Je, Rais Magufuli anaizika kaburini CCM?

Je, Rais Magufuli anaizika kaburini CCM?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,076
Maana kubwa ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi nchini ni kujibizana kwa hoja. Hiiyo maana yake ni kuwa kama wapinzani wanaikosoa serikali kwa jambo fulani, ni wajibu wa Chama kinachounda serikali kujibu kwenye majukwaa ya kisiasa hoja hizo.

Kwa bahati mbaya sana hiyo dhana imetoweka tokea serikali hii ya CCM awamu ya 5 imeingia madarakani na badala yake ni yeye Magufuli pekee ambaye "amejiona" ndiye mwenye haki za kuzunguka nchi nzima na kukinadi chama chake na kuwaaambia wapinzani, eti wao wasubiri mwaka 2020 ndipo wafanye kampeni zao!

Yeye Magufuli anaamini kuwa hiyo ONE MAN SHOW yake ndiyo itakayoivusha salama CCM

Anajidanganya kupita kiasi, kwa kuwa hiyo staili yake ya uongozi ndiyo anaichimbia kaburi CCM!

Hata hivyo wananchi wanaona uonevu huo na wataamua kuonyesha "hasira" zao kupitia sanduku la kura, ambayo ni SIRI kuanzia Novemba 26, kwenye chaguzi ndogo za kuziba nafasi za madiwani zilizoachwa wazi nchi nzima.

Tumeshuhudia pia Magu akifanya upendeleo wa wazi katika hotuba zake. Alipokuwa Mwanza hivi karibuni aliwaambia wakazi wa huko kuwa "wasibomoleshwe" nyumba zao kwa kuwa CCM inayo "human face" na hao wakazi wa Mwanza ndiyo waliomchagua!

Kwa kauli hiyo pekee Rais ameonyesha "double standard" ya hali ya juu, kwa kuwa wapo wakazi kwa maelfu waliobomolewa nyumba zao bila kulipwa fidia yoyote, kuanzia Kimara hadi Kiluvya kwa kuwa wakazi hao wameichagua Chadema kwenye uchaguzi mkuu 2015!

Pia ziko "double standard" nyingine anazofanya Magufuli.

Wakati maelfu ya watumishi wa serikali wameachishwa kazi kwa kile kinachoitwa kuwa na vyeti feki, lakini zoezi hilo "lilipomgusa" Mkuu wa Mkoa wa Dar, tulimsikia Magufuli akisema kuwa huyo kijana "wake" amekuwa "spared" kwa kuwa hata kama hajui hata kusoma A lakini kwa kuwa anamkamatia wauzaji wa madawa ya kulevya, basi huyo ndiye RC bora kabisa nchini na kwake yeye, huyo RC vyeti feki havimuhusu!

Magu pia ameonyesha "double standard" nyingine kubwa.

Wakati serikali yake ikijinadi kuwa ina zero tolerance linapokuja suala la rushwa, lakini akina Gobless Lema na Joshua Nasari walipoonyesha ushahidi wa rushwa jinsi DC wa Arumeru Alexander Mnyeti "alivyowanunua" madiwani wa Chadema kujiunga na CCM ndiyo kwanza amempa promotion DC huyo na kuwa RC wa mkoa wa Manyara!

Ni wazi kuwa kuwa kwa vitendo hivyo anavyovifanya Magu ni sawa na kuichimbia kaburi CCM na vitendo hivyo vinafanyika huku wananchi wakiwa wanaviona na "hasira" yao wataionyesha kwenye sanduku la kura ifikapo Novemba 26 mwaka huu
 
Umeandika Kwa hisia Kali sana
Mpaka niliyesoma nimeumia.God knows our Tomorrow. Let us wait
Huo ndiyo ukweli wenyewe, as far as kura ni SIRI na unapopiga kura hakuna kitu kinachoitwa "pyupyu" basi nategemea CCM watadondokea pua!
 
mimi naomba tusiseme tumeibiwa kura tuu wakati ukiwadia,kwasababu tatizo kubwa la kila siku na chaguzi zotee hamtaki kulitafutia ufumbuzi badala yake kila siku mnaota ndoto ya CCM kufa.
Lakini na sisi tunaombea akipatikana mshindi kusiwe na "kusuasua" kumtangaza!
 
Lakini na sisi tunaombea akipatikana mshindi kusiwe na "kusuasua" kumtangaza!
As long as Magufuri ni mshindi kusuasua kunatokea wapi??

Pambaneni kwenye Ubunge sio Uraisi kwa sasa,bunge ndo kila kitu,wenzenu Uganda wanapigana hadi Bungeni hii ndio nguvu ya bunge. Pambaneni kuitoa CCM bungeni sio kwenye Uraisi huko bado sanaaa
 
Uoga.com
Wa kujua upinzani kwishney wala hauna lolote maana wapo kama wapiga story chini ya mwembe.

Nchi inataka upinzani tofauti na uliopo.. usio wa wenye tamaa ya kujaza mifuko na matumbo yao tu.. bali ya kujali wananchi na sio kulialia huku hawana hoja hata ya sekunde..

Vimikutano vyao vyenyewe wanapoenda ni outing kwa wanaoenda kuwaangalia hizo sura zao za upinzani mchofu wenye viongozi wachovuuuuuuu.. hakuna kura hapo.. hivyo msilie

Kiongozi wa upinzani anamficha anayetakiwa kuhojiwa juu ya jambo walilomtendea anakwenda bungeni kuulizia hayo hayo.. eti mambo hayaendi.. kituko cha karne zote duniani

Magufuli ni kiboko yao ndio maana mnabwabwaja ovyo juu yake.. na bado juzi alisemaje???.. eeeeeeh
 
Msema kweli ni Novemba 26.....

Usije likimbia hili jukwaa letu wewe binti?
 
CCM utapata viti vingi vya udiwani,hakuna mtu anahangaika na huu upinzani wa kipumbavu wa akina sumaye kingunge nyalandu mbowe na kubwa la mafisadi lowassa,bora ya CCM aisee kuliko hiyo NGO ya wachaga
Ala kumbe mtu anakuwa fisadi akishajiunga Chadema??

Akiwa bado yupo CCM anakuwa ni mtu safi kabisa??
 
Naweza kufanananisha ccm na mithili ya mnyama aitwaye x....! Ukitaka kumchinja unampa kamba ya kutosha ili ajinase mwenyewe halaf ukishamchinja unamkaanga kwa mafuta yake mwenyewe na kumla kwa pilipili nyingi sana......!
 
nilivyomuona akibabaika kujibu swali la mwandishi Uganda niliskitika sana,exposure ni jambo muhimu sana..mtu anakuambia haki za binadamu siyo kitu cha msingi,so sad nchi imeenda kushoto hii
 
Tuliishasema sana humu kuwa, waTz ni wadhaifu sana kwa mambo makubwa!
Hivi hakuna mtu anayeweza kuanzisha chama cha upinzani "cha maana" kuliko hivi vilivyopo sasa vyenye sura ya ukanda, ukabila na uchumia tumbo?

Furaha yangu kwa sasa juu ya upinzani haipandi kama ilivyokuwa ikipanda wakati wa dr. Slaa.

Lakini mlivyoweza kumnunua mzee yule, basi vyama vyote vya upinzani nchini vimebakia ni vijiwe vyenye sura ya wapigadili kwa maslahi ya vikundi vyao na matumbo yao tu.
 
nilivyomuona akibabaika kujibu swali la mwandishi Uganda niliskitika sana,exposure ni jambo muhimu sana..mtu anakuambia haki za binadamu siyo kitu cha msingi,so sad nchi imeenda kushoto hii
Yeye akishasema amepata mialiko isiyopungua 60 ya kwenda nchi za nje, lakini haendi!

Kisa eti akienda nje, huku nyuma watu watapiga dili!

Ina maana hata wasaidizi wake wakuu, VP na PM nao hawaamini kwa kuwa ni miongoni ya wapiga dili??
 
Tuliishasema sana humu kuwa, waTz ni wadhaifu sana kwa mambo makubwa!
Hivi hakuna mtu anayeweza kuanzisha chama cha upinzani "cha maana" kuliko hivi vilivyopo sasa vyenye sura ya ukanda, ukabila na uchumia tumbo?
Furaha yangu kwa sasa juu ya upinzani haipandi kama ilivyokuwa ikipanda wakati wa dr. Slaa.
Lakini mlivyoweza kumnunua mzee yule, basi vyama vyote vya upinzani nchini vimebakia ni vijiwe vyenye sura ya wapigadili kwa maslahi ya vikundi vyao na matumbo yao tu.
Hivyo vyama ambavyo ni "useless" mbona mnavigwaya hadi kuvinyima mikutano ya kisiasa??

Hizo ndiyo propaganda zenu wana-Lumumba

Hivi vyama visivyo na dira ndiyo mngehangaika navyo hadi viongozi wake kuwapiga "pyupyu" ??
 
Tuliishasema sana humu kuwa, waTz ni wadhaifu sana kwa mambo makubwa!
Hivi hakuna mtu anayeweza kuanzisha chama cha upinzani "cha maana" kuliko hivi vilivyopo sasa vyenye sura ya ukanda, ukabila na uchumia tumbo?
Furaha yangu kwa sasa juu ya upinzani haipandi kama ilivyokuwa ikipanda wakati wa dr. Slaa.
Lakini mlivyoweza kumnunua mzee yule, basi vyama vyote vya upinzani nchini vimebakia ni vijiwe vyenye sura ya wapigadili kwa maslahi ya vikundi vyao na matumbo yao tu.
kama hivyo vyama mnavyoviita dhaifu vinawapelekesha mpaka mnategemeo mbeleko la policcm na kununua kina propesa je vikija kama hivyo unavosema itakuwaje?si watarishiwa mabomu kabisa maana risasi sasa hivi zatumiaka shehe wangu...mmmejawa uoga tu kuwazuia watu wasifanye siasa na kujidanganya eti upinzani umekufa
 
Back
Top Bottom