Je, Sanitaiza inalewesha?

Je, Sanitaiza inalewesha?

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
6,767
Reaction score
20,870
Mimi mwenzenu zaidi ya miezi miwili sasa kila siku najisikia kama nimelewa lewa hivi, mawenge mawenge, kichwa nakisikia kizito, kuna wakati kinauma, mara mapigo ya moyo yananienda mbio mara najisikia kuchoka choka, kama kukosa pumzi hivi.. nk.

Mpaka kuna wakati nikawa naogopa nikahisi labda ni corona lakini miezi inakatika sijawahi kupata homa wala kikohozi. Hizi dalili zinakuja na kupotea baada ya muda lakini karibu kila siku najisikia hivyo.

Sasa leo nimekaa nikawaza labda kuna kitu nimebadilisha katika maisha yangu mfano vyakula, mafuta, nk hakuna. Nikagundua kitu pekee cha tofauti tangu nianze kupata hizi dalili ni matumizi ya sanitaiza yenye alcohol ambayo natumia kila siku mara kadhaa kusafisha mikono.

Je, kuna uwezekano kwamba sanitaiza ndio inaniletea hii hali? Je, kuna mtu mwingine amepatwa na hali kama hii?

Wataalamu mnasemaje?
 
MKUU INASABABISHA KICHWA KUWA KIZITO, KUUMA NA PIA HALI YA KUTOJIELEWA HIVI.
 
Hiyo ni alcohol babu na inawaka kabisa unaweza washia mkaa
Kwahiyo inawezekana ndio inasababisha najisikia hivi mkuu? Kwakweli nimeshafikiria sana mpaka nilitaka niende hospitali ila nikaogopa maana hospitali nako siku hizi kwenda kwenda ni hatari.
 
Kwahiyo inawezekana ndio inasababisha najisikia hivi mkuu? Kwakweli nimeshafikiria sana mpaka nilitaka niende hospitali ila nikaogopa maana hospitali nako siku hizi kwenda kwenda ni hatari.
Ndio yenyewe tena ni orginal hiyo feki haziwi hivyo haya wataalamu wamesema ukitaka kujua kama ni ornmginal uitest hivyo ikiwa tuu ni yenyewe
 
MKUU INASABABISHA KICHWA KUWA KIZITO, KUUMA NA PIA HALI YA KUTOJIELEWA HIVI.
Nawaza nifanye experiment niache kabisa kutumia sanitaiza niwe nanawa mikono kwa sabuni tu halafu nione baada ya siku chache kama hali itabadilika.
 
Hii nimekutana nayo huko google

"Alcohol is a volatile substance and diffuses rapidly in the presence of air hence, In addition to the above consequences, apart from those that may be absorbed into the blood through the skin, there is the tendency to inhale a copious amount of the alcohol into the body which may cause ocular irritation, abdominal discomforts, conjunctivitis, coughs, respiratory discomfort, oral irritations etc.

Such outcomes can be more prevalent to those that are alcohol intolerance and those that may be allergic to the alcohol and these allergic reactions (hypersensitivities) could be serious."
 
Ungejalibu kuinywa, hata usingepata tabu ya kuuliza hapa jamvini.
 
Waitaliano wanasema (latin) In vino veritas, in aqua sanitas kwa kimakua kwenye mvinyo kuna ukweli, kwenye maji kuna afya.

Tumia maji achana na pombe tayari imedhihirisha ukweli
 
Watoto huku Ulaya wananusa na kufanya kama kilevi
Alcohol imo kwenye utengenezaji ila haileweshi hivyo kwa kunusa lakini kama sio mtumiaji wa ulevi wowote basi lazima utahisi kitu

Hata kutumia sana kwenye mikono pia Ina madhara yake kwa kufanya mikono mikavu sana na wengine hupata skin disease


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Watoto huku Ulaya wananusa na kufanya kama kilevi
Alcohol imo kwenye utengenezaji ila haileweshi hivyo kwa kunusa lakini kama sio mtumiaji wa ulevi wowote basi lazima utahisi kitu

Hata kutumia sana kwenye mikono pia Ina madhara yake kwa kufanya mikono mikavu sana na wengine hupata skin disease


Sent from my iPhone using Tapatalk
Ulaya ya buza hio mkuu
 
Ulaya ya buza hio mkuu

Jisomee hii maana huwa sidanganyi
Hii shule ni USA
Adjustments.jpg



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Tangu ijumaa nimeacha kutumia sanitaiza na mpaka leo hii yale mawenge, kuumwa kichwa, moyo kwenda mbio, vyote vimeisha sasa najisikia kawaida kabisa. Nime conclude kwamba ni sanitaiza ndio ilikua inaniaffect.
 
Back
Top Bottom