Je, nina gundu au nimerogwa? Kila kazi nayoomba siitwi

Trendz

Member
Jun 27, 2021
78
125
Kila nafasi ya ajira inayotangazwa mm naomba, lakini hawaniiti hata kwenye interview. Je, nina Gundu au nimerogwa au Mungu hataki niende kwenye mishahara minono?

Kuna vitu wengi tunachanganya katika hizi issue za kuomba kazi. Kuna CV na RESUME

CV: hii inaeleza zaidi career yako ACADEMICALLY, yaani ni ya kuombea kusoma zaidi sio ya kazi

RESUME: hii inaeleza zaidi career yako PROFESSIONALLY, yaani hii ndio inahitajika aswa uombapo kazi

Kuhusu uandishi wa Resume unaweza kugoogle au kuingia youtube ukajifunze au ukawapa watu wakuandikie unawalipa ni kama laki 1 mpaka laki 2

Goodluck
 

mandwa

JF-Expert Member
Aug 13, 2013
1,434
1,500
Kama unavigezo vyote ni suala la muda wako bado mungu ndiye mtoa kazi binadamu atachelewesha tu
 

lady Jay

JF-Expert Member
May 29, 2016
469
1,000
Usife moyo mkuu jaribu utaitwa Usiache kujaribu na kumtanguliza Mungu hata mm nilikuwa kwenye situation Kama hiyo nashukuru mungu nimeitwa kwenye enterview minzani. Kitendo cha kuitwa tu kwenye enterview nimeona nihatua kubwa Sana maana niliapply nafasi nyingi sana sikuwahi itwa japo interview
Amen
 

FURY BORN

JF-Expert Member
Jul 11, 2020
482
1,000
Kila nafasi ya ajira inayotangazwa mm naomba, lakini hawaniiti hata kwenye interview. Je, nina Gundu au nimerogwa au Mungu hataki niende kwenye mishahara minono?
Cheza saaana na CV yako, kwenye skills experience jaribu kucheza na mistari Yao. Ila usikate tamaa ukiwa unatafuta kazi Hali kama hiyo hujitokeza. Unaweza hata kuitwa interview Mkoani ukachoma nauli na usipate kazi, alafu siku unarudi nyumbani unakuta wife anakusubiri ndani Hamna kitu. Duh haya Maisha Noma.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom