Je ni Sawa mtu anapofariki kusema kapoteza maisha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni Sawa mtu anapofariki kusema kapoteza maisha?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Nyamanoro, Feb 19, 2011.

 1. N

  Nyamanoro JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
  Nimekuwa nikisikia watu wakitumia neno "kupoteza maisha" kumaanisha mtu amefariki dunia,mimi nafikiri si sahihi kwani inaonekana imetokana na maneno ya kiingereza " lost life". Naomba nisaidiwe.
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Sarufi za lugha hutofautiana, kupoteza maisha huwa na maana ya kutokuwa na ile karama ya uhai, ambayo tunaipata kwa Mungu. Ni neno lenye mahadhi ya kishairi zaidi...
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Sasa mbona hau'suggest neno unalohisi ni sahihi kulitumia...?
  Mtu anapokuwa katika kufani, anakuwa na tabia ya kustruggle fulani hata kwa kumtazama physically...hivyo kule ni kupigania maisha..hivyo akifa ni kupoteza!..by my opinion its just ok!
  Una habari wazungu wanasemaje mtu akinusurika kufa...?, wanasema "PakaJimmy has cheated death"!...Sasa kwa lugha hiyo ya wenzetu sijui ungesemaje!
   
 4. N

  Nyamanoro JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60

  Ushauri wangu tuendelee kutumia neno kufariki dunia kwa kuwa ndio neno sahihi,tuachane na kasumba ya kutafakari kwa kiingereza alafu unasema kwa kiswahili.
   
 5. N

  Nyamanoro JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
  Nashukuru kwa mchango. Mimi nafikiri kwenye lugha rasmi si vema kutumia lugha za kimashairi au nahau mfano "muda unatutupa mkono" hizi zinaweza kutumika katika lugha ya mazungumzo ya kawaida ambayo wakati fulani ishara zinaweza kutumika kufikisha ujumbe badala ya neno.
   
 6. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Jee amefariki haijitoshelezi - bila kuongeza 'dunia' mbele yake?
   
 7. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Subiri ufe ndo utajua :angry::angry::angry:
   
 8. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  neno la msingi ni "kufa" na ni neno muafaka la mzizi kwa tendo husika kwa nayakati na nafsi mbalimbali. maneno mengine yote yakiwemo kupoteza maisha, kumwaga damu, kukata roho, kusalimu roho, kufariki, kufariki dunia nk. ni ya kishairi tu.

  Nyamanoro umependekeza tutumie neno kufariki dunia, alakini maana halisi ya "kufariki" ni "kutengana" yaani "separate" kwa kiingereza na limetokana na neno la mzizi la "faraka" na maneno mengine ya jamii hii ni pamoja na farakana, mifarakano farakanisha nk. soma kitabu cha Isaya 59:2 utaona neno "kufarikisha" limetumika.

  pmwasyoke, unauliza ikiwa kusema kufariki pekee bila kuongeza "dunia" mbele yake kunakamilisha maana iliyokusudiwa. jibu ni kuwa haikamilishi maana ya kufa. kama nilivyomjibu nyamanoro hapo, kufariki ni kutengana au "to be separated" kwa kiingereza. mtu anaweza kujifarikisha au kufarikishwa na familia, marafiki, dunia, Mungu nk. kwa hiyo kama una maana kuwa huyo fulani katengana na dunia au maisha ni muhimu kuongezea hayo maneno mbele yake ili tujue katengana na nini, vinginevyo utatuacha bila kujua katengana au kafarakana na nini. mfano mtu akitumbukia dhambini huwa amefarakana na Mungu au dhambi zake zimemfarikisha na Mungu wake kwa maana kuwa zimemtenga (zimem-separate) na Mungu wake na si kuwa amekufa. kwa hiyo ni muhimu kusema amefariki dunia au amfariki maisha.

  stay blessed.

  Glory to God
   
 9. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Maelezo haya YAMEENDA SHULE.
  Thanks, Miss J and be blessed!
   
 10. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  thanks
   
 11. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kwa kweli kwa maelezo haya, unathibitisha kuwa u-kiumbe mwenye vipaji vingi sana. hongera sana kwa kutawala nyanja mbalimbali za maisha...............

  natamani kuwa kando yako kila wakati nipate kujfunza toka kwako, ..................nitaku-PM juu ya hili............... serious!................ ubarikiwe sana shangazi...............
   
 12. nkyandwale

  nkyandwale Member

  #12
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Duh ! Baadhi ya matumizi ya maneno yanayochomolewa kutoka lugha ya kiingereza huharibu utamu wa lugha ya kiswahili, hayo ni matokewo ya kuchanganya ndimi na tunajidai ati tunakuza lugha! Kwa mfano wengine hutumiya neno kupelekeya badala ya kusema husababisha. Mfano mwendo kasi ulipelekeya ajali. Miye naamini kuwa kitu kikipoteya upo uwezekano wakukitafuta na upo uwezekano wa kukipata au la! Lakini si uhai. Mtu akifa ndiyo kwaheri Mwalimu. Je, maisha yakipoteya upo uwezekano wa kuyatafuta? :angry:
   
 13. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Mimi nilidhani 'kufa' ni kifupisho tu cha neno kufariki (kufariki dunia):embarassed2:!
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kwanza sikubaliani na mantiki yako....kwamba neno linapoteza usahihi wake kwa sababu limetokana na lugha nyingine! Kama ni hivyo maneno mengi ya kiswahili hayawezi kuwa sahihi (mf: shule (kijerumani:schule), skuli (kiingereza:school), shule ya upili (kiingereza/kijerumani: secondary/schule), shule ya sekondari (kijerumani/kiingereza: schule/secondary) nk nk)!

  Pili, lugha ni kwa ajili ya mawasiliano baina ya watu na watu wanabadilika (vivyo hivyo na lugha). Hivyo 'kupoteza maisha' hata kama imetokana na tafsiri sisisi ya maneno ya kiingereza 'lost life', bado linaweza kuwa sahihi kama limepata mashiko (kwa nasibu limekubaliwa na wazumngumzaji wa kiswahili kutumika katika mawasiliano yao!).

  Tatu, sio mara zote unaweza kubadili neno kufa, kufariki nk na maneno 'kupoteza maisha'. Kuna namna na muktadha maalumu ambapo unaweza kutumia maneno 'kupoteza maisha'.

  Na mara nyingine nimeona hiyo 'kupoteza maisha' ikitumika kama tafsida hivi, kujaribu kupunguza ukali wa neno kufa, kufariki nk.

  Hivyo, kwa maoni yangu ni neno/msemo sahihi.
   
 15. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  hapana, siyo kifupisho chake. kufariki ni kutengana au separate kwa kiingereza. rejea maelezo yangu katika post #8 hapo juu
   
 16. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Nimesoma vizuri tu maelezo yako. Unadhani neno 'kufa' limetokana na nini (kwa asili)? [neno gani la kibantu, kiarabu, kiingereza,kijerumani, iajemi nk].

  Ni kama vile mtu anaposema neno 'pop' (vz pop music), kwa jinsi lugha ilivyobadilika imekuwa ni neno linalojitegemea na ni vigumu mtu kufikiri ni kifupisho cha neno 'popular'.Mimi naamini neno kufa limetokana na neo kufariki (fariki) ambalo asili yake ni kiarabu ingawa kwa kiarabu likiwa na maana tofauti kidogo na ilie iliyochukuliwa na kiswahili. Kwa kiswahili kufariki (mara nyingi, kufariki dunia - 'kutengana na dunia') ndio kufa.
   
 17. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa,

  issue hapa si kuamini bali kuelewa.

  ubarikiwe sana

  Glory to God!
   
Loading...