Je, Nyerere alikuwa nyuma ya Mapinduzi ya Zanzibar, au Okello alikuwa peke yake kweli?

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Habarini wadau

Nimekuwa nikifuatilia sana Historia ya Zanzibar siku za karibuni

Kuna sehemu nilisoma kuwa anae enziwa kuwa ni baba wa mapinduzi Sheikh Aman Karume hakuwa anahusika kwa kiasi kikubwa na mapinduzi hayo na siku ya Mapinduzi alikuwa bara

aliyepanga na kutekeleza mapinduzi yake alikuwa ni John Okello, mwenye asili ya Uganda na baafa ya mapinduzi kufanyika alimuita Karume kutoka bara na kumfanya kuwa Rais huku yeye akijipa cheo cha Field Marshal

Lakini leo nimekuja kusoma mahali tena wanasema Karume na Nyerere ndio waliohusika na mapinduzi yale nyuma ya pazia, na kuwa huyu Okello walimtumia tu na baadae wakamtema kisha wakaunda Muungano

Sasa nashindwa niamini lipi japo hilo la pili ndio lina make sense kidogo

Wana Historia naomba msaada
CC Mohamed Said Pascal Mayalla Yericko Nyerere barafu Nguruvi3 Mag3
 
King8ne cha kutafakuri kuhusiana na Zanzibar ni kwamba utapata historia nyoofu kwa utawala wa sultan japo ni version yao but atleast watazungumzia ukweli wao kwa mazuri yqo na kuficha mabaya but historia ya mqpinduzi utqpewa ukweli mbadala mwanzo mwisho hakuna kiti cha kueleweka njia pekee ni kuvichoma vitabu kwa mboni za macho yako then uanze kuunganisha dot kwa vitqbu na simulizi za mdomo ndio utapata mwanga.
Binafsi nipo katikati ya historia yq nchi zetu mbili hizi ila kwanza nimejikita kwa kuuawa kwa Mwanamapinduzi Karume na wauaji baadhi kuuliwa on the spot na waliokamatwa nao kuuawa bila kuhojiwq na aluyetoa amri ya kuuawa kwa wayqji nae kukamatwa kuletwa Dar es salaam na then kuamriwa kuhama nchi kwa nchi ya msumbiji kupewa zawadi ya komandoo yule aliyeongoza operation ya kukamata wauaji wa rais .
Hizi ndio aina historia zetu unapewa kile wanachotaka wao the whole truth upite mitaani na kujiongeza na vitabu ila hutopata njia ya kuamini maneno yao maana historia zetu zina mirengo ya kisiasa sana !
Nakutakia mawindo mema ya historia tutabadilishana notes
 
Kitafute hiki kitabu...
FB_IMG_1532788088683.jpeg
 
Habarini wadau

Nimekuwa nikifuatilia sana Historia ya Zanzibar siku za karibuni

Kuna sehemu nilisoma kuwa anae enziwa kuwa ni baba wa mapinduzi Sheikh Aman Karume hakuwa anahusika kwa kiasi kikubwa na mapinduzi hayo na siku ya Mapinduzi alikuwa bara,

aliyepanga na kutekeleza mapinduzi yake alikuwa ni John Okello, mwenye asili ya Uganda na baafa ya mapinduzi kufanyika alimuita Karume kutoka bara na kumfanya kuwa Rais huku yeye akijipa cheo cha Field Marshal

Lakini leo nimekuja kusoma mahali tena wanasema Karume na Nyerere ndio waliohusika na mapinduzi yale nyuma ya pazia, na kuwa huyu Okello walimtumia tu na baadae wakamtema kisha wakaunda Muungano

Sasa nashindwa niamini lipi japo hilo la pili ndio lina make sense kidogo

Wana Historia naomba msaada
CC Mohamed Said Pascal Mayalla

Uongozi wa Sheikh Moh'D Shamte wa Pemba ulitolewa madarakani kwa hila za Karume akishirikiana na watu wa bara. Ilijengwa dhana kuwa waswahili kutokana na weupe wao na kwa kuwa ni minority kwa wakti huo hawakuzidi elfu 65 walikuwa ni warabu. Lakini ukweli ni kuwa waswahili ni zao la mchanganyiko la warabu na waswahili.
Pia kwa kuwa walikuwa wengi wanatokea Pemba basi wakafanyiwa hila na kina Karume kwa njia za ubaguzi wa rangi wakapinduliwa madarakani. Ila kwa kuwa hawa walichaguliwa kihaki kabisa kwenye uchaguzi wa 1961 nadhani basi kupindua nchi lilikuwa jambo la kihaini.. Lile kundi la kina Karume, Babu na wengine walienda Bara na kumuacha Okello kwa sababu walikuwa waoga na hawakuwa na mafunzo thabiti ya kijeshi.
Okello alitolewa Zanzibar kupitia bara baada ya kukamilisha mapinnduzi ya kumtoa mPemba kama kiongozi wa Zanzibar na kumueka Karume ambaye ni mweusi. Okello aliitwa Bara na Mwalimu kisha akazungukwa akawekwa kwenye ndege na huo ndo ukawa mwisho wake.. Alishangaa ametua Entebe ghafla.

Hila ile na kinyongo hakijawatoka wapemba toka enzi zile mpaka leo.. Nje ya muungano hakuna Zanzibar bali ni Pemba na Unguja.. Zanzibar itakuwepo endapo tuu Muungano upo. Wapemba wanataka uongozi na mamlaka kamili waitawale Zanzibar.. Hawa waswahili idadi yao imeongezeka kwa kasi sana kwa kuzaliana na watu wengi weusi walirudi Bara. Kwa sasa inasemeka ndio wengi na ndio hao waliitaka CUF ambayo ina asili ya chama cha Moh'd Shamte Hamadi. Kwa idadi yao ni fika kila uchaguzi lazima watashinda tuu.

Nikiiangalia Zanzibar kwa mahali flani Nakubaliana na mtu aliesema kwamba nchi za kijamaa kabla ya kuvunjika Umoja wa Soviet ziliiona Zanzibar kama mahali pazuri pa kuuendeleza ujamaa na sehemu yenye jiografia nzuri kieneo kwa ajili ya masuala ya kijeshi ili kumpunguza nguvu Adui ya mkubwa aliekuwa nchi za kibepari..Sasa ukiangalia miaka ya 70 Mwalimu nyerere alienda marekani kumwona jf Kennedy,,,nikajiuliza kulikuwa na uhusiano gani wa ujamaa na ubepari,,,kwa nini Nyerere asiende china,,Russia,,n.Korea,,Hungary na nchi nyingine za kijamaa,,,sasa wazo la kuiunganisha Zanzibar na tanganyika ni ili kutekeleza mawazo yenye hofu ya wazungu kwamba Zanzibar isije ikawa sehemu ya kufanikisha mipango ya kijamaa kwa hio kuondokana na huo wasiwasi na isitoshe tanganyika ishakuwa puppet wa wazungu basi iimeze na Zanzibar ili wawe na tanganyika kwenye kamba moja.Ndipo nikaamini kuiunganisha tanganyika na Zanzibar halikuwa wazo la mwalimu ila alipewa kama kazi aifanye kwa makubaliano flani.
 
Ukitaka kujipunguzia kujiuliza ungeanza kutafiti kwa nini " Mwanamapinduzi"Okello "alimtunuku"urais Marhum Sheikh Abeid A.Karume na kwa nini siku hiyo Sheikh Karume awe bara.
Kuhusu kwa nini Okello alitemwa na "wageni"wake hiyo ni hoja nyingine kwa siku nyingine
Karume ndio alikuwa kiongozi wa ASP ambayo Okello alikuwa mwanachama, so aliona mtu aliyeiva kisiada mwenye uwezo zaidi wa kuiongoza Zanzibar ni Karume

Kuhusu kwa nini Karume alikuwa bara siku ya Mapinduzi, sijajua ila inaweza kuwa ni coincidence tu

Na hoja ya kuhusu Okello kutimuliwa Zanzibar, nasikia jamaa alikuwa kama chizi, au alikuwa na wenge sana na alikua haendani na Zanzibar ya Waswahili Waislam huku yeye akiwa ni Mganda halafu Mkristu, Karume akaona atamsumbua akamfungia asirudi tena Zanzibar

Vyanzo vyangu ndio vinavyonuambia, nipo tayari kusahihishwa
 
Uongozi wa Sheikh Moh'D Shamte wa Pemba ulitolewa madarakani kwa hila za Karume akishirikiana na watu wa bara. Ilijengwa dhana kuwa waswahili kutokana na weupe wao na kwa kuwa ni minority kwa wakti huo hawakuzidi elfu 65 walikuwa ni warabu. Lakini ukweli ni kuwa waswahili ni zao la mchanganyiko la warabu na waswahili.
Pia kwa kuwa walikuwa wengi wanatokea Pemba basi wakafanyiwa hila na kina Karume kwa njia za ubaguzi wa rangi wakapinduliwa madarakani. Ila kwa kuwa hawa walichaguliwa kihaki kabisa kwenye uchaguzi wa 1961 nadhani basi kupindua nchi lilikuwa jambo la kihaini.. Lile kundi la kina Karume, Babu na wengine walienda Bara na kumuacha Okello kwa sababu walikuwa waoga na hawakuwa na mafunzo thabiti ya kijeshi.
Okello alitolewa Zanzibar kupitia bara baada ya kukamilisha mapinnduzi ya kumtoa mPemba kama kiongozi wa Zanzibar na kumueka Karume ambaye ni mweusi. Okello aliitwa Bara na Mwalimu kisha akazungukwa akawekwa kwenye ndege na huo ndo ukawa mwisho wake.. Alishangaa ametua Entebe ghafla.

Hila ile na kinyongo hakijawatoka wapemba toka enzi zile mpaka leo.. Nje ya muungano hakuna Zanzibar bali ni Pemba na Unguja.. Zanzibar itakuwepo endapo tuu Muungano upo. Wapemba wanataka uongozi na mamlaka kamili waitawale Zanzibar.. Hawa waswahili idadi yao imeongezeka kwa kasi sana kwa kuzaliana na watu wengi weusi walirudi Bara. Kwa sasa inasemeka ndio wengi na ndio hao waliitaka CUF ambayo ina asili ya chama cha Moh'd Shamte Hamadi. Kwa idadi yao ni fika kila uchaguzi lazima watashinda tuu.

Kwa hiyo mkuu Okello ilikuaje hadi akafika Zanzibar na kwenda kupindua?
Kulikuwa na nguvu ya Nyerere nyuma ya Okello?
 
Nikiiangalia Zanzibar kwa mahali flani Nakubaliana na mtu aliesema kwamba nchi za kijamaa kabla ya kuvunjika Umoja wa Soviet ziliiona Zanzibar kama mahali pazuri pa kuuendeleza ujamaa na sehemu yenye jiografia nzuri kieneo kwa ajili ya masuala ya kijeshi ili kumpunguza nguvu Adui ya mkubwa aliekuwa nchi za kibepari..Sasa ukiangalia miaka ya 70 Mwalimu nyerere alienda marekani kumwona jf Kennedy,,,nikajiuliza kulikuwa na uhusiano gani wa ujamaa na ubepari,,,kwa nini Nyerere asiende china,,Russia,,n.Korea,,Hungary na nchi nyingine za kijamaa,,,sasa wazo la kuiunganisha Zanzibar na tanganyika ni ili kutekeleza mawazo yenye hofu ya wazungu kwamba Zanzibar isije ikawa sehemu ya kufanikisha mipango ya kijamaa kwa hio kuondokana na huo wasiwasi na isitoshe tanganyika ishakuwa puppet wa wazungu basi iimeze na Zanzibar ili wawe na tanganyika kwenye kamba moja.Ndipo nikaamini kuiunganisha tanganyika na Zanzibar halikuwa wazo la mwalimu ila alipewa kama kazi aifanye kwa makubaliano flani.
Hiyo pia niliisikia, sababu nyingine nikisikia pia Karume alikuwa akikabiliwa na nguvu kubwa ya Upinzani kutoka chama chama kilichojiita Umma Party, kujilinda kisiasa ikabidi aungane ili kuwamaliza nguvu Wapinzani wake

Lakini hili ni baada ya Mapinduzi, swali langu ni je Nyerere alikuwa nyuma ya haya Mapinduzi kweli au alikuwa ni Okello pekee?
 
Nyerere aliivamia zanzibar kijeshi january 1964,hakuna lugha nyengine ya mkato hapo.
 
Karume pamoja na Nyerere walishiriki kikamilifu katika mapinduzi ..okello alitumika kama chambo..baada ya mapinduzi okello akatemwa nje ya boksi...

Mbeleni karume akazidiwa ujanja na Nyerere ...karume akajaribu kuescape makubaliano ndio yakamkuta ya kumkuta
 
Hivi Karume na Nyerere ndio walimuagiza Okello kuchinja Waarabu na Wahindi kama kuku baada ya Serikali kupinduliwa au alijiamulia mwenyewe tu
 
Okello alitumika tuu kama daraja, sababu uwezo alikua nao wa kufanya hivyo...

Ila kilichomponza ni tamaa zakena ile kua siyo Raia wa either bara au visiwani ndiyo maana wakamtimua kuogopa kugeukwa muda wowote...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom