Je, Nimwinde Wapi Mpenzi Wangu? Mwisho wa Kutembeza CV Barabarani!

Davidmmarista

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2024
Posts
2,266
Reaction score
4,427
Wadau wa Jamiiforums, Habari Zenu?

Natumai mpo fresh na maisha hayajakubana sana kama viatu vya ndugu yangu Juma vilivyojaa viraka. Leo nimekuja na kero kubwa inayowasumbua wengi, hasa mabachelor wa mtaani kutafuta mpenzi! Yaani, kila siku unakutana na dada mmoja barabarani, unajifanya kama umeuliza njia kumbe unalenga namba ya simu. Hapo ukipigwa na "Sina bando” au "Nina mtu" moyo unakauka kama jua la Dodoma.
Lakini sasa, tutoke huko! Leo napasua jipu kwa kutafuta wapi unaweza kumpata mpenzi wa maana bila kutumia mistari ya darasani au kuitwa "mjomba" kwa kutongoza hovyo hovyo.

1. Kazini Usichezee Nyavu Ulizozitandaza
Ofisini kunaweza kuwa mahali pazuri pa kupata mpenzi, lakini sio kila dada anayekusalimia kwa tabasamu ni 'single'. Mwangalie kwa makini, usije ukamtongoza HR halafu usipate mpenzi wala kazi! Mfano, jamaa yangu alimtongoza secretary wa boss, akajikuta anaandika resignation letter badala ya love letter.

2. Kanisani/Misikitini Mahali pa Baraka au Jaribu?
Hapa kuna wake na waume wa ndoa wa maana. Lakini usije ukaenda kanisani au msikitini na lengo la kutongoza tu, utajikuta unahubiriwa badala ya kupata mpenzi. Kuna jamaa alienda kwa lengo hilo, akajikuta anakuwa shemasi! Ukiona dada yupo 'serious' na imani yake na unaona mnaendana, jitahidi kumkaribia kwa hekima.

3. Sherehe na Harusi Hapa ni Kusuka au Kunyoa
Kama unaenda harusi ya rafiki yako, usiende na suti ya kuvutia tu jitahidi pia kuwa na mistari ya maana. Lakini kuwa makini, usije ukatokea kwa bibi harusi ukifikiri ni bridesmaid! Harusi ni eneo zuri la kukutana na mtu mpya, haswa kama wewe ni 'single'.

4. Wanachuo Wachangamkie Wanafunzi Wenzao

Hapa kuna vijana wengi wenye mawazo mapya na malengo makubwa. Lakini usikimbilie kuoa mtu wa semester ya kwanza, bado ana 'assignments' nyingi za maisha. Utakuta unajitahidi kumpa mapenzi, yeye anafikiria coursework!

5. Gym Mpenzi Mnene au Mchongoko?
Gym ni sehemu nzuri kwa sababu watu huwa na malengo ya kujiboresha. Lakini kabla hujamfuata dada unayemzimia, hakikisha unajua kama ni single au anakuja na mchumba wake wa "six-pack" Jamaa mmoja alijaribu kutongoza mwanamke gym, akajikuta ananyanyuliwa juu kama dumbbell!(Ni chai lakini😂)

6. Matamasha na Tamasha za Kijamii Furaha na Mahaba
Kwenye matamasha ya muziki, filamu au hata makongamano, unakutana na watu wapya. Usianze kuzungumza tu bila mpangilio, unakutana na mtu unamwambia "Habari yako, natokea Kibaha" halafu kimya! Jenga mazungumzo ya maana, siyo kuharibu mood ya tamasha.

7. Masoko na Maduka Makubwa Mahali pa Bahati na Simu za Haraka
Watu wengi hawajui kuwa unaweza kupata mpenzi kwenye soko la kawaida. Dada mmoja anaweza kuwa ananunua matunda, ukamwambia, "Hivi machungwa haya ni matamu kama tabasamu lako?" Lakini hakikisha huna dharau, usianze na "Unapika chakula cha mumeo?" hapo utashangaa unajibiwa "Sina muda wa upuuzi!"

8. Social Media DM Usizidanganye!

Instagram, Facebook, na Twitter zinaweza kuwa sehemu nzuri za kupata mpenzi, lakini ukitaka mafanikio, usiingie na mistari ya copy-paste. "Hey, beautiful" haifanyi kazi siku hizi! Kuwa mbunifu, anzia na mjadala wa maana. Mfano, badala ya "niaje mrembo," unaweza kumwambia, *"Mimi napenda kujadili series, je, kuna series unaipenda sana?"$

9. Usafiri wa Umma Mapenzi Kati ya Daladala na BRT
Hapa panahitaji ujasiri wa hali ya juu. Kama umekaa karibu na dada anayependeza, usianze kwa kuuliza "Unaenda wapi?" atajua unajifanya trafiki. Badala yake, tafuta njia nzuri ya mazungumzo, labda kama kuna hali ya kuchekesha kwenye gari. Lakini ukiona hana mood, usijilazimishe!

10. Hospitali.
Wakati mwingine unaweza kupata mpenzi hospitalini, lakini si kwa wagonjwa! Kama unamhudumia mtu na unakutana na daktari au nesi anayevutia, unaweza kujenga urafiki. Lakini usifanye kosa la kutongoza mgonjwa anayepata dripu, anaweza kukujibu vibaya kwa uchungu wa sindano!

11. Mahali pa Kazi za Kujitolea (Mapenzi ya Kujenga Jamii)
Ukijihusisha na kazi za kijamii kama kusaidia yatima au mazingira, unakutana na watu wenye roho nzuri. Mahali kama haya, watu huwa na malengo makubwa, hivyo ni rahisi kupata mtu anayeendana na maisha yako.

12. Familia na Marafiki (Referrals za Mahaba)
Marafiki zako au familia wanaweza kuwa na watu wazuri wa kukutambulisha. Lakini kuwa makini, usije ukakubali kila mtu anayeletwa! "Nina rafiki yangu mzuri" inaweza kuwa njia ya kushinikizwa uingie kwenye mahusiano usiyotaka.

13. Mikusanyiko ya Kitaalamu: Future Wife Material?
Kama unahudhuria semina za kitaalam au vikao vya maendeleo, unakutana na watu wenye malengo kama yako. Ukiona mtu unayempenda, ongea naye kwa heshima, usianze na "Mimi ni CEO wa maisha yangu," atajua unajisifia. Badala yake, tafuta mazungumzo yenye maana.

Pata Mpenzi Kwa Ustaarabu, Sio Kutembeza CV Barabarani!
Mapenzi hayapaswi kuwa kama kutafuta kazi ambapo unapeleka CV kila kona. Weka hadhi yako, kuwa na subira, na tafuta mtu anayekufaa bila kujidhalilisha. Sio kila dada unayekutana naye anaweza kuwa mpenzi wako, na si kila mwanaume anayejitahidi anakufaa.
Kwa hiyo, ndugu zangu, kama hujampata bado, tafuta sehemu sahihi. Wacha kuomba namba hovyo barabarani, kuna njia bora za kupendwa na kuheshimika.
Naomba niwasilishe!
 
Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe - twanga pepeta song

lakini mimi nasema

Mtaji wa mpiga punyeto ni mikono yake mwenyewe🥶
 
Back
Top Bottom