My dear kwa unavyomjua huyo mwanaume wako anaweza kujisimamia? Maana kushauri mwanaume ambae hana msimamo ni wa kupelekeshwa na mama

utajichosha bure. Anaweza kubali ushauri wako sababu hataki kuachana na wewe but Utekelezaji zero, na ukiolewa nae ndo utakinywea.
Nakwambia from my experience, nilipata mkwe mwenye tabia kama za huyo wako.... siku ya utambulisho ananisifia "Masha Allah mtoto mzuri, umeumbika shape kweli kweli hapa mwanangu kapata". Baada ya hapo akawa mtu wa kuagiza ninunulie hiki, ninunulie kile kwa ufupi simu za pesa pesa zikazidi haswaa (imagine mama wa mchumba anakwambia umnunulie kitu cost yake laki7

) . Kumbe ashajua nafanya kazi gani so familia nzima wanaamini mtoto wao kanipendea hela


Nikamkaushia tena vingine nikawa namjibu sina hela, baadae mwanae alivotaka tufunge ndoa akakataa eti asubiri afanye kwanza maendeleo nyumbani. Kijana akagoma keshaamua kuoa, tukafunga ndoa mkoa tuliopo (sio kwao) though mama mtu alikuja harusini kinafiki tena kwa kuchelewa...... from there hakuna mahusiano mazuri kati yetu na familia yake.
Na huu ni mwaka wa Sita wa ndoa ila hatuna mtoto.
So my dear tumia akili yako effectively, kama utaweza mikiki na mengine yasojulikana endelea na huyo mwanaume.