Kama hilo eneo unaloishi ni eneo lake la Kazi basi hutomlipa zaid ya kununua dawa.
Ila ni vizuri ukamotivate kidogo ili akuhudumie vizuri zaid
Sio kweli. Maafisa mifugo wameajiriwa kutoa ushauri na sio kutibu. Kwa hiyo bwana mifugo anapaswa amuandikie dawa mfugaji anunue na amwambie atafute mtaalam yeyote wa mifugo amtibie. Kama atatibu yeye sawa lakini kazi ya kutibu ni ya kibinafsi( private) haihusiani na ajira. Kwa hiyo akitibu anapaswa kulipwa hiyo sio fadhila. Tambua kuwa wanatibu wataalam mbalimbali hata wasio katika ajira ya serikali kwani wao hawapaswi kulipwa? Kwa hiyo akitibu yeye au akatafuta mtaalam mwingine wa kutibu katimiza wajibu wake.Kama hilo eneo unaloishi ni eneo lake la Kazi basi hutomlipa zaid ya kununua dawa.
Ila ni vizuri ukamotivate kidogo ili akuhudumie vizuri zaid
Kwa kuongezea matibabu sio dawa tu. Kuna vifaa kama syringe, thermometer, pamba, gloves, stethoscope, mikasi, visu vya kupasulia, dawa za kuosha vidonda, nk. Serikali haimpi chochote kati ya hivyo ananunua kwa mshahara wake. Halafu aje kutibu unasema utamlipa kwa fadhila tu? Hizo gharama za vifaa vya tiba atamrudishia nani?Sio kweli. Maafisa mifugo wameajiriwa kutoa ushauri na sio kutibu. Kwa hiyo bwana mifugo anapaswa amuandikie dawa mfugaji anunue na amwambie atafute mtaalam yeyote wa mifugo amtibie. Kama atatibu yeye sawa lakini kazi ya kutibu ni ya kibinafsi( private) haihusiani na ajira. Kwa hiyo akitibu anapaswa kulipwa hiyo sio fadhila. Tambua kuwa wanatibu wataalam mbalimbali hata wasio katika ajira ya serikali kwani wao hawapaswi kulipwa? Kwa hiyo akitibu yeye au akatafuta mtaalam mwingine wa kutibu katimiza wajibu wake.
Sawa na mtaalam wa kilimo. Sio kazi yake kubeba bomba la kunyunyizia dawa na kunyunyizia mazao ya mkulima. Yeye anapaswa kumuonyesha kwa vitendo jinsi ya kunyunyizia kisha amuachie aendelee mwenyewe. Hata wafugaji wapo waliofundishwa kuchoma sindano , kuhasi, nk. Hiyo ndio kazi rasmi ya bwana mifugo.
Mkuu Coral angalia kwenye post yangu pale juu, Gharama zote hizo unazozisema ninagharamia mimi. Kuanzia dawa hadi hizo syringes na gloves, wao ni kuja shambani na kutoa ushauri/utabibu kwa gharama ya shilingi laki 2 (200,000/-) kila wanapokuja. hiyo ndio hoja yangu na swali langu je kiwango hiki cha malipo ni cha kawaida kwa watu wote? au wamenifuma mimi tu?Kwa kuongezea matibabu sio dawa tu. Kuna vifaa kama syringe, thermometer, pamba, gloves, stethoscope, mikasi, visu vya kupasulia, dawa za kuosha vidonda, nk. Serikali haimpi chochote kati ya hivyo ananunua kwa mshahara wake. Halafu aje kutibu unasema utamlipa kwa fadhila tu? Hizo gharama za vifaa vya tiba atamrudishia nani?
Wanakuibia kama ni hivyo. Siwezi kuelewa mfugaji uwe na vifaa tiba vya nini? Mfano forceps, stethoscope, mfugaji atafanyia nini? Lazima akasome huo utaalam.Mkuu Coral angalia kwenye post yangu pale juu, Gharama zote hizo unazozisema ninagharamia mimi. Kuanzia dawa hadi hizo syringes na gloves, wao ni kuja shambani na kutoa ushauri/utabibu kwa gharama ya shilingi laki 2 (200,000/-) kila wanapokuja. hiyo ndio hoja yangu na swali langu je kiwango hiki cha malipo ni cha kawaida kwa watu wote? au wamenifuma mimi tu?
Kama unafuga kuku wa mayai laki mbili kutoa ni alali kabisa' mfano kuchanja chanjo ya CORYZA au SALMONELLA tunafanya kuku 1 sh. 150 had 200 sasa wewe una kuku 3000 unataka ufanyiwe bure' kwanza ujasema unamifugo gani unakuja kulialia huku.