POTOSHI Je, pichani ni Maria Sarungi akiwa na Jeffrey Epstein?

POTOSHI Je, pichani ni Maria Sarungi akiwa na Jeffrey Epstein?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu

Nimekutana na hii taarifa huko X ikiambatana na huu ujumbe:

Kumbe maria alikua akiwauza dada zetu huko ughaibuni Ushahidi mzito umeibuka ukionyesha uhusika wa Maria Sarungi katika mafaili yanayohusishwa na kesi ya Jeffrey Epstein. Taarifa zinadai barua pepe kwa Epstein zilihusisha Miss Universe Tanzania katika biashara haramu.
Epstein 2.jpg
 
Tunachokijua
Jeffrey Epstein ni raia wa Marekani ambaye anahusishwa na kuwanyanyasa watoto kingongo, ubakaji, na kufanya biashara ya kuuza binadamu ambaye alijulikana pia kutokana na umaarufu wake pamoja ni utajri aliokuwa nao, alifariki Agosti 10, 2019.

Hivi karibuni kumekuwa na nyaraka, picha na video mbalimbali ambazo zinamuonesha Epstein akifanya vitendo hivyo huku akiwa pia na viongozi na watu wengine wengi mashuhuri duniani katika nyakati tofauti tofuti.

Madai

Mdau amehitaji kupata uhalisia wa picha iliyochapishwa Kupitia mtandao wa X ikimuonesha Maria Sarungi akiwa na Epstein pamoja na watu wengine. Picha hiyo imembatanishwa na ujumbe pia unaoeleza kuwa mwanaharakati huyo, anahusika pia katika yaliyotajwa kumuhusu Epstein.

Uhalisa wa Madai hayo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejirirdhisha kuwa picha hiyo imehaririwa kwa teknolojia ya Akili Unde kutoka katika picha ya awali ambayo pia ilitengenezwa kwa akili Unde.

1770298278683-png.3539578

Kwa kutumia nyenzo za kidigitali ikiwemo google reverse image search imebaini kuwa picha hiyo imehaririwa kutoka katika picha ya awali iliyotengenezwa kwa Akili Unde na kumuondoa mtu mmoja ambaye nafasi yake amewekwa Maria Sarungi.
epstein-1-jpg.3539554

Picha ya awali iliyotengenezwa kwa AKili Unde
Katika picha ya awali inamuonesha Diddy, Bill Gates, Jay-Z, Hillary na Bill Clinton, Stephen Hawking pamoja na Epstein mwenyewe, ambapo baada ya ufuatiliaji picha hiyo imeonesha kuwa imetengenezwa kwa AI.
screenshot-2026-02-05-155534-png.3539548
Back
Top Bottom