Je nisome PCB au PCM?

umeshinda bro[emoji38] [emoji38] [emoji38] nimeangalia nimeona wametoa cku hizi, ila sie wa nyuma tulisoma kupitia PCM bro usibishe, ukitaka na vyeti nakuwekea uone,, ila sasa wanataka usome na Bios.[emoji41] [emoji41] [emoji41]
Zamani nakubaliana na wewe ila saivi bila Biology huwezi kusoma Pharmacy.
 

Yaani tuongee tu ule ukweli, mimi nipe chchote hapa duniani nitasoma lakini PCB hiyo ndiyo mwisho wangu wa reli, naiogopa kama ukoma halafu nawavulia kofia wote waliosoma hii kitu na waka-excel !
 
Yaani tuongee tu ule ukweli, mimi nipe chchote hapa duniani nitasoma lakini PCB hiyo ndiyo mwisho wangu wa reli, naiogopa kama ukoma halafu nawavulia kofia wote waliosoma hii kitu na waka-excel !
Kipenda roho tu sio ngumu kama kweli umechagua mwenyewe sio kwa kuchaguliwa
 
Ipo siku ata ukumbuka huu ushauri
 
PCB haruhusiwi kabisa kusogeza pua yake kwenye Engineering.
Ukitaka kuwa Engineer hakikisha Advance unasoma Pure Mathematics, na sio BAM (hesabu za Form Two)
Si kweli, mwaka 2014 baada ya competition kua kubwa kwenye MD kuna vijana nafahamiana nao walichaguliwa Mech na Electrical engineering StJoseph, miaka ya hapa nyuma kidogo mambo yalivurugika sana ila sasa naona wameshaweka sawa kila watu wanapambana na hali zao.
 
Haya mambo ya kusoma, kufauulu na kuishia kukosa chuo au kukosa Ajira kwa sasa yameshakuwa kawaida sana, na unaweza usiamini mpaka yakukute wewe au mtu wako wa karibu.

Kusoma kozi ya PCB kuna future nzuri zaidi huko mbeleni, lakini inabidi muhusika ajipange kwa lolote huko mbele ya safari, maana sera za serikali kwenye udahili zinayumba mnoo kiasi ambacho mwanafunzi wenye ufaulu mzuri wa form six anaweza akakosa chuo hata kama ana division One au Division two.

Mwaka uliopita kuna wanafunzi wenye Division One na Two kibao wamekosa chuo. Kwanini? Changamoto za udahili ziliwazidi. Walikomaa na vyuo fulani fulani na kozi fulani fulani tu, mwisho wa siku wakakosa vyote.

Mtu ana Division One ya point Tisa ya PCB halafu anataka kwenda kusoma Medicine pale MUHAS, kwa mwaka jana haikuwezekana kudahiliwa, anakosa nafasi.
 
Ningependa kuwa daktari special, but kilichonivunja moyo nimeambiwa kwanza inabidi usome udokta wa kawaida MD miaka 5, then ndo uspecialize. Halafu nimeambiwa kuspecialize mpaka nje ya nchi TZ hakuna
Kwenye udaktari hakuna shortcut aisee, ni lazima ukomae miaka isiyopungua mitano kwa hapa Tanzania halafu baada ya hapo ni lazima kisheria upige mazoezi(internship) mwaka mmoja. Kwa baadhi ya nchi kama China, Medicine sio chini ya miaka 6.

Daktari specialist maana yake amesomea master's of Medicine na uwe umefanya mazoezi mwaka mmoja(internship), na kusomea Master's of Medicine ni lazima uwe na Bachelor of Medicine kwanza.
Na kama unataka kuwa Specialist utapaswa kufanya kazi kwa at least miaka miwili kwanza(Japokuwa wapo wanaokwepa hili kwa sasa) ndio uende kuusomea. Kwahapa Tanzania Master's of Medicine huwa ni miaka mitatu kwa vyuo vingi na vichache miaka minne. Kwa nchi kama UK, USA, Canada nk. ni miaka minne na kuendelea.

Sio kweli kuwa kuusomea uspecialist ni lazima uende nje ya nchi. Karibu vyuo vyote hapa Tanzania vinavyotoa kozi ya Medicine basi pia vina kozi mbalimbali za specialist. Na kwa sasa zaidi ya 90% ya madaktari wanaosomea uspecialist wanasoma katika vyuo vya Tanzania.

Na huwezi amini kabisa, katika vyuo vya Tanzania, kuna wageni wengi sana kutoka nchi za nje hususani Afrika wapo wanasimea uspecialist.

Kwa utafiti wangu mdogo katika kuwadadisi madaktari wao wenyewe huwa wanadai kuwa, pamoja na kozi ya medicine na uspecialist kuwa ngumu na za muda mrefu lakini ni TAMU MNOO, INA HESHIMA YAKE YA KIPEKEE SANA KIJAMII, NA MARA ZOTE WANATAMANI SANA HADI WATOTO WAO WAJE KUISOMEA(niligundua pia madaktari wengi wazazi wao walikuwa madaktari au wataalamu wa Afya)
 
Kazi ya Baba inainfluence kazi ya mtoto kwa kiasi kikubwa sana sio tu idara ya afya
 
Naongeza mwaka jana kuna madogo nawajua wamesoma PCB na wapo engineering mmoja yupo Chuo cha maji mwengine Arusha Tech
 
umeshinda bro[emoji38] [emoji38] [emoji38] nimeangalia nimeona wametoa cku hizi, ila sie wa nyuma tulisoma kupitia PCM bro usibishe, ukitaka na vyeti nakuwekea uone,, ila sasa wanataka usome na Bios.[emoji41] [emoji41] [emoji41]
Stay updated...ungeshampoteza dogo wa watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…