Je, nina gundu au nimerogwa? Kila kazi nayoomba siitwi

Kila nafasi ya ajira inayotangazwa mm naomba, lakini hawaniiti hata kwenye interview. Je, nina Gundu au nimerogwa au Mungu hataki niende kwenye mishahara minono?

Kuna vitu wengi tunachanganya katika hizi issue za kuomba kazi. Kuna CV na RESUME

CV: hii inaeleza zaidi career yako ACADEMICALLY, yaani ni ya kuombea kusoma zaidi sio ya kazi

RESUME: hii inaeleza zaidi career yako PROFESSIONALLY, yaani hii ndio inahitajika aswa uombapo kazi

Kuhusu uandishi wa Resume unaweza kugoogle au kuingia youtube ukajifunze au ukawapa watu wakuandikie unawalipa ni kama laki 1 mpaka laki 2

Goodluck
 
Kama unavigezo vyote ni suala la muda wako bado mungu ndiye mtoa kazi binadamu atachelewesha tu
 
Amen
 
Kila nafasi ya ajira inayotangazwa mm naomba, lakini hawaniiti hata kwenye interview. Je, nina Gundu au nimerogwa au Mungu hataki niende kwenye mishahara minono?
Cheza saaana na CV yako, kwenye skills experience jaribu kucheza na mistari Yao. Ila usikate tamaa ukiwa unatafuta kazi Hali kama hiyo hujitokeza. Unaweza hata kuitwa interview Mkoani ukachoma nauli na usipate kazi, alafu siku unarudi nyumbani unakuta wife anakusubiri ndani Hamna kitu. Duh haya Maisha Noma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…