Serikali ya Amerika itakuwa ina undugu na Lucifer. Kwani hiyo hali ya Venezuela kiuchumi aliyeisababisha ni nani kama si yeye? Nchi haina chakula kabisa, raia wa Venezuela wanashinda njaa kama nchi ipo kwenye vita. Venezuela ina utajiri mkubwa kabisa, utajiri wa mafuta na utajiri wa madini. Kuna ripoti moja ya Marekani ya mwaka 1993, jiolojia wa Amerika walienda kufanya tafiti Venezuela. Tafiti ikatoka kwamba Venezuela ina utajiri wa madini mengi kwa kiasi chake.
Amerika kama kawaida yake akautaka huo utajiri Venezuela akakaza. Amerika akajaribu mpaka njia za mapinduzi akashindwa. Akafanya ya kwake ndiyo haya yaliyotokea. Nchi ina utajiri wa mafuta mengi na madini mengi halafu unaambiwa kuna baa la njaa. Kuna kumbukumbu moja niliisoma kuhusu Mzungu mmoja miaka ya zamani sana hapa Tanzania na sijui huyo mzungu alikuwa ni raia wa wapi. Aliwekeza Shinyanga huko kwenye mgodi na aliwapenda wafanyakazi wake. Laa haulaa! Hao Wazayuni wanaomiliki biashara ya madini huko Mataifa makubwa wakamtaka jamaa awauzie mgodi, jamaa akakaza. Kilichotokea maduka yote yanayofanya biashara ya madini yakatonywa yasinunue madini ya jamaa. Yaani madini yanakosa soko hayanunuliwi lakini ni ya kwake tu. Mwisho wa siku alifilisika na akafa.
Ila matikiti maji kama kawaida yao yatakuja hapa na kuandika kilochoua uchumi wa Venezuela ni ujamaa kama western media zinavyokazia. Serikali ya Marekani kwa hapo ilipofikia inabidi iambiwe basi, uliyoyafanya unabidi ukae kimya sasa.