Je, ni sahihi Mwanajeshi na Polisi kutolipa nauli?

maamuzi haya ni makengeza ya kufikiri. Yaani askari, watu wazima ambao wanalipwa mshahara wasilipe nauli, halafu walemavu wasiojiweza walipe, akili kweli?
 
Heshima mbele wakuu... Pamoja na kuamua kutokuwalipisha nauli, pia tunawaahidi kuwaboreshea mishahara na kipato chao!! I waish I was the right age to join the army!! ha ha ahaaa

Angalia hii kutoka Nipashe la leo:

Maslahi ya askari kuboreshwa

2008-08-20 12:58:42

Na Beatrice Bandawe, Dodoma



Serikali inakusudia kurekebisha Sheria ya Ulinzi wa Taifa ili kuboresha maslahi ya askari. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliliambia Bunge jana wakati akifunga mjadala wa makadirio na matumizi ya wizara yake.

Alisema kamati imeundwa kupitia sheria hiyo na mwezi ujao inatarajiwa kuwasilisha mapendekezo yake wizarani ili yafikishwe bungeni.

Alikiri kuwa viwango wanavyolipwa wanajeshi ni vidogo mno na hata makazi yao ni duni.

Aliongeza kuwa, pensheni wanazopata ni ndogo na kwamba wengi wanapata Sh. 23,000 kwa mwezi.

Alisema kanuni za sheria hiyo inaonyesha kuwa, malipo ya pensheni ni kwa waliofikisha miaka 36 tu kazini na kwamba sheria hiyo imepitwa na wakati.

Kuhusu makazi ya wanajeshi, Dk. Mwinyi, alisema mahitaji ya nyumba zao ni 10,000 na uwezo wa serikali ni mdogo.

Alisema mwaka jana, walipata nyumba 212 tu zilizojengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 20 na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Juu ya pendekezo la wabunge la kutaka wanajeshi walipwe posho ya Sh. 10,000, alisema ili kiwango hicho kifikiwe wizara itahitaji kwenye bajeti yake Sh. bilioni 170 zaidi, jambo ambalo ni gumu.

Akizungumzia wanajeshi walioumia vitani, Dk. Mwinyi, alisema sera ya kuboresha malipo yao inaandaliwa ya kuwatunza na kuwaenzi wastaafu.

Kuhusu uwiano wa ajira kati ya Bara na Visiwani, alisema ajira zinatolewa sawa, isipokuwa tatizo linalojitokeza ni pale wapopimwa afya na kukutwa hawana sifa za kujiunga, ndipo nafasi hizo huchukuliwa na mikoa mingine.

Hata hivyo, alisema ili kuondoa malalamiko yanayojitokeza kuanzia sasa wanaomba nafasi katika Majeshi ya Kujenga Uchumi (JKU) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wataajiriwa moja kwa moja na serikali badala ya kupelekwa kwenye ngazi za mikoa.

Kuhusu maombi ya wabunge ya kutaka JKT irudishwe tena, Dk. Mwinyi, aliahidi kuwa hadi kufikia mwaka 2010 watu wote watakuwa wanapitia jeshi hilo kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu kanuni inayowataka vijana wanaoajiriwa jeshini wasioe hadi wanapotimiza miaka sita kazini, alisema serikali imezungumza na viongozi wa jeshi kuangalia uwezekano wa kupunguza muda huo.

Awali akichangia mjadala huo, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Bi. Faida Mohamed Bakar, alipendekeza askari watengwe na raia kwa kujengewa nyumba, zahanati na maduka yao ili wasidhalilike wanapokwenda kukopa.

Aliiomba serikali iwatafutie viwanja vya kujenga nyumba ili wanapostaafu wasihangaike.

Wabunge 63 walichangia wizara hiyo kwa maandishi na maneno, bajeti ya wizara hiyo ilipitishwa jana mchana.

SOURCE: Nipashe
 
mbona kama ugomvi au matatizo yametokea ndani ya gari na kuna askari mle ndani mimacho yenu yote mnamwangalia askari au mwanajeshi aliyepanda mle ndani? kama asingalipanda mngemwangalia nani? mimi naona wasilipe nauli na wazagae kwenye magari yote ya abiria ndo na usalama utazidi, vibaka na makonda hawataonea wananchi. ndo mawazo yangu, sipingwi na mtu ukweli ndo huo pamoja na kwamba mimi si mwanajeshi.
 
Serikali ya kifisadi hii. Mzigo wao wa kuwahudumia vizuri wanajeshi na polisi umewashinda kwa ufisadi na matanuzi yaliyokithiri ndani ya chama na serikali sasa wanataka kuwabebesha mzigo huo wale usiowahusu wenye mabasi. Kwa nini basi wasiseme watedaji wote muhimu wa Taifa kama vile waalimu, manesi, madakatari n.k. nao wasafiri bure!!!!? Maana hata wao gharama za maisha pia zimewashinda. Watafanya kila njia kuwaridhisha wanajeshi na polisi maana wanajua wakisema sasa basi wataichukua nchi.
 
Nashukuru sana ndugu wana JF kwa kuweka jambo hili mahala hapa tukajadili ili uongozi husika ulifanyie kazi maana naamini JF ni sehemu nyeti inayotoa muelekeo kwa viongozi na mara zote wamekuwa wakitekeleza kama JF inavyoshauri.

Kwa mtazamo wangu Wanajeshi wetu wasilipe nauli. Tuwape muda waone wanathaminiwa katika nchi yao. Kundi lingine ambalo sasa Serikali inatakiwa kulifanyia kazi ni Watabibu wote wa Hospitali za Serikali. Nao waachwe wasilipe nauli, utawaona mara nyingi wakihangaika kuokoa maisha yetu nao wapewe heshima hiyo.
 
NI aibu na fedheha km wanajeshi watakubali aibu hii ya kusafiri kwa dezo ktk magari ya abiria ya kiraia, wakati hata wenye ulemavu wa kupindukia, watoto wadogo na wa shule, pamoja na maiti wanasafirishwa kwa malipo. Kila mfanyakazi kwa nafasi yake ni muhimu sana..kwani kada yoyote ikikosekana ina athari kwa jamii.
 
Mbona wanajeshi wana magari mengi na yamepaki tu si wayatumie kubeba wanajeshi! Jamaa wanalazimika kulipa nauli kwa magari ya watu binafsi vinginevyo STJ, DFP, JW na PT yawabebe kila yanapowakuta haiwezekani Ma VX yanayobeba watu 8 anapanda mtu mmoja halafu wanajeshi wanaleta utata katika kulipa nauli kwenye daladala.

Bongo noma wanaoumia ni watu wa sekta binafsi kodi nyingi wakati wafanyakazi wa umma ambao ndio wanaoukula hiyo kodi wanaabudiwa na kutaka kuendelea kuhudumiwa na walipa kodi. Kama askari walipanda bure wakati wa UDA sawa hizi ni zama nyingine na serikali inawajibika kuwafidia wenye daladala.

Kuwa nice guys hakutamsaidia hata Mwinyi mwenyewe, Jembe liitwe jembe jamani!!!
 
Serikali ya Tanzania ina maamuzi mengi ya ajabu, na hili ni moja wapo.Si jui kinachoendelea ni nini.Ni kana kwamba wale watu waliokuwa wanaweza kufikiri Tanzania siku hizi hawapo.Jamani, askari au mwanajeshi asilipe nauli wakati anapata mshahara kama wafanyakazi wengine?Oh!Tena nimesahau,wanajeshi wanapata mishahara mikubwa kuliko wafanyakazi wengine wote wa serikali!Halafu kwa nini kwenye dala dala tu,basi hata wakienda kwenye huduma zingine zote wasilipe.Mbona na zenyewe ni biashara?Hili la wanafunzi nalo lina chekesha. Eti wapande kwa sh.100.Utadhani serikali ilichangia kwenye kununua hayo mabasi. Kweli hivi ni vituko.Basi kwanini isiwe hivyo kwenye biashara zote? Maana hii nayo ni biashara kama zingine!Huu ni uonevu wa wazi ambao serikali yetu inapashwa kuukomesha, kama kweli inasimamia utawala wa haki.
 
mbona kama ugomvi au matatizo yametokea ndani ya gari na kuna askari mle ndani mimacho yenu yote mnamwangalia askari au mwanajeshi aliyepanda mle ndani? kama asingalipanda mngemwangalia nani? mimi naona wasilipe nauli na wazagae kwenye magari yote ya abiria ndo na usalama utazidi, vibaka na makonda hawataonea wananchi. ndo mawazo yangu, sipingwi na mtu ukweli ndo huo pamoja na kwamba mimi si mwanajeshi.

...Kumuangalia kuna tatizo gani?? Yeye si mlinzi wa amani na usalama? ndio kazi yake kama anapanda dala dala na kunatokea tatizo lolote la kiusalama anawajibika kuchukua hatua lakini nauli lazima alipe wanunue hiace zao basi wapandishane bure tuone kama watamudu...Mshahara analipwa, pension na vitu vya bei ya chini kibao kuanzia bia, sigara, bati,radio mpaka TV bei ubwete. Nenda MIlitary super market Lugalo uliza bei za hivyo vitu then ukafananishe na bei za kariakoo...What's special kwao??? Mnataka kuwaendekeza eh!!
 
husika na kichwa hapo juu,nimekuwa nikijiuliza kwanini askari wetu hawatozwi gharama hii ya usafiri kwa upendeleo kiasi hiki,huku watumishi wengine wakigharamia huduma hii japo nao wanafanya kazi ktk mazingira magumu na mshahara japo ni mdogo.kama walimu, manesi nk

kama unazijua
TAFADHARI ORODHESHA
 
husika na kichwa hapo juu,nimekuwa nikijiuliza kwanini askari wetu hawatozwi gharama hii ya usafiri kwa upendeleo kiasi hiki,huku watumishi wengine wakigharamia huduma hii japo nao wanafanya kazi ktk mazingira magumu na mshahara japo ni mdogo.kama walimu, manesi nk

kama unazijua
TAFADHARI ORODHESHA
Nidhani umeweka hizo sababu.... Kumbe nawe unauliza....
 
hivi jamaa hujui hawa police na wanausalama kwa ujumla wanalinda USALAMA wetu...? au unataka waseme tu?
 
husika na kichwa hapo
juu,nimekuwa nikijiuliza kwanini askari wetu hawatozwi gharama hii ya
usafiri kwa upendeleo kiasi hiki,huku watumishi wengine wakigharamia
huduma hii japo nao wanafanya kazi ktk mazingira magumu na mshahara japo
ni mdogo.kama walimu, manesi nk

kama unazijua
TAFADHARI ORODHESHA

Kama nyie hamuwatozi nauli itakuwa labda ni makubaliano yenu tu..
Otherwise,hakuna sababu ya kumfanya asitoe nauli
 
hivi jamaa hujui hawa police na wanausalama kwa ujumla wanalinda USALAMA wetu...? au unataka waseme tu?

Mimi sijui unazungumzia ulinzi wa usalama upi. Liangalie swala la ulinzi wa usalama kwa mapana yake. Hebu jiulize ni nchi gani ambayo inaweza kuwa salama wakati wananchi hawajasoma ? au wanaumwa ? Au kodi haikusanywi ? n.k. Kwa namna moja au nyingine kila taaluma inahusika katika kulinda amani.
 
Hakuna sheria yoyote inayowalinda, wanachofanya ni kitendo cha WIZI.
 
Unalalamika kwani we unachombo cha usafiri kusema wanakuonea? Acha wenye magari walalamike maana huenda wao wanajua 7bu.
 
hawa jamaa walipe nauli haiwezekani mtoto wa primary alipe huku polisi na wanajeshi wasilipe ata kidogo wanavyolinda usalama wa raia vivyo manesi na madaktari wanavyolinda afya za raia vivyo hivyo walimu nao wanavoondoa ujinga kwa raia OVER.
 
Back
Top Bottom