi ya uwakilishi jimbo la Kibamba (Fenella) amekua akiendesha Range Rover hadharani tena yeye mwenyewe na hata baada ya kukatwa ubunge EAC..

Ama ndio wanaiga lifestyle ya sampuli za viongozi wa Equtorial Guinnea, Congo Brazaville, Cameroon na hata Gambia? Name it!

Si kwamba namuonea wivu! LA hasha..kuna kitu kinakosekana hasa cha uongozi!

Unatoa taswira gani kwa mwananchi anae tembea kwa miguu kwa kukosa nauli toka msasani mpaka mbezi beach kwenda lindoni ?

This is not fair jamani..uswahili huu ukiufanya kimya kimya nani atakuuliza?

Tuna mijitu mishamba ya hovyo na milimbukeni inayojali social status bila kujali hali na maisha ya wanyonge!

Eti tuwaombee..! Tuwaombee nini? Kuomba omba bila kua specific ni uwendawazimu..mnachosha mnakera na kukatisha tamaa!
Well said
 
Habari wanaJF,

Katika peruzi peruzi yangu mitandaoni nimekutana picha iliyonishangaza baada ya kuona Gari aina ya Range Rover ikiwa na Plate Number inayoashiria kuwa anapaswa kuitumia Mkuu wa Mkoa RC DSM yaani RC(Regional Commissioner) DSM(Dar es Salaam).




Je, ni wakuu wa mikoa wote wanatumia Magari haya?

Je, kama si mali ya Serikali inawezekana Watu binafsi kutumia Magari yenye Plate Number zinazofanana na za viongozi wa umma?

Kama ni mali ya Mkuu wa Mkoa, Je ni sawa kutumia Plate Number yenye hadhi ya Uongozi wa Umma katika magari binafsi?


Wapinzani wa Makonda mtakufa na vijiba vya Roho
 
Back
Top Bottom