Je, ni vibaya kunyonyesha ukiwa mjamzito?

Nameless-

Member
May 21, 2009
47
1
Mwenye jibu la kisayansi anisaidie.

Kama mama ananyonyesha mtoto mfano mwenye umri miezi 9 na kuendelea, akipata ujauzito, kuna athari zozote kuendelea kunyonyesha mwanawe?
 
Haina uhusiano wowote mie kuna rafiki yangu alipata ujauzito huku ana mtoto wa miezi mitano akaenda kwa daktari wake kuomba ushauri, dr akamwambia hakuna tatizo basi kanyonyesha mtoto mpaka siku anaenda kujifungua, na hakukuwa na madhara yoyote watoto wote wana afya njema mpaka leo hii mdogo tayari ana miaka 2 na nusu.
 
Mwenye jibu la kisayansi anisaidie. Kama mama ananyonyesha mtoto mfano mwenye umri miezi 9 na kuendelea, akipata ujauzito, kuna athari zozote kuendelea kunyonyesha mwanawe?


Tumia nyota ya Kijani Nameless.

Shauri yako,

Utachekwa na mama mkwe!
 
Swali lako lina utata kidogo nimewahi kusikia kwamba sijui ukifanya hivyo unaweza bemenda mtoto..ila hilo sina uhakika nalo...ni vyema ukapata ushauri wa daktari.

Ila kuna kajiblog nimekaona leo kanaitwa; mashosti.blogspot.com

Ni kazuri kwa kina mama wajawazito unaweza kujifunza lolote
 
Wataalam,

MTOTO WANGU ANA UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI MITATU, MKE WANGU ANA UJAUZITO WA MWEZI MMOJA.

Je, kuna madhara yeyote ambayo mtoto anaweza kuyapata akinyonya katika kipindi hiki cha mabadiliko ya mwili sababu ya ujauzito?

Kama inaruhusiwa kuendelea kunyonyesha ni kwa mda gani?

Nashukuru sana.
 
Na mimi hili swali linanihusu, tafadhali tafadhali wataalam......
 
Kuna siku nilikuwa namsikiliza mtaalamu akasema wakati wa ujauzito mtoto anaweza kuendelea kunyonya hadi miezi sita au saba.

Ila kipindi ambacho mama amebeba ujauzitomwingine kunakuwa na mabadiliko ya homoni ambayo husababisha maziwa kuwa na virutubisho vingi na hivyo kusababisha mtoto anayenyonya kuweza kupatwa na tatizo la kuharisha, lakini ni kwa kipindi cha mpito tu yaani kipindi cha kushika mimba na baadae mtoto anaendelea kunyonya bila tatizo (kuna kasumba ya kusema mtoto amenyonya maziwa machafu ndo hicho kipindi cha mpito).
 
Nakubaliana na wewe MKEMPIA. Mtoto wake BabaJunior anakaribia mwaka mmoja na nusu sasa. Bora amwachishe kunyonya tu.
 
Habari wana JamiiForums,

Mimi nimeoa na nimebahatika kupata mtoto mmoja ambaye mpaka sasa ana mwaka mmoja.

Sasa tatizo ni kwamba mke wangu ana mimba nyingine na bado mtoto wetu ananyonya.

Kiukweli sijui nini cha kufanya na ukizingatia mke wangu alijifungua kwa njia ya upasuaji mimba ya kwanza.

Naamini mtanishauri vizuri nini cha kufanya na wapi nianzie.
 
Mwachisheni mtoto kunyonya. Ila na wewe uwe makini bana watoto wapishane kidogo, sasa watakuwa kama mapacha bana!
 
Wadau,

Naombeni mnijuze kama kuna madhara yoyote kwa mtoto endapo mama atamnyonyesha huku akiwa na ujauzito mwingine.

Na je,ni baada ya kipindi gani mama anatakiwa kusitisha kunyonyesha akishajigundua kuwa ana ujauzito?
 
Back
Top Bottom