Fatuma ana mume wake wa ndoa kwa mda wa miaka minne sasa, ana kazi nzuri, wamejaaliwa mtoto mmoja ana 3years, wanavumiliana kwa mengi. Wanafanya mambo yao pamoja wanasaidiana ila Fatuma amekua akiona charts za mumewe na wanawake tofauti kwenye simu anavumilia anajipa moyo kwamba watakua wanataniana. Saa ingine anafanya uchunguzi wake anamuuliza mumewe yaani si mdada wa kukurupuka na haamini kama mumewe anaweza kumsaliti.
Fatuma ana rafiki yake anaitwa Hidaya ni rafiki sio sanaaa japo ni marafiki sasa amegundua ya kwamba Hidaya amezaa na mumewe tangu january kajua na ana ushahidi wote kuhusu huyu baby boy wa Hidaya na mumewe japokua hajamuuliza mumewe hajamwambia chochote sasa anajipanga aombe uhamisho akafanyie kazi Morogoro ni mfanyakazi wa local government anaipenda ndoa yake.
Hataki kuiacha ila kamchukia mumewe sana anataka kukaa nae mbali na hataki kumwambia chochote mumewe
Je yupo sahihi?