Je, Rais Magufuli hakuyaona haya alipokuwa mbunge/waziri?

Kama alishiriki kupitisha mikataba hovyo tumwaminije sasa ivi??

Je haya madhara ya kuivunja kama ikibidi unadhani atalipa yeye au mimi na wewe?
Kwa swali la kwanza waulize Tiss na Lubuva na kama ni kulipa ni Mimi , wewe , watoto na wajukuu wetu, huwezi kukwepa
 
Hata yeye angeshinda angekuwa raisi.....kwa pia tungekuwa na raisi mwingine muoga au sio..!!?
Hapo unaongelea kitu ambacho hakipo! Mimi naongelea rais ambaye tunaye sasa ivi na sio Lowassa!!

Kama aliyaona haya na akakaa kimya kwa woga je tumuaminije???
 
Kama alishiriki kupitisha mikataba hovyo tumwaminije sasa ivi??

Je haya madhara ya kuivunja kama ikibidi unadhani atalipa yeye au mimi na wewe?
Mbona wengine tuliwaamini pamoja na kutusainia mikataba mibovu inayoutaghalimu mpaka sasa....!!??
 
Kwanza nianze kwa kusema nnaumia sana kuona makaburu wakijinufaisha na rasilimali zetu huku mzawa akipata shida zisizo na ulazima.

Lakini nnajiuliza haya...

Hii mikataba ya madini wakati inasainiwa magufuli si alikua waziri? Si alikua mbunge? Kwanini alikaa kimya kipindi hicho?

Wakati mikataba hii inasaini Rais Magufuli si alikua mbunge? Kwanini asingetoa wazo mikataba hii ijadiliwe bungeni? Lakini cha kushangaza kwanini alikaa kimya kama mbunge?

Je ni mikataba mingapi ya hovyo alipitishwa bungeni yeye akiwa mbunge na alikua mstari wa mbele kusema NDIO huku akizani anawakomoa CHADEMA?

Kwanini kipindi hicho asingeikataa kama kweli alikua na nia ya kuipigania nchi?

Ni mara ngapi mkiwa bungeni akina zitto na mnyika waliwaonya juu ya hii mikataba mkawapuuzia?

Sasa tayari mikataba imesainiwa na kama hujui tu hamna mkataba unavunjwa bila kumlipa mzungu uliyewekeana nae makubaliano.

Nitoe tu angalizo... HAWA WABUNGE WA CCM WANAOSEMA NDIOOOOO NA KUPIGA MEZA BILA KUJUA MADA NDIO WAMETUFIKISHA HAPA! Na bado tutayaona mengi.

Angalizo tu..haya ya ACCACIA yasije kuwa kama Dowansi na akina Escrow!

Mungu ibariki Tanzania!
Mzee kipindi hicho alikuwa analinda ugali wake...angejitia kifront front labda leo asingekuwa na hiyo nafasi...Lakini mwisho wa siku mi naona haya ni maigizo tuu..hichi hichi kibao sijui kama hakita tugeukia..kama yale ya samaki!!!!!
 
Mzee kipindi hicho alikuwa analinda ugali wake...angejitia kifront front labda leo asingekuwa na hiyo nafasi...Lakini mwisho wa siku mi naona haya ni maigizo tuu..hichi hichi kibao sijui kama hakita tugeukia..kama yale ya samaki!!!!!
Ndio maana nasema hawa wabunge wanapiga makofi wakizani wanawakomoa ukawa na upuuzi mtupu!! Hata yeye alikua waziri na mbunge na alikua mstari wa mbele kupiga makofi na sasa ivi ndio anajua alikosea!!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
.
Kama kweli magufuli ana uchungu na rasilimali za nchi hii serikali yake na ipitie upya mikataba yote tata aache maigizo ya kuumia na kusononokea rasimali zetu mbele ya kamera na vipaza sauti.
Na abadili sura namba 46, kifungu cha 3 ya katiba ya JMT. Hiki kinatoa kinga kwa mtu aliyeshika madaraka ya Urais kushitakiwa mahakamani, akiwa madarakani na baada ya kutoka madarakani.
 
Kama ilivyo hivi sasa wapo wabunge wa ccm na mawaziri ambao kwa hivi sasa wanaona kuna mambo ya hovyo kabisa yanafanyika lakini hawathubutu kusema lolote kutokana na njaa zao na kuonekana wasaliti!
Ni hivyo hivyo ilivyokuwa kwa magufuli!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kumlaumu rais kwamba alikuwepo wakati haya yaletayo tafrani leo unamwonea. Ukiwa ndani ya mfumo si kweli kuwa unakubaliana nao 100%, na ukionesha upinzani unatemwa, collective responsibility. Lawama kwake ni sasa ambapo anajua tatizo kuu la nchi hii ni katiba na sheria mbovu ambazo alishiriki kuzipitisha japo ni kwa shingo upande, lakini anazikumbatia, au kutaka kuzikwepa bila kuziondoa kwanza kwa taratibu zinazoeleweka.
 
Kama ilivyo hivi sasa wapo wabunge wa ccm na mawaziri ambao kwa hivi sasa wanaona kuna mambo ya hovyo kabisa yanafanyika lakini hawathubutu kusema lolote kutokana na njaa zao na kuonekana wasaliti!
Ni hivyo hivyo ilivyokuwa kwa magufuli!

Kwa maneno yako uliyoandika unamaania magufuli alikua

1. Na njaa

2. Muoga au alikua anaogopa kuonekana msaliti??

Kama haya ni kweli, na ukizingatia kwa sasa ndiye rais TUNAIPELEKA WAPI NCHI??
 
  • Thanks
Reactions: SDG
kinacho ni shangaza ni kuwa hawa watu tuliwafukuza kipndi kile cha ukoloni ila sasa tunawaita wawekezaji na tunawatetea kwa nguvu kubwa.
 
Back
Top Bottom