Je, ni Sawa Kuvaa Hereni

Je, ni Sawa Kuvaa Hereni

John Achila Mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
111
Reaction score
214
Je, ni Sawa Kuvaa Hereni

Maandiko yanavyosema kuhusu kuvaa hereni.

Kitabu cha Hosea 2:13

Kitabu cha Hosea kinasema: “Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito, asema BWANA”.

Kitabu cha Waefeso 4:14
Tuzingatie hoja hii: Mungu akuumbe na masikio yaliyo kamili, halafu akuambie au akuruhusu uyatoboe masikio hayo, ili tu upendeze?
Jambo hilo linaweza kuwa kweli, kwamba Mungu aliagize au aliruhusu. Huo ni ujanja tu wa akili za binadamu, kama maandiko yanavyosema katika kitabu cha Waefeso: “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”.

Siyo rahisi kumhukumu mtu moja kwa moja kwa kutobolewa masikio. Huenda si yeye kwa hiari alifanya hivyo, bali walimtoboa tu akiwa mchanga/mdogo. Aidha, inawezekana waliomtoboa huenda nao pia walipokea tu kwa waliotangulia. Hivyo, huenda kosa si lake wala la wazazi, bali la yule wa kwanza kuanzisha makosa hayo.

Hata hivyo, baada ya kuelewa, si sawa kuendeleza hayo makosa kwa vizazi vyako. Vile vile si sawa kuweka chuma au dhahabu katika matundu ya masikio yaliyotobolewa, kwani kwa kufanya hivyo bado utakuwa unaendeleza desturi hiyo.

Tukirudi kusoma tena kitabu cha Hosea 2:13: “Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema BWANA”. Utaona kabisa kuwa Mungu atawaadhibu wanaovaa pete/hereni kwenye masikio. Yuko wazi kabisa kwa hilo. Yaani, hata kama watu wanavaa hereni, lakini wajue kuwa ni chukizo mbele ya Mungu, yaani si sawa kufanya hivyo.

Asili ya kuvaa hereni

Kabla ya kuvaa kitu, au kuiga mtindo fulani, hebu kwanza tufuatilie asili ya kitu hicho, kibiblia/kiimani, kwa sababu kuna vitu vingine asili yake ni mbaya, na isiyo na baraka kwa Mungu.

ASILI YA KUJIPAMBA KWA PETE ZA MASIKIONI (YAANI KUWEKA HERENI) ILIKUWA NI KUJIWEKA TAYARI KWA KUVUKIZA UVUMBA KWA MABAALI. Tukumbuke kuwa baali si mwingine, bali ndiye shetani mwenyewe (katika kinyago chake kingine). Kwa hiyo, zamani mtu akijipamba kwa kutoboa masikio na kuweka hereni, alikuwa, aidha ametoka kuvukiza uvumba kwa baali, au ndiyo anakwenda kuvukiza uvumba kwa baali. Na hereni zamani hazikuwa zinavaliwa tu na wanawake, bali hata na wanaume. Lengo lilikuwa ni hilo hilo, kumvukizia uvumba baali.

Kitabu cha Mwanzo 35:2, 4
Tuangalie ni wapi tena pengine katika maandiko, panapoonyesha hereni zinahusishwa na ibada za miungu.

Katika kitabu cha Mwanzo 35: 2“Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu. 4 Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, NA PETE ZILIZOKUWA MASIKIONI MWAO, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu”.

Hapo tunaona wazi kuwa mbele za Mungu, si sawa kuvaa herein, ndiyo maana Yakobo, mcha Mungu, aliwaambia watu waziondoe kutoka kwenye masikio, kisha akazifukia ardhini.

Turejee kuwa shetani (baali) ni yule yule, na ibada zake ni zile zile, hazijabadilika. Kama bado yupo kwenye makafara ya ng’ombe mpaka leo, na mbuzi, na bado waganga wake ni wale wale, na mavazi yao ni yale yale, na uchawi wake ni ule ule, je, uchawi wake kupitia HERENI (pete za masikioni) utakuwa umebadilika? Jibu ni hapana, utakuwa ni ule ule tu.

Tujue kuwa kuambiwa usivae hereni kunakufanya unakuwa huru, kwani inafanya unaondokana na chukizo mbele ya Mungu.

Aidha, tofauti na maandiko yaliyotajwa hapo juu, hakuna sehemu yo yote katika Biblia, ambapo uvaaji wa hereni umeruhusiwa.

Hebu tujiulize zaidi. Ni kweli kuwa kuacha kuvaa hereni ni kuonekana si mrembo kwa baadhi ya watu? Kinyume chake, ni kujiepusha na ibada za sanamu, ambazo zitakuzalia madhara makubwa ya kiroho.


Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, sawasawa na maandiko katika kitabu cha 1Wakorintho 3:16, na 1Wakorintho 6:19. Kwa jinsi tunavyozidi kuiweka miili kuwa mitakatifu, ndivyo Roho Mtakatifu anavyokaa ndani yetu, na ndivyo tunavyomfaidi Roho Mtakatifu kwa matunda yake yaliyotajwa katika Wagalatia 5:22: "Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu".

Hereni zinachukuliwa kuwa ni sehemu ya mavazi. Kwamba ni mapambo. Hata hivyo, siyo lazima kila vazi ni sawa mbele za Mungu.

Baadhi ya watu wanapenda kuvaa hereni.

Lakini, kupitia maandiko, Mungu mwenyewe amesema kuwa uvaaji wa hereni/pete masikioni ni chukizo kwake, ambapo uvaaji huo atautolea adhabu.
Je, tuko tayari kuendelea kuvaa hereni kama mapambo, na papo hapo tuko tayari kupokea adhabu kutoka kwa Mungu, kwa ajili hiyo?

Ni muhimu kuimarisha imani yetu kwa Mungu na kufuata Neno Lake kuhusu uvaaji wa hereni.
 
Hayo yanawahusu nyie wajukuu wa Yakobo na vitukuu vyote vya Israel. Ila Mimi mngoni WA songea huko hayanihusu Kwanza huyo Hosea mwenyewe sina ukoo nae na hata anachoandika hakutuandikia sisi kina mapunda.

Mimi wazee wangu mahoka (mizimu ya kingoni) inafarijika endapo kila mwaka nitatoa sadaka ya pombe za kienyeji na kuchinja mnyama kwenye jiwe kubwa la mbuji. Hapo nitahakikishiwa ulinzi wa wangu na watoto wangu.

Sasa endelea kujipendekeza kwa mababu au mizimu isiyokuhusu. Na usiniambie nimepotoka kwa kuleta ushahidi wa kitabu cha biblia au kuruani sitakuelewa kwa sababu havinihusu Mimi wala mababu zangu walioasisi kizazi changu.
 
ASILI YA KUJIPAMBA KWA PETE ZA MASIKIONI (YAANI KUWEKA HERENI) ILIKUWA NI KUJIWEKA TAYARI KWA KUVUKIZA UVUMBA KWA MABAALI. Tukumbuke kuwa baali si mwingine, bali ndiye shetani mwenyew
si kweli
Muasisi wa mapambo ni Mungu mwenyewe

Nenda kasome Ezekiel 16 ndo utaelewa
 
Back
Top Bottom