Crimea Bridge
Member
- Oct 8, 2022
- 51
- 152
Nina mke wa ndoa ambaye nina watoto naye watatu, umri wangu sasa ni miaka 32 na umri wa mke wangu ni miaka 28. Zamani nilikua na uwezo mkubwa na alinipenda sana, ila tokea pesa zimepungua ndiyo nimeona mapungufu yake. Kuna kipindi alitoroka akaniachia watoto, nikapambana kumrudisha maisha yakaendelea ila sasa hivi naona tena dharau na maneno yameanza tena.
Anawadharau wazazi wangu, yeye anasikiliza sana maneno kutoka kwa mama yake, mimi hata niseme nini sisikilizwi, ila mama yake chochote anachomwambia ndiyo anakifuata.
je nini nifanyeje, nimuache aendelee na maisha yake, au nifanyeje ili akae sawa? Na je, vipi kuhusu watoto wetu watatu, mkubwa miaka 5 (Ke), wa kati ana miaka 3 (Me) na wa mwisho ana mwaka mmoja (Me)?