mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Kwanza tuwe waungwana kumpongeza mkuu wa mkoa DSM kwa juhudi alizoanzisha kwa Udogo au ukubwa wake Kuhusu madawa ya kulevya. Juhudi hizi hata kama zikimsaidia mtanzania mmoja ni faida kwa Maana hata Mexico,Colombia na US vita hivi sio vya magavana bali taifa zima.
Kurudi kwenye mada, Tumekuwa na desturi ya kuwalaumu wengine kwa kuhamahama kwa mawazo na kuwa wasahaulifu wa mambo ya msingi pale linapoibuka jipya. Leo tangu imeibuka hoja ya Madawa tumekimbia hoja yetu ya elimu na mawazo mazuri tuliokuwa tukiyatoa kwa gharama ya madawa.
Hatuoni kama na sisi Tunaojiita Great Thinkers tumechagua kuwa Small Minded?
Hatuoni uwezo wetu wa kujadili jambo zaidi ya moja kwa uzito sawa ni mdogo au haupo kabisa?
Kwa mtazamo wangu: Elimu ni Ufunguo wa maisha, Vijana wakiwa na elimu ya kutosha hata madhara ya Muda mrefu ya Madawa watayajua. Ni pia ni njia mbadala ya kupunguza soko huku dola ikipambana wa upande mwingine.Maana inaaminika mtu akielimika anaongeza uwezo wa kufanya maamuzi kwa kuyachakata kwanza bila mkumbo.
Tunatokaje hapa????