Navyofahamu mimi Ridhwani hakuajiriwa Imma kabla hajamaliza shule,bali alikwenda pale kama mwanafunzi katika program ya internship,na baada ya kumaliza wakambakiza pale yeye na wenzake wawili.Hata hivyo tuhuma za ufisadi dhidi yake zinapaswa kuchunguzwa zaidi ili tujiridhishe kuhusika kwake,na kama kweli kampuni ya Imma inahusika na moja ya bogus contracts basi labda ndio maana jamaa(JK) akaamua kulipa fadhila kwa kumteua masha kuwa waziri,maana kwanza alimuajiri mtoto wake yaani ridhwani na pili hiyo mikataba.Hizi facts zinatakiwa kuwa corroborated hebu mwenye facts azishushe zaidi hapa kabla hatujaamua kutoa hitimisho
Ni kweli jamani, hebu mnaojua mtueleze:
Ridhwan Kikwete amehusika na kashfa ya Richmond?
Ridhwan Kikwete aliajiriwa IMMA kabla ya kumaliza shule?
Ridhwan Kikwete alikwenda kusomeshwa Hull kwa mchango wa IMMA?
Ridhwan Kikwete aliwasaidia IMMA kwa namna yoyote katika suala la Deep Green?
Ridhwan Kikwete alifahamu chochote kuhusu Deep Green wakati wa kampeni?
Ridhwan Kikwete anaukaribu gani na Masha wa kibiashara?
Ridhwan Kikwete ni kiunganishi kati ya Kikwete na ile Kampuni ya kina Masha ya Madini ule Mererani?
Ridhwan Kikwete alishiriki kufanikisha Kikwete kuchangiwa kwenye kampeni na yale makampuni ya madini kule Mererani?
Ridhwan Kikwete alisadia vipi IMMA kupewa tenda za uwakala na masuala ya mikataba ya makampuni makubwa ya madini? Je, ni wakati Masha akiwa naibu waziri wa wizara husika, kabla au baada?
Ridhwan Kikwete ana nafasi gani IMMA, ni mtumishi wa kawaida au ni partner?
Je- anafaa kuwa Rais wa Tanzania katika miaka ijayo ukimlinganisha na Zitto, Kitila, Mwanakijiji na Madela wa Madilu?
Asha