Je, nini siri ya mwanamke kitandani na mume wake?

Ukweli si size wala shape wala appearance ya mwanamke ndiyo inayo dhihirisha ufundi wake kitandani bali mtazamo (attitude) kuhusu tendo la ndoa (sex) ndio msingi unaoweza kuelezea mafanikio na kushindwa kitandani.

Kama mwanamke anaamini kufanya mapenzi ni uchafu au ni kitu kibaya au mtazamo wowote potofu katika ndoa hataweza kuleta furaha ya kweli.
Kama anaamini mapenzi katika ndoa ni legalize rape basi hata siku moja hataweza kufurahia mapenzi atakuwa anajiona anabakwa kila siku.


Kama anaamini matiti yake ni madogo sana au makubwa kupita kiasi ambacho hawezi kufurahia kufanya mapenzi ni kweli hataweza kufurahia na anaweza kukosa feelings za kweli kuhusu mapenzi ndani ya ndoa.

Kama anaamini skills zake katika kufanya mapenzi ni pungufu basi hataweza kufurahia raha ya kuwa mwili mmoja.

Kama anaamini mwili wake upo ovyo kiasi kwamba hawezi kuwa uchi mbele ya mume wake basi ni dhahiri faragha na mumewe imeingiliwa.

Katika utafiti ambao ulihusisha wanaume ambao sehemu zao za siri ziliondolewa testicles na wanawake ambao waliondolewa clitoris na kuwachunguza wanavyofanya (enjoy) mapenzi na partners wao; ilikuja kujulikana kwamba walifurahia kufanya mapenzi sawa na wengine ambao wapo salama.
Hii ni kudhihirisha kwamba organs hazikuwa msingi wa wanandoa kufurahia mapenzi bali jinsi wanavyofikiria au mtazamo wao kuhusu tendo la ndoa.

Hii ina maana unaweza kuwa na size, shape na appearance tofauti au yenye hitilafu kwa mtazamo wa jamii lakini ukiwa na mtazamo (binafsi) mzuri kuhusu mapenzi unaweza kufurahia tendo la ndoa kwa njia ya ajabu sana na unaweza kuwa moto kitandani na mumeo kukufurahia.
niaje bwanaaaaa
 
Back
Top Bottom