Je, nikimuoa naweza nikampenda?

Je, nikimuoa naweza nikampenda?

Habari za majukumu ndugu zangu, nipo hapa kuomba ushauri wa kimahusiano natumaini ntapata majibu ya hiki kinachonitatiza.

IPO HIVI

Miaka miwili nyuma niliwahi kuzoeana na mdada mmoja, kiumri namzidi miaka miwili, nilifahamiana nae kipindi nimeenda kijijin kuwasalimia wazazi na kupata baraka zao.

Alikuwa ni jirani yetu (nyumba ya 3 kutoka kwetu) na pia mara nyingi tulikuwa tunaonana baada ya salamu kila mtu nachukua hamsin zake.

Sasa katika kuanza kuzoeana nilimuomba namba, hakusita alinipatia maongezi yahakamia kwenye simu, cha ajabu huyu binti alinizoea kupitiliza ikawa yeye ndo ananitafuta mara kwa mara hatimaye akaamua kunifungukia juu ya hisia zake kwangu na kuniambia ametokea kunipenda,

Niliona nimkubalie tu lakini hakuwa moyoni mwangu kabsa,sikuwahi kumwelewa nilimchukulia kama mdogo wangu (niliona nifanye hivyo asinichukie wala kujisikia vibaya)

Ndani ya hii miaka miwili huyu binti sijawahi kumhisi kwa chochote kibaya,pia hata nikiwa na shida ni mwepesi sana wa kunisaidia (hasa kifedha).

Binti huyu ana kila sifa ya kuitwa mke (namaanisha vigezo vyote ninavyovihitaj kutoka kwa mwanamke anavyo vyote ,changamoto tu ni kwamba sina hisia naye hata kidogo.

Wiki 2 zilizopita aliomba kuja kunitembelea,na alikuja kwa gharama zake na wala sikushtuka nilipomtuka bikra (maana amejituliza mno, mno, mno )

Kuhusu kipato chake.
Ameajiriwa na shangazi yake stationary, anamlipa 150k kwa mwez

Kuna muda namjaribu kwa kumwambia mshahara wake awe anautuma kwangu,hana noma anatuma tu badae namuonea huruma namrudishia.

Ila na mm sometimes huwa namtumia pesa za matumiz (kwa aibu baada ya kula vyake vingi)

kwa upande wa mawasiliano sijawahi mtafuta ,siku zote anaanza yy wala hajawah kuhoji hiki kitu,ndani ya mwezi naweza mtafuta mara 1 yy mara hata 1000 (anatekeleza kwa moyo wake wote)

Ndugu zangu moyo wangu huna chembe yyte ya hisia kwake,naweza nikaongea lolote,chochote ni nikaona poa tu ,ila yy ni mnyenyekevu

JE nimuoe hivyo hivyo ntampenda hapo mbeleni au nimpotezee tu nisije nikamtesa mtoto wa watu

Ushauri tafadhali.
Hapana wewe ni mwanaume kama hujampenda kipindi chote hicho ni ngumu kumpenda mkiishi pamoja, maana hapo mapungufu ya kila mtu ndio huanza kuonekana,ninachokiona hapo unamuhurumia ila huna hisia hata chembe aisee utakuja uchukie maisha ya ndoa... ni mke mwema sawa ila moyo wako haupo kwake utakuja ujute baadaye pale ambapo utakutana na mwanamke atakayeuteka moyo wako ndio utakapoona dunia chungu.
 
Kaka achana na dada wa watu kabla hamjafika mbali, usimpotezee muda wake na kiuungwana kama hujamtoa utando usitoe aje tolewa na mtu ambaye atakuwa sahihi unless yeye atake umtoe kwa mahaba yake lakn ni baada ya kumwambia huna interest naye.

Nilishawahi kuwa na scenario kama yako miaka kadhaa nyuma, huyu mdada alinizidi miaka 2 nyuma, nilikuwa namsaidia hizi application za Ualimu hadi akanizoea akafunguka.

Lakini sikuwa na hisia nae, nlijikuta ni mtu ambaye asiponicheki sawa ,akinicheki sawa, kosa dogo nammaindi kinoma.

Japo watakuja watu waseme bora uoe mdada anayekupenda LKN kuishi na mtu usie na hisia naye ni ngumu.
Sure
 
Back
Top Bottom