Habari wadau, ama kweli yakikufika huna namna utazungumza tu. Mwenzenu yamenifika shingoni na sijui kama nikichukua maamuzi ya kumuacha nitakua nakosea au lah.
Nikiri katika mahusiano yote niliyopitia sijawahi kuwa na mwanaume anayenifanya nijisikie furaha kama huyu kaka.Uhusiano wetu una mwaka sasa. Ni mkaka anayepambana sana, anajali, anahudumia pale anapoweza na kule 6*6 ndo usiseme. Hamna kitu ananificha. In short he is a man in every woman's dream mpaka nikawa naogopa kumpoteza bwana.
Mbembe ikaja baada ya kunitambulisha kwa mama yake mzazi (Eh Mungu). Mama alinipokea vizuri tu lakini siku ya kwanza tu akaniambia ukija niletee bia, mtoto wa kike nikapeleka. Baada ya hapo kila nikiona simu ya yule mama yeye ni kutaka hela tu kwangu. Nikajiuliza ni kisa kaniona na gari au ni nini?
On top of that mama yake hatak apange, kashikilia akae nyumbani eti asiharibu hela kwa kulipa kodi. Mshahara wake wote unatumika kwenye matumizi ya nyumbani, kama anabakiza ni kiasi kdg sana. Sasa kutokana na ukaribu huo kati yao naogopa hata kumshauri asije ona nawaingilia maisha yao.
Napata hofu kuwa ntakua adui kwa yule mama, maana akibadilika kimatumizi ataona mimi ndo kisababishi. Jamaa anapanga mipango ya ndoa lakini naogopa sana kuingia kwenye ile familia. Maana hata akiongea nae kwenye simu akiomba hela akimwambia hana anamwambia ahakikishe anaipata anampa na kijana anafanya hivyo.
Je, nikimuacha huyu kijana mapema nitakuwa nakosea?