Panya Roads ni matokeo ya unemployment na poverty mkuu, tutibie ugonjwa sio dalili zake, vijana hawa tunaishi ishi nao majumbani mwetu hawatoki kwenye sayariya Mars, president Nyerere (rip)aliliona hili na alipambana na kuwapa uchaguzi ingia kwenye vijiji ili ulime au mitaani huku utahangaika,sasa unawachoma moto na hujawapa alternatives ya kujiajili huku sio kutibia ugonjwa we need a political will wa kuwafanya vijana wetu to think out of box

, kilimo na ufugaji ndiko kunaweza kutuzalishia ajira zaidi kwa vijana wetu, elimu ya uzazi ipewe umuhimu, hatuwezi uchumi ukue kwa 5% na tuongezeke kwa more than 3%,it's craze kikawaida Tanzania ilitakiwa iwe na raia kama 23M,but now tuna 60M!,tunaishi in a timing bom
Kwani wakati wa utawala wa Magufuli kulikuwa hakuna Unemployment?
Ninakubaliana na wewe kwamba ufukara wa mali,pia husababisha ufinyu wa fikra na hatimae kuzalisha mawazo mabaya ambayo huweza kumtuma ntu kufanya uhalifu kama njia pekee ya kujiponya(kwa mtazamo wake ambao sio sahihi pia).
Lakini tusihalalishe uhalifu kwa kuufanya kuwa ajira mbadala!
Huu utakuwa ni moja ya fikra mbaya kabisa kuwahi kutokea.
Kila jambo katika maisha linao mustakabali wake.
Huwezi kwenda kuchinja watu na ukishakamatwa na kufikishwa mahakamani ujitetee kwamba ni kwa sababu ya kukosa ajira.kwa vyovyote ni lazima utapatikana na hatia.na adhabu yake itachukua mkondo kulingana na uzito wa kosa kisheria.
Hapa nchini pamoja na kukumbwa na tatizo la ukosefu wa ajira.
Lakini bado kuna fursa nyingi mbadala za watu kuweza kuzitumia na kuendesha maisha yao.
Japo kwa kipato cha chini.
Na hilo ni jambo ambalo liko wazi kabisa.
Kuna mambo mengi ya kuweza kufanya na kama Mungu akikuwekea mkono wake....wengine hubadili maisha yao kabisa.
Hatujawafikia kiwango baadhi ya majirani zetu wa nchi za kiafrika,ambako hali ni mbaya sana kama Ethiopia ,Somalia,Eritrea na hata DRC na Burundi kwa uchache tu.
Ambako wamefikia viwango vya kuhatarisha maisha uao kwa kuzikimbia nchi zao,kwa baadhi ya njia ambazo ni hatarishi kabisa.
Lakini hawana namna ingine zaidi ya hiyo.
Ushahidi upo maana tunawaona kila siku wakikamatwa kwenye malori,tena yasiyostahili kwa kusafirishia Binadamu.
Pia ikumbukwe kwamba hawa Panya Road wengi,ni vijana au watoto ambao bado kwa umri wao wanapaswa kuwa mashuleni na vyuoni.
Kuna mahali fulani ambako kuna tatizo la kimalezi na uangalizi kwa watoto wetu kwenye hatua za mwanzo kabisa.
Tunapaswa kutimiza wajibu wetu kama wazazi,kabla ya kuirushia serikali lawama ambazo saa ingine zinatuhusu sisi wenyewe.