Maana kubwa ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi nchini ni kujibizana kwa hoja. Hiiyo maana yake ni kuwa kama wapinzani wanaikosoa serikali kwa jambo fulani, ni wajibu wa Chama kinachounda serikali kujibu kwenye majukwaa ya kisiasa hoja hizo.
Kwa bahati mbaya sana hiyo dhana imetoweka tokea serikali hii ya CCM awamu ya 5 imeingia madarakani na badala yake ni yeye Magufuli pekee ambaye "amejiona" ndiye mwenye haki za kuzunguka nchi nzima na kukinadi chama chake na kuwaaambia wapinzani, eti wao wasubiri mwaka 2020 ndipo wafanye kampeni zao!
Yeye Magufuli anaamini kuwa hiyo ONE MAN SHOW yake ndiyo itakayoivusha salama CCM
Anajidanganya kupita kiasi, kwa kuwa hiyo staili yake ya uongozi ndiyo anaichimbia kaburi CCM!
Hata hivyo wananchi wanaona uonevu huo na wataamua kuonyesha "hasira" zao kupitia sanduku la kura, ambayo ni SIRI kuanzia Novemba 26, kwenye chaguzi ndogo za kuziba nafasi za madiwani zilizoachwa wazi nchi nzima.
Tumeshuhudia pia Magu akifanya upendeleo wa wazi katika hotuba zake. Alipokuwa Mwanza hivi karibuni aliwaambia wakazi wa huko kuwa "wasibomoleshwe" nyumba zao kwa kuwa CCM inayo "human face" na hao wakazi wa Mwanza ndiyo waliomchagua!
Kwa kauli hiyo pekee Rais ameonyesha "double standard" ya hali ya juu, kwa kuwa wapo wakazi kwa maelfu waliobomolewa nyumba zao bila kulipwa fidia yoyote, kuanzia Kimara hadi Kiluvya kwa kuwa wakazi hao wameichagua Chadema kwenye uchaguzi mkuu 2015!
Pia ziko "double standard" nyingine anazofanya Magufuli.
Wakati maelfu ya watumishi wa serikali wameachishwa kazi kwa kile kinachoitwa kuwa na vyeti feki, lakini zoezi hilo "lilipomgusa" Mkuu wa Mkoa wa Dar, tulimsikia Magufuli akisema kuwa huyo kijana "wake" amekuwa "spared" kwa kuwa hata kama hajui hata kusoma A lakini kwa kuwa anamkamatia wauzaji wa madawa ya kulevya, basi huyo ndiye RC bora kabisa nchini na kwake yeye, huyo RC vyeti feki havimuhusu!
Magu pia ameonyesha "double standard" nyingine kubwa.
Wakati serikali yake ikijinadi kuwa ina zero tolerance linapokuja suala la rushwa, lakini akina Gobless Lema na Joshua Nasari walipoonyesha ushahidi wa rushwa jinsi DC wa Arumeru Alexander Mnyeti "alivyowanunua" madiwani wa Chadema kujiunga na CCM ndiyo kwanza amempa promotion DC huyo na kuwa RC wa mkoa wa Manyara!
Ni wazi kuwa kuwa kwa vitendo hivyo anavyovifanya Magu ni sawa na kuichimbia kaburi CCM na vitendo hivyo vinafanyika huku wananchi wakiwa wanaviona na "hasira" yao wataionyesha kwenye sanduku la kura ifikapo Novemba 26 mwaka huu