Je, nimruhusu aje kunitembelea mkoa nilipo?

Je, nimruhusu aje kunitembelea mkoa nilipo?

blogspot

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2017
Posts
1,269
Reaction score
1,147
Habari wakuu katika Jukwaa Pendwa!

Niwarudishe nyuma kidogo. Mwaka 2011 nilibahatika kua na Mahusiano na binti Aliekua anaitwa Asha (sio jina halisi) tuliweza kudumu katika mahusiano yale kwa miaka miwili lakini nilipata safari familia yetu tukahama kwa sababu za kazi upande wa wazazi wangu.

Huyu binti alikua ananipenda sana kila Aliyekua karibu yangu alikua anajua ni jinsi gani napendwa na huyu Binti ilifika kipindi mpaka alikua hawezi kusoma asiponiona mimi. Alitumia Muda wake mwingi kuwa na mimi karibu,Zawadi za hapa na pale zilikua nyingi sana.

Wakuu kipindi hicho mimi bado nilikua young sana na tulikua shule na hata maswala ya Mahusiano ya kimapenzi nilikua sijaanza kabisa"yaani sumu ya penzi nilikua sijailamba" hivyo huyu binti nilikua namuogopa sana although alikua ananipa nafasi nyingi sana ila nilikua nazikwepa sana.

Washkaji zangu walikua wananicheka sana. Muda mwingine hadi walitani wao wawe mimi ila binti alikua anawachomolea nje na baadae ananiambia kila kitu.

Baada ya kuwa mbali kwa muda kidogo (kupotezana) .mwaka 2017 huyu binti Asha alinipata kupitia Mtandao wa facebook na tukabadilishana mawazo na mawasiliano pia. Niliitaji kufahamu kiundani kuusu anapatikana wapi na anajishughulisha na nini. Alinipa ushirikiano nikaweza kufahamu yote hayo kuwa alikua Anafanyakazi kampuni moja ya Madini kama Kama Mwasibu huko Mwanza.

Basi tukawa tunajuliana hali mara kwa mara. Siku moja aliniomba muda niweze kuongea nae jambo(Via phone call)Nikampa nafasi tuliongea Mengi sana ila Nilishangaa sana alianza kuniomba Msamaha kuwa alipata ujauzito na Aliempa Ujauzito alimkataa. Hii ishu iliniumiza sana nikamfariji sana.

Mawasiliano yetu kupitia simu yaliendelea mpaka hivi majuzi ambapo Binti huyu amekua akicheki mara kwa mara huku akinitumia Miamala ya kifedha. Nikiuliza ya nini anasema anafurahi kuona nakua sina mawazo haswa napokua na jambo linalohitaji utatuzi wakifedha. Amekua akiniita kila jina La kimahaba ila anapenda sana kuniita "My Boss.." . Pia amekua akimpa mwanae simu niongee nae na akimwambia "msalimie baba" Mtoto amekua akijua kua mimi ndio baba yake na ana miaka mitatu pia amekua akiniuliza sana lini narudi nyumbani. Mimi huwa napenda sana Watoto hivyo kuhusu hili jambo linakua linaniumiza sana kama binadamu bila kujali uhusiano wa mm na mtoto.

Binti huyu anajua fika niko ktk mahusiano lakini amekua akiamini kua mimi ndio furaha yake na ndio Mfariji wake mkuu ktk kila jambo. Yaani wakuu haipiti masaa matano najuliwa khali. Binti amekua akionesha dhahiri kua bado ana ndoto na mimi,Leo amenipigia simu akiniomba ruhusa nimruhusu aje Mkoani Mbeya Tuonane.

Wakuu naombeni ushauri Nimkataze asimwambie mtoto asiniite Baba? Pia Nimruhusu aweze kufika Mbeya au nimkatalie. Mpaka sasa bado sjampa majibu sahihi!

●Wakuu Mwanamke akikupenda kapenda. Yaani hajali lolote.

●Mwanaume ukimfanya mwanamke mliechana ktk mahusiano kua rafiki Atakuheshimu sana.

●Mwanaume ukiwa na Busara Mwanamke atakuheshimu pia.
 
Mwanaume kula hela ya mwanamke ni uzwazwa,undaza na umama.
 
Na usimkule mdada wa watu,mwambie yeye ni mzuri sana,ana akili,amesoma kabahatika ana kazi nzuri,na kikubwa ana mtoto watu wengi wanahangaika hawapati watoto,haijalishi huyo fala kumkataa
 
Mkuu, huyu rafiki yako Asha atakua sumu ya mahusiano yako ya sasa hivi.

Mweke wazi kuwa hutaki akuite majina ya kimahaba kwasababu una mtu tayari.Kuhusu mtoto, kwa umri wake mkiendelea hivyo ataamini wewe ndiye baba halafu baadae mtamuumiza.Ni bora akuite uncle kama vipi.
 
Muambie unampenda sana na itakuuma kuona unamtumia au ukimuumiza mbeleni,miaka mliyoachana ni mingi na una mahusiano rasmi,kwa sasa tuwe marafiki na kama ushauri nitakupa muambie atapata mwanaume bora kabisa kwake na akawa baba bora wa familia yake,asipokuelewa kata mawasiliano,block kila mahali ataumia mda mfupi ila atakushukuru sana mbeleni.
 
Muambie unampenda sana na itakuuma kuona unamtumia au ukimuumiza mbeleni,miaka mliyoachana ni mingi na una mahusiano rasmi,kwa sasa tuwe marafiki na kama ushauri nitakupa muambie atapata mwanaume bora kabisa kwake na akawa baba bora wa familia yake,asipokuelewa kata mawasiliano,block kila mahali ataumia mda mfupi ila atakushukuru sana mbeleni.
Ushauri mzuri, ila akiufuata si atakosa Hiyo miamala Sasa?

Anataka kufaidi miamala huyu, ndio maana kabaki njia panda.
 
Back
Top Bottom