Je, nimekosea kuwapotezea baadhi ya ndugu zangu? Naomba ushauri tafadhali

Kama una kipato cha kutosha cha kuweza kuwasaidia we Sadia tu. Hii Dunia tunapita we samehe naamini Mungu amekupitisha ktk changamoto zote hizo ndo maana Leo umekuwa ivo.
Hakuna!! Asamehe hiyo vipi? Kwenye kukata hiyo migogo ili apate ada angeshuka mshipa wangemsaidia hata matibabu? Vipi km angepata tb au ulemavu wowote? Angeishia kuwa chokoraa au kibaka au teja kutokana na kutengwa na kudharauliwa ingekuwaje?

Mbona mnapenda kujazana unyonge bila sababu za msingi? Kwa kukushauri tu, mleta uzi, wanunulie smart 4n ndugu zako wote bila kumsahau baba ako, kisha anzisha group la whatsp, waunge wote, thereafter, anza kula bata huku unapiga picha na kuzitupia kwa group kila siku!

Hata ukiweza nenda viwanja vikubwa km mahoteli makubwa, piga picha ondoka, kawapostie, wakijileta tu unawapa kubwa, unawachana live bila chenga! Bila kusahau kutupia status za vijembe kwa baba ako, anza na hizi chache:

Uliookota nae kuni ndie utaota nae moto.

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Mama yangu ndio kila kitu kwenye maisha yangu.

Mtu mwenye kitu, asie na kitu kinyama cha mwitu.

Kikulacho ki nguoni mwako.

Mchawi ndugu, paka katumwa tu.
 
Hakuna!! Asamehe hiyo vipi? Kwenye kukata hiyo migogo ili apate ada angeshuka mshipa wangemsaidia hata matibabu? Vipi km angepata tb au ulemavu wowote? Angeishia kuwa chokoraa au kibaka au teja kutokana na kutengwa na kudharauliwa ingekuwaje?...
Mzee nimepigana hasa. Buguruni niliishi kwenye chumba cha 8,000/= na hapo nikaishia kutimuliwa baada ya kodi kunishinda. Leo nakula bata ulaya wote waliyonidharau wanajileta. Kwa kweli nimekataa
 
Nakushauri Dala.... tumia lugha nzuri yenye diplomasia kwa ndg zako... kama hutaki kusaidia. tafuta sbb ya kueleweka ili waridhie.. usikatae ili mradi tu.. kuwa muungwana na mpole.

Ndivyo nilivyofanya. Nimemwambia Mzee nina ukata mbaya kwa sasa akanielewa. Nimempa na ushahidi maana nina miradi yangu nimewekeza hela wiki mbili zilizopita akanielewa.

Dada hathubutu hata kunitafuta moja kwa moja
 
Hakuna!! Asamehe hiyo vipi? Kwenye kukata hiyo migogo ili apate ada angeshuka mshipa wangemsaidia hata matibabu? Vipi km angepata tb au ulemavu wowote? Angeishia kuwa chokoraa au kibaka au teja kutokana na kutengwa na kudharauliwa ingekuwaje? ...
Mkuu vijembe vyako si vya nchi hii!!! Kwa wabongo hawatochelewa kukupiga kipapai.
 
Nawasalimu nyote!

Moja kwa moja kwenye mada, historia yangu ina changamoto nyingi. Naamini kila mmoja ana changamoto yake. Kwa kifupi ni kwamba nimezaliwa kwenye familia ya wake wawili...
Watu wabaya yao achana nao walitamani ufe tu ila Mungu sio Asuman,
 
Nawasalimu nyote!

Moja kwa moja kwenye mada, historia yangu ina changamoto nyingi. Naamini kila mmoja ana changamoto yake. Kwa kifupi ni kwamba nimezaliwa kwenye familia ya wake wawili...
Fuata moyo wako unavokuambia, ila zaidi uwe mtu wa kusali sana, maana wanaweza kukuzingua na mambo yao ya kiswahili sababu tu wewe umefanikiwa zaidi.
 
Fuata moyo wako unavokuambia, ila zaidi uwe mtu wa kusali sana, maana wanaweza kukuzingua na mambo yao ya kiswahili sababu tu wewe umefanikiwa zaidi.

Najitahidi kujiweka mbali kidogo nao pia
 
Jitahidi kuwa nao mbali wasifahamu mambo yoyote kuhusu wewe na familia yako!

Waombee kwa Mungu fu labda yeye ndio ataweza kuwabadilisha tabia,

nikiri kwamba huruma yako na upole wako unaouleta kwao si chochote,

maana kuna uwezekano mkubwa wakawa wanakumanipulate tu ili wakutumie watakavyo, na watafanya kila njia ujione muovu au unakosea sana unaposhindwa kuwasaidia!

Pambana na familia yako pamoja na watoto wako hakikisha unawatunza vyema pamoja na akiba yao siku za usoni, hakikisha una uwekezaji wakutosha kibiashara... mwisho kabisa ndio usaidie hao jamaa,

Huyo dada yako kaolewa na ana mme , mme wake pia inabidi a play party kubwa.. unless kama wewe ndio ukiwa unatoa misaada kila kukicha uyo shemeji yako anaweza kudharauliwa na kuqchwa na dada yako , kwa kushindwa kuprovide!
 
Jitahidi kuwa nao mbali wasifahamu mambo yoyote kuhusu wewe na familia yako!

Waombee kwa Mungu fu labda yeye ndio ataweza kuwabadilisha tabia....

Uko sahihi mkuu. Nimekuelewa
 
Back
Top Bottom