Je, Rais Samia Suluhu ni mnafiki?

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Ukifuatilia kwa ukaribu mambo mengi aliyokubaliana wazi wazi na mtangulizi yeye akiwa msaidizi wake kwa sasa amekuwa kinyume nayo.

Mfano suala la machinga Samia katika kikao fulani alichokuwa akipewa maagizo ya kuwasimamia wamachinga alisikika kwa uchungu akichangiza "na umachinga ndizo ajira zenyewe" ajabu sasa ndiye aliyetoa maagizo wafukuzwe katika maeneo walipo.

Suala la pili linalo leta ukakasi ni kuhusu dhuluma.Samia alipoingia madarakani alijinasibu eti hataki kodi za dhuluma akimaanisha maamuzi yale yale aliyoyafanya na mtangulizi wake ajabu baada ya yeye kuwa kiongozi yamekuwa dhuluma!

Leo,kuna tozo za dhuluma wanazokatwa wananchi kwenye miamala ya simu.

Je,Samia ni mnafiki?!
 
Suala la pili linalo leta ukakasi ni kuhusu dhuluma.Samia alipoingia madarakani alijinasibu eti hataki kodi za dhuluma akimaanisha maamuzi yale yale aliyoyafanya na mtangulizi wake ajabu baada ya yeye kuwa kiongozi yamekuwa dhuluma!

Leo,kuna tozo za dhuluma wanazokatwa wananchi kwenye miamala ya simu.
Kuna watu wana mmisslead kwa manufaa yao binafsi kwakuwa ni mwoga inabidi awe mpole siku zisogee
 
Ila tusichanganye suala la machinga na hili la wachuuzi wa bidhaa mbalimbali ambao wanaondolewa katika makazi ambayo waliyavamia.

Machinga ni vijana ambao hutembeza bidhaa zao huku wamezishika mikononi mwao. Lakini wachuuzi wao huuza bidhaa zao katika mabanda.

Wachuuzi wengi walijenga mabanda yao kiholela katika maeneo ambayo hata hawakustahili kuwepo na kuleta bugudha kwa wananchi wengine. Hapo wala hapakuhitajika suala hili kufanyiwa siasa wala nini, walipaswa kuondolewa kutokana na sheria ndogo ndogo za miji na manispaa.

Machinga bado tunawaona wakiuza bidhaa zao katika makutano ya barabara, sehemu za vinywaji baridi, makanisani, misikitini na katika maeneo mbalimbali ya starehe na burudani.
 
Ukishaingia tu kwenye siasa, ni lazima uwe mnafiki. Na hasa siasa za Afrika.
 
Pia alikataa kubambikia watu kesi. Sasa hivi watu wanabambikiwa kwa kwenda mbele.
 
mkuu samia sio mnafki Ila mama lao siasa ndo unafki. Samia alikuwa anakubali kutokukubaliana. ndio siasa ilivyo bosi.
 
Back
Top Bottom