Je, Polepole ndani ya CCM atasimamia kile anachoamini au asichoamini?

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,943
2,000
Sote tunajua umaarufu wa ndugu Polepole umekuja baada ya misimamo yake iliyotokana na rasimu ya katiba mpya ambayo kimsingi inakizana kwa kiasi kikubwa na chama chake. Tujiulize kama hatakuwa mnafiki atahubiri nini ndani ya chama chake?. Ni mabadiliko gani makubwa atayafanya ndani ya chama chake?. Naamini Polepole alimaanisha kile alichokisema wala haikuwa njaa kama wengi wanavyosema. Mabadiliko ya kweli ni kusimamia kile unachohubiri:
1. Serikali 3
2. Kupunguza kwa madaraka ya rais
3. Nafasi za wakuu wa wilaya & Mkoa hazina tija hivyo zifutwe.
3. Ukomo wa ubunge
4. Mawaziri wasitokane na wabunge
5. Tume huru. Na mengine mengi.
 
Nondoh

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
303
500
Watu wanabadili dini sembuse misimamo ya utawala. Je hujawahi ona au sikia Mchungaji kaslim au shekhe kaokoka... Labda utuambie haupo Tanzania hii. Hebu jiulize huyo polepole Ana vyanzo gani vya mapato au vitegauchumi vitakavyo mpa kiburi asimamie kile anacho kiamini?
 
Biashara Mtaji

JF-Expert Member
Aug 19, 2016
324
500
Njaa mbaya sana kama angekuwa mjanja mwenye msimamo na mwenye kusimamia mamuzi yake na msimamo angekataa ukuu wa wilaya alio teuliwa ila kwa Njaa na kutakuwa na msimamo kakubali hivyo usitarajii chochote katika hayo
 
Jozi 1

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
6,203
2,000
Sote tunajua umaarufu wa ndugu Polepole umekuja baada ya misimamo yake iliyotokana na rasimu ya katiba mpya ambayo kimsingi inakizana kwa kiasi kikubwa na chama chake. Tujiulize kama hatakuwa mnafiki atahubiri nini ndani ya chama chake?. Ni mabadiliko gani makubwa atayafanya ndani ya chama chake?. Naamini Polepole alimaanisha kile alichokisema wala haikuwa njaa kama wengi wanavyosema. Mabadiliko ya kweli ni kusimamia kile unachohubiri:
1. Serikali 3
2. Kupunguza kwa madaraka ya rais
3. Nafasi za wakuu wa wilaya & Mkoa hazina tija hivyo zifutwe.
3. Ukomo wa ubunge
4. Mawaziri wasitokane na wabunge
5. Tume huru. Na mengine mengi.
Mabadiliko huja kwa wenye mawazo na mtizamo tofauti kusimamia kidete mawazo yao na ndoto zao.
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,757
2,000
Suala lililopo mbele ya awamu hii ni kupeleka katiba pendekezwa ili ikapigiwe kura ya ndio au hapana na wananchi.
Kwa hiyo Polepole hana sababu ya kubadilia au kutobadili msimamo wake.
Cha msingi ni Kuwa na kambi mbili za ndio au hapana.
Anaweza pia akaikataa kwenye kura.
Hata ndani ya CCM wengi walikua wametoa maoni yao kwa Warioba lakini njaa na michuano ya madaraka iliwabadilisha.
 
Drifter

JF-Expert Member
Jan 4, 2010
2,298
2,000
Sote tunajua umaarufu wa ndugu Polepole umekuja baada ya misimamo yake iliyotokana na rasimu ya katiba mpya ambayo kimsingi inakizana kwa kiasi kikubwa na chama chake. Tujiulize kama hatakuwa mnafiki atahubiri nini ndani ya chama chake?. Ni mabadiliko gani makubwa atayafanya ndani ya chama chake?. Naamini Polepole alimaanisha kile alichokisema wala haikuwa njaa kama wengi wanavyosema. Mabadiliko ya kweli ni kusimamia kile unachohubiri:
1. Serikali 3
2. Kupunguza kwa madaraka ya rais
3. Nafasi za wakuu wa wilaya & Mkoa hazina tija hivyo zifutwe.
3. Ukomo wa ubunge
4. Mawaziri wasitokane na wabunge
5. Tume huru. Na mengine mengi.
Mkuu, Chama kina misingi yake ambayo ndiyo inayofuatwa na wanachama na kusimamiwa na watendaji wake. Kwa kukubali uteuzi wake ndani ya Chama tayari mh. Polepole analazimika kusimamia misingi ya Chama. Hiyo ni hesabu ya 1+1=2. Mjadala kama yeye ni mnafiki au vipi, haupo tena.
 
lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,943
2,000
Mawazo yote ni mazuri, lakini tujiulize kwanini ateuliwe mtu mwenye mtizamo na misimamo tofauti na chama? Hatuoni hata kama atatekeleza sera za chama bado kutakuwa na kaugumu fulani. Je, ndani ya chama hakuna mtu mwingine asiye na doa? Kwa upande wa pili kwanini tusifikiri ameteuliwa yeye ili alete mabadiliko katika chama hasa kwa yale anayoyaamini?
 
lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,943
2,000
Mkuu, Chama kina misingi yake ambayo ndiyo inayofuatwa na wanachama na kusimamiwa na watendaji wake. Kwa kukubali uteuzi wake ndani ya Chama tayari mh. Polepole analazimika kusimamia misingi ya Chama. Hiyo ni hesabu ya 1+1=2. Mjadala kama yeye ni mnafiki au vipi, haupo tena.
Unafikiri ni kitu gani husababisha siri za chama kutoka kama sio watu kama hawa ambao kuna mambo huwa hawakubaliani nayo! Madhalani kikao cha chama cha watu 10 tu, bila hata mwandishi wa habari hata 1 kuwemo, pamoja na mikwala kuzuia kutoa taarifa kesho yake mambo yote yaliyojadiliwa yako kwenye magazeti!
 
lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,943
2,000
Suala lililopo mbele ya awamu hii ni kupeleka katiba pendekezwa ili ikapigiwe kura ya ndio au hapana na wananchi.
Kwa hiyo Polepole hana sababu ya kubadilia au kutobadili msimamo wake.
Cha msingi ni Kuwa na kambi mbili za ndio au hapana.
Anaweza pia akaikataa kwenye kura.
Hata ndani ya CCM wengi walikua wametoa maoni yao kwa Warioba lakini njaa na michuano ya madaraka iliwabadilisha.
Sio rahisi kama unavyofikiri!! Kabla ya kuipigia kura kutakuwa na kampeni kuwashawishi wananchi waipigie Ndiyo au Hapana? Yeye kama Katibu mwenezi atasimama jukwaani kupingana na kile alichokuwa akikihubiri? Atawashawishi vipi wananchi kuhusu uzuri au ubaya wa hiyo rasimu! Tutegemee sasa Polepole asimame jukwaani atetee serikali 2!! Aibu!!
 
Nyangomboli

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
3,200
2,000
Kamuulizeni kwanza mgombea wenu ni nini msimamo wake kuhusu katiba au rasimu ya Mzee JS?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom