Je, Nyerere alishindwa kutupatia katiba mpya kabla hajang'atuka?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,150
Mwalimu Nyerere alikuwa ndio mwanaccm wa kwanza kutujuza "ukuu" wa katiba yetu na kwamba inaweza kuwa rafiki au kinyume chake kulingana na matakwa ya kiongozi aliyopo madarakani kwa wakati husika.
Najiuliza kwanini hakufanya mchakato wa ama kuirekebisha au kutupatia katiba mpya?
Ni hilo tu!
 
Sababu alitaka ccm itawale maisha

Hujiulizi uchaguzi wa 1995 kwenye kampeni alisema nini?

"Siwezi kuacha nchi yangu kuangukia mikononi mwa mbwa.

Hata ukiangalia venezuela maduro kamuachia predecessor wake maduro na hakutaka wapinzani wapewe angalia Urusi ,China ambao ni role models wa mwl wanaachiana party kwa party au wenyewe kwa wenyewe

sasa katiba angebadilisha si angewapa nafasi wapinzani "mbwa" kuchukua nchi.
 
Papara za nini? Uwe unahakiki kabla ya kubandika.
 
Sasa mbona wapinzani walipopata fursa ya kuandika katiba mpya walikimbia bungeni wakiongozwa na Prof Lipumba?........ Au ndio waliufyata mkia!
 
Papara za nini? Uwe unahakiki kabla ya kubandika.
Mkuu CCM marafiki zao ni chama cha ukomunisti wa china na chama cha ukomunisti wa vietnam na kama sijakosea Frelimo cha Angola ambao wote sera zao za kijamaa

Na urafiki huo umeundwa kipindi cha nyerere na mpaka leo bado ni ally
.tumeona kinana akienda kwenye chama cha ukomunisti wa china huko china na akiwakaribisha lumumba same kwa polepole na juzi walikuwa Angola kusherehekea miaka ya frelimo

Kama ccm marafiki zao ni hao chama cha ukomunisti wa china,vietnam na frelimo na wanashirikiana mpaka kesho hivyo kurekebisha katiba kukuachia mpinzani kiupenyo sahau..tizama frelimo na siasa za Angola,tizama china ni chama kimoja tu na vietnam ambao ni role models wa ccm

So nipo sahihi ..

Nipo tayari kukosolewa
 
Mwalimu Nyerere alikuwa ndio mwanaccm wa kwanza kutujuza "ukuu" wa katiba yetu na kwamba inaweza kuwa rafiki au kinyume chake kulingana na matakwa ya kiongozi aliyopo madarakani kwa wakati husika.
Najiuliza kwanini hakufanya mchakato wa ama kuirekebisha au kutupatia katiba mpya?
Ni hilo tu!
Alirekebisha hiyo katiba mwaka 1984 kwa kuweka vipengele vya haki za binadamu, vikomo vya mihula ya uongozi na kuondoa sheria ya kuwekwa kizuwizini.
 
Nyerere alikuwa mbinafsi kama walivyo watawala wengi waliomfuata!! Kwa kinywa chake alishakiri ubovu wa katiba yetu.

Utakuta hata walimu waliokufundisha kuandika walipata elimu ya bure kwa sababu ya Mwalimu.

Mkuu CCM marafiki zao ni chama cha ukomunisti wa china na chama cha ukomunisti wa vietnam na kama sijakosea Frelimo cha Angola ambao wote sera zao za kijamaa

Na urafiki huo umeundwa kipindi cha nyerere na mpaka leo bado ni ally
.tumeona kinana akienda kwenye chama cha ukomunisti wa china huko china na akiwakaribisha lumumba same kwa polepole na juzi walikuwa Angola kusherehekea miaka ya frelimo

Kama ccm marafiki zao ni hao chama cha ukomunisti wa china,vietnam na frelimo na wanashirikiana mpaka kesho hivyo kurekebisha katiba kukuachia mpinzani kiupenyo sahau..tizama frelimo na siasa za Angola,tizama china ni chama kimoja tu na vietnam ambao ni role models wa ccm

So nipo sahihi ..

Nipo tayari kukosolewa

Haya bana.
 
Nyerere alikuwa akiadvocate mabadiriko ya mambo ya msingi baada ya yeye kuondoka ktk nyadhifa fulani au kama alikuwa anajua soon ataondoka!, hakuwa genuine kwenye baadhi ya mambo mengi ya msingi.
Kwa mfano

1. Alikataa kuingiza bill of human rights kwenye katiba kwa miaka mingi ila akaiingiza mwaka 1984 ili kumbana atakayekuja

2. Aliweka term limits, kumuwekea ambaye angemrithi

3. Aliadvocate kurudi vyama vingi mwaka 1992 baada ya kuwa ameng'atuka nafasi zote za Uraisi na ile ya uenyekiti wa CCM mwaka 1990, kabla ya hapo alikuwa kanyuti tu

Nyerere siyo Reformist, alikuwa anajua sana kuwa hii katiba ni mbaya, na alikiri hivyo lakini hakuwa na Ujasiri wa kuibadiri
 
Mkuu CCM marafiki zao ni chama cha ukomunisti wa china na chama cha ukomunisti wa vietnam na kama sijakosea Frelimo cha Angola ambao wote sera zao za kijamaa

Na urafiki huo umeundwa kipindi cha nyerere na mpaka leo bado ni ally
.tumeona kinana akienda kwenye chama cha ukomunisti wa china huko china na akiwakaribisha lumumba same kwa polepole na juzi walikuwa Angola kusherehekea miaka ya frelimo

Kama ccm marafiki zao ni hao chama cha ukomunisti wa china,vietnam na frelimo na wanashirikiana mpaka kesho hivyo kurekebisha katiba kukuachia mpinzani kiupenyo sahau..tizama frelimo na siasa za Angola,tizama china ni chama kimoja tu na vietnam ambao ni role models wa ccm

So nipo sahihi ..

Nipo tayari kukosolewa
frelimo iko msumbiji na siyo angola.
 
Mwalimu Nyerere alikuwa ndio mwanaccm wa kwanza kutujuza "ukuu" wa katiba yetu na kwamba inaweza kuwa rafiki au kinyume chake kulingana na matakwa ya kiongozi aliyopo madarakani kwa wakati husika.
Najiuliza kwanini hakufanya mchakato wa ama kuirekebisha au kutupatia katiba mpya?
Ni hilo tu!
Kwani ile ya 1977 alitupatia nani? na je haikuwa mpya?
 
frelimo iko msumbiji na siyo angola.
Asante kwa usahihisho ni MPLA ambacho kina mlengo wa kijamaa tokea uhuru mpaka leo wanaongoza wao tu na hata hao Frelimo wana mlengo wa kijamaa kama ccm tokea uhuru mpaka leo wanaongoza wao tu.
 
Tumwache Nyerere apumzike alishafanya kazi yake kubwa sana,alituachia madini tuchimbe tukipata akili wanafaidika wachache na angeweza kufanya lolote kina makongoro,madaraka wakawa wanamiliki migodi tanzanite,almasi,gold etc,sioni sababu ya kumlaumu kuhusu katiba babu kwasababu aliamini kuongezeka kwa wasomi kutaleta mapinduzi,headline yako ingesomeka wasomi wetu wametuangusha ningekuelewa mkuu,ila Nyerere JK unamuonea tu
 
Nyerere kwa hili simuelewi kabsaa. Alitaka CCM wasilale, wasibweteke LAKINI hakutaka CCM itoke madarakani, hivyo alihakikisha anatuachia hili likatiba la hovyo kabisa akijua kwamba linaweza wa kuzalisha madikiteta (hili alisema yeye mwenyewe) na mambo mengine ya hovyo kama mshindi wa uraisi akisha tangazwa basi hata mahakama haiwezi kulijadili hilo.
Na awamu hii ndiyo tunayaona mengi yanatimia-fikiria kule KOROGWE vyama vya upinzani tunaambiwa na TUME YA UCHAGUZI kwa masaa yasiyopungua matano vilishindwa kujua formu za wagombea wao zilrudishwa kwa nani na ofisi gani. KINONDONI mawakala wa Upinzani mpaka jioni ya mkesha wa uchaguzi hawana vitambulisho lakini wa CCM wanavyo.
Kiama cha wapinzani (sijui kama ni wao peke yao) ni 2019 na 2020-na sheria mpya ya Vyama vya Siasa ndiyo inatuletea USTARABU aina hiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom