Je nini asili au chanzo cha misemo hii kutumika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je nini asili au chanzo cha misemo hii kutumika?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by vukani, Mar 6, 2010.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kuna baadhi ya misemo inanitatiza, lakini naamini hapa kuna wajuzi wa lugha, ya Kiswahili ambao watanipatia msaada.
  Ninachotaka kujua, Je nini asili au chanzo cha misemo hii kutumika?

  Misemo yenyewe ni hii ifuatayo:

  Haikufua dafu (Msemo huu hutumika zaidi pale mtu anapojaribu kitu kikashidikana, kwa mfano mtu anaweza kuumwa akanywa dawa fulani kisha ikashindwa kufanya kazi, anaweza kusema nimekunywa dawa Fulani lakini haikufua dafu-Tafsiri ni yangu)

  Mungu sio Athumani (Huu msemo nao hutumika pale mtu anapokuwa amefanikiwam katika jambo ambalo hakulitarajia-Tafsiri ni yangu)

  Hamadi Kibindoni (Msemo huu hutumika pale mtu anapokuwa amepata bahati ya kuokota kitu aua kupata kitu-Tafsiri ni yangu)

  Kasimama pale kama mzungu wa reli (Msemo huu unatumika pale mtu anaposimama mahali muda mrefu bila kusogea, na ndo huambiwa kuwa amesimama kama mzungu wa reli-Tafsiri ni yangu)
   
 2. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Hii inamaanisha kuwa Mungu anauwezo wa hali ya juu,haufanani na wa binadamu!!
   
 3. T

  Tall JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mzungu wa reli.......wakati reli ya kati inajengwa wasimamizi walikuwa wajerumani,waliweza kusimama muda mrefu bila kukaa wakiwaangalia watu wakichapa kazi, ili kuona kazi inafanyika
   
 4. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 996
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Kufua dafu ni kufanikisha jambo hata likafauru,aghalabu jambo gumu,haikufua dafu - ni kinyume chake yaani kushindwa kufaulisha

  .................................

  Amani yetu inatumiwa vibaya.
   
 5. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #5
  Apr 9, 2010
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Majibu/tafsiri unayo sasa maswali ya nini??????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. Katibukata

  Katibukata Senior Member

  #6
  Apr 12, 2010
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kandambili, mwanzisha thread kataka kujua asili/ chanzo cha misemo na si TAFSIRI ya misemo. hebu soma thread yake vizuri, utakubalina nami
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...