Je, ni sahihi Mwanajeshi na Polisi kutolipa nauli?

Mkombozi

JF-Expert Member
Feb 19, 2008
805
424
Ndugu wana JF, jana na leo nimekua nikifuatilia vyombo vya habari na ususani tamko alilotoa Waziri wa Ulinzi kua wanajeshi hawatakiwi kutoa nauli. Mpaka sasa najaribu kuwaza ni kigezo kipi kimetumika kutoa msamaha hua na hasa pale wanajeshi wanapopanda magari ya watu binafsi.

Kwa upande wangu mimi nadhani si sahihi kwa wanajeshi na polisi kutolipa nauli. Hapa nchini tuna wafanyakazi wa aina nyingi kama walimu, madakitari, polisi, wanajeshi, wahasibu, mahakimu n.k. Sasa iweje hawa maaskari wasilipe nauli wao tu? Haiingi akilini kwa kusema ukweli. Hata kama wanalinda taifa sii sahihi kutolipa nauli pale wanapotumia vyombo vya usafiri vya watu binafsi, kama ni magari ya serikali hapo sawa.

Nadhani ingekua busara sana kumpigania mwanafunzi ambaye hana kipato chochote kutolipa nauli, inashangaza mwanafunzi asiye na kazi kulipa nauli halafua askari wetu wenye kazi na mishahara hawalipi nauli. Tunamganadamiza mfanyabiashara wa usafiri, mwanafunzi atoe mia moja, askari asilipe, Je! Atarudishaje gharama za uendeshaji? Chukulia kwa mfano Hiace moja ipande askari 8 na wanafunzi 8 je gari si imeshajaa hapo? Yaani uende tripu kwa sh 800.

Ni muhimu sana askari wetu kulipa nauli kama wafanyakazi wengine, wanafunzi na vilema wanavyolipa.

Je wewe mwana JF una Maoni Gani?

Naomba kuwasilisha hoja
 
Ni ajabu sana kwa kweli kwa mwanajeshi na polisi kutolipa nauli. Wafanyakazi wengine walipe. Hicho kigezo cha waziri kuwa wengi wa askari hawana nyumba ktk eneo la kambi zao sioni msingi wake, mbona walimu wapo ambao hawana nyumba ktk maeneo yao ya shule lakini serikali haijatoa tamko la kuwasamehe nauli? Au kwa sababu wanajeshi wana silaha viongozi wanaogopa wanaweza wakazitumia kuwang'oa? Tatizo ni kwamba, viongozi wanajua kabisa hawako madarakani kwa ridhaa ya wananchi, sasa wanachofanya ni kuwanyenyekea wanajeshi ili waendelee kuwalinda wabakie madarakani. Lakini wajue kabisa hakuna nguvu ya dola duniani iliyowahi kuwanyamazisha wananchi walipoamua kuasi kutokana na kuchoka na kukata tamaa. yana mwisho haya. Walikuwepo wababe duniani lakini walipita tena kwa fedheha na aibu. Mungu ibariki TZ.
 
Ni jambo la muhimu wanajeshi kuzoea kulipa nauli kama raia wa kawaida.
Nchi kwa sasa haipo kwenye mfumo wa ujamaa na kujitegemea ambapo kuna kujitolea kuhudumia umma.Tupo kwenye soko huria.
Kuzoea kulipa nauli kutawasaidia hata kuyazoea maisha ya mtaani baada ya kustaafu.Leo hawalipi nauli,bia jeshini bei chee,vitu vingi wanasamehewa kodi n.k.
Je akistaafu tena kwa cheo cha chini cha kungojea malipo baada ya miezi sita ataweza kupanda tena gari bure?Na tena akistaafu malipo yaweza kuota mbawa kama wazee wastaafu wa iliyokuwa Jumuia ya Afrika MASHARIKI.Kwa kuwa hakuzoezwa hivyo atajifunza kuua kwa ukatili maana ndo taaluma yao kuu waliyofuzu.

Makamanda hawa walipe nauli kama wanafunzi,walimu,mahakimu au serikali iwaandalie usafiri wa kwao nchi nzima kama wabunge ili wasichanganyikane na raia maana ni unyonyaji kupanda gari la mtu binafsi halafu tena unatunisha msuli huku gari hilo mfanyabiashara anategemea kuendesha maisha yake na familia yake.
 
naona na walimu, manesi, madaktari nao wasilipe ili kuleta usawa
 
kwa nini iwe nauli tu? hata madukani wapewe vitu bure, hotelini wale bure n.k!!! nina wasi wasi na uwezo wa kufikiri kwa wabunge wetu na mawaziri wao pia!!!!
 
naona na walimu, manesi, madaktari nao wasilipe ili kuleta usawa

Kwa muono wangu mimi naona hao wanajeshi wana vyombo vingi tu vya usafiri kuliko kitengo kingine chochote cha serikali; Kwa nini wasiwe na utaratibu wao mbali basi wa usafiri kama ni muhimu hivyooo hadi kuwa exempted nauli?
Hii yote ni nidhamu ya woga tu wanasiasa wetu waliyonayo, kesho watakuja na hoja ya kutaka kupangishwa nyumba za raia wa kawaida bure, na sisi tunyamaze.....Nooo!!
 
naona na walimu, manesi, madaktari nao wasilipe ili kuleta usawa

Ochu, hapo umegonga panapo penye sabau wote ni "Public Servants"......

Unajua wote hawa tunafahamu kuwa wanapokea mishahara midogo (so is me and you) lakini kwa sensitiveness ya kazi zao, tunaweza kuwapa special consideration, swali ni at whose cost?? Kingine hapo juu Mwan... amesema kuwa wanajeshi wana magari mengi kuliko Public Servants wote, hiyo ni jambo muhimu sana manake walimu wote hawana usafiri pia madaktari!

Mimi kwa upeo wangu ni kwamba SI SAHIHI KWA WAJESHI KUTOKULIPA NAULI NI UBAGUZI WA WAFANYAKAZI WA SEKTA YA KIJAMII.... lakini pia naelewa kuwa:
1. Logically sio sahihi,
2. Practically - ha ha haaaa, hawa wakuu wa kijeshi wakiambiwa walipe nauli wanaweza amua chochote kile!! Mnakumbuka issue ya kukatiwa maji makao yao makuu?? turudi nyuma miaka ya 80 mwanzoni, pia miaka ya themanini wakati wa land cruissers za Salim na mikopo ya magari ya Mwinyi!!

So, naona Wakuu kule Dodoma waliangalia practicality na kuamua liliamuliwa!!

Lakini swali ni, "Kwa nini lakini hawa jamaa wawe ni wa kuogopewa kiasi hiki?"
 
Tunako elekea sasa ndiko siko mbona walemavu ambao ni watu wakupewa msaada wananyimwa hii haki??na huku hawa wanajeshi wameletewa mabus mazuri ya kuwabeba.Hii serikali inataka kufanya nini sasa askari wapande daladala bure??mnajua gharama za kuyaendesha haya mabus kweli?alafu mtu apande bure mmempunguzia kodi mwenye chombo hicho?
 
Sio nauli tu, hata bia wanapelekewa kwa bei nafuu, kuna vyakula vinapikwa makambini na wanakula bure, humo majeshini ndimo CAG hakanyagi,....
 
Walikuwa!!

ni kweli kuwa wanajeshi na polisi walikuwa hawalipi nauli, lakini kama mnakumbuka kuwa toka wanafunzi walipopandishiwa bei, nauli ya daladala kupanda sumatra walitangaza rasmi kuwa wanajeshi na polisi wote wataanza kulipa nauli kama abiria wa kawaida kuanzia tarehe 01-08-2008.

na hata makondakta wameshukuru sana kwa mabadiliko hayo na wanasema wanatoa ushirikiano mzuri tu katika kulipa nauli, huyo asiyetoa ashitakiwe maana anakaidi amri iliyotolewa kuwataka watoe nauli.
 
Sisi raia tunafanya kazi kwa bidii ili tulipe kodi wanajeshi wetu walipwe mishahara watulindie nchi. Wakishapata mishahara yao wanaingia bar kunywa na wakishalewa huanza kutupiga baadala ya kutulinda, wakati magari ya wakubwa wao wakipita mijini raia wenye magari huambiwa wakae kando ili gari ya mkubwa ipite! Waache usanii, HAKUNA CHA BURE SIKU HIZI, WALIPE NAULI. Kama serikali ikiamua kuuza mashangingi yote ya wakubwa serikalini halafu inunue magari ya bei nafuu kwa viongozi, bila shaka serikali ingewza kununua usafiri tosha kwa wanajeshi wetu pamoja na kuwajengea makambi ya kuishi.
 
Ndugu wana JF, jana na leo nimekua nikifuatilia vyombo vya habari na ususani tamko alilotoa Waziri wa Ulinzi kua wanajeshi hawatakiwi kutoa nauli. Mpaka sasa najaribu kuwaza ni kigezo kipi kimetumika kutoa msamaha hua na hasa pale wanajeshi wanapopanda magari ya watu binafsi.

Kwa upande wangu mimi nadhani si sahihi kwa wanajeshi na polisi kutolipa nauli. Hapa nchini tuna wafanyakazi wa aina nyingi kama walimu, madakitari, polisi, wanajeshi, wahasibu, mahakimu n.k. Sasa iweje hawa maaskari wasilipe nauli wao tu? Haiingi akilini kwa kusema ukweli. Hata kama wanalinda taifa sii sahihi kutolipa nauli pale wanapotumia vyombo vya usafiri vya watu binafsi, kama ni magari ya serikali hapo sawa. Nadhani ingekua busara sana kumpigania mwanafunzi ambaye hana kipato chochote kutolipa nauli, inashangaza mwanafunzi asiye na kazi kulipa nauli halafua askari wetu wenye kazi na mishahara hawalipi nauli. Tunamganadamiza mfanyabiashara wa usafiri, mwanafunzi atoe mia moja, askari asilipe je atarudishaje garama za uendeshaji? Chukulia kwa mfano Hiace moja ipande askari 8 na wanafunzi 8 je gari si imeshajaa hapo? Yaani uende tripu kwa sh 800.

Ni muhimu sana haskari wetu kulipa nauli kama wafanyakazi wengine, wanafunza na vilema wanavyolipa.

Je wewe mwana JF una Maoni Gani?

Naomba kuwasilis hoja

Ndugu Mkombozi, ni kweli kabisa hakuna hoja ya msingi ya kuwafanya askari wasilipe nauli kwenye vyombo vya usafiri vya raia (yaani daladala). Ingekuwa kama vyombo hivyo ni mali ya serikali, afadhali. Mimi sioni sababu kabisa. Na hasa iweje askari asilipe na hali mtoto wake alipe nauli? Si kama hawana hela ya kulipia basi hata watoto wao wasingelipia Sh100.

Na ni kwa nini wakisafiri kwa ndege au treni wanalipa au na huko hawatalipa? Halafu kununua vitu dukani je? Itakuwa bure? Na elimu? Huduma za afya?
Taxi?

Kilichofanyika ni 'imposition'. Nchi yetu kwa sasa haina mwelekeo ndiyo maana walio madarakani wanatupeleka jinsi wanavyotaka wao na siyo jinsi inavyotakiwa.

Ukiwa na madaraka fulani unaweza ukaamua kitu fulani kifanyike ili upate sifa wewe mwenyewe na kikafanyika. Ndiyo maana inabidi sheria zirekebishwe ili walio madarakani watakapoboronga, mara tu baada ya kumaliza au hata kama hawajamaliza muda wao, waweze kuchukuliwa hatua kama inavyofanyika nchi nyingine. Bila hilo tutaendelea kuwatumikia viongozi wetu badala ya wao kututumikia.

Mimi nasikitika kuona umaskini unazidi kuongezeka nchini wakati madini yanazidi kugunduliwa na kuchimbwa. Ni aibu kubwa! Hata baadhi ya nchi zisizo na madini zinatuzidi sisi wenye madini kadhaa. Si ni aibu hiyo na ni kwa sababu ya uamuzi au uongozi mbaya tu!
 
Hawa hata bila kufikiri ni lazima walipe nauli. Ni wafanyakazi kama wafanyakazi wengine tu, na mishahara haitoshi kama wengine.
 
Ochu, hapo umegonga panapo penye sabau wote ni "Public Servants"......

Unajua wote hawa tunafahamu kuwa wanapokea mishahara midogo (so is me and you) lakini kwa sensitiveness ya kazi zao, tunaweza kuwapa special consideration, swali ni at whose cost?? Kingine hapo juu Mwan... amesema kuwa wanajeshi wana magari mengi kuliko Public Servants wote, hiyo ni jambo muhimu sana manake walimu wote hawana usafiri pia madaktari!

Mimi kwa upeo wangu ni kwamba SI SAHIHI KWA WAJESHI KUTOKULIPA NAULI NI UBAGUZI WA WAFANYAKAZI WA SEKTA YA KIJAMII.... lakini pia naelewa kuwa:
1. Logically sio sahihi,
2. Practically - ha ha haaaa, hawa wakuu wa kijeshi wakiambiwa walipe nauli wanaweza amua chochote kile!! Mnakumbuka issue ya kukatiwa maji makao yao makuu?? turudi nyuma miaka ya 80 mwanzoni, pia miaka ya themanini wakati wa land cruissers za Salim na mikopo ya magari ya Mwinyi!!

So, naona Wakuu kule Dodoma waliangalia practicality na kuamua liliamuliwa!!

Lakini swali ni, "Kwa nini lakini hawa jamaa wawe ni wa kuogopewa kiasi hiki?"

Mkuu unachosema ni kweli. Kama tungefikiria unyeti wa kazi na kusema fulani asilipe nauli, waganga, wakunga, marubani, walimu, mahakimu, wanasheria, nk nao wasingelipia.

Watu wengine wanasema eti wakati tunalala wao wanatulinda. Lakini ndivyo kazi yao inavyohitaji. Na kwa kutulinda sisi wao wanapata ajira. Kwa hiyo kuna 'symbiotic relationship' kati yetu na hiyo askari tu.

Kitu muhimu cha kufanya ni kuboresha maisha yao - kupata mshahara mzuri - kuliko kuwapendelea ili wapate huduma bure. Watu ambao inabidi tuwapendelee na hatufanyi hivyo ni watoto wadogo, wajawazito, wagonjwa, walemavu na wazee.
 
Serikali Inapojivua majukumu yake yote - isipokuwa la ukusanyaji na utumiaji wa kodi na misaada.

Wanafunzi - jukumu la kuwasafirisha wamebebeshwa wenye daladala;
Askari - usafiri wao wanaachiwa daladala;
Ujenzi wa shule - wanaachiwa wananchi;
Ulinzi/Usalama - wanaachiwa wananchi through sungusungu/ulinzi jamii.

Kwa vile majukumu ya serikali yanaonekana kupungua, ni vyema kwa ukubwa na upana wa wanasiasa kupungua vilevile.
 
Naona serikali inajua ni jinsi gani nauli zinavyowaumiza wananchi na mishahara iliyo kiduchu. Wasingependa wanajeshi nao waexperience hali ya ugumu wa maisha, kwani kwa kufanya hivyo wanatengeza mazingira ya jeshi kuungana na kilio cha walalahoi, kitu ambacho ni hatari kwa ustawi wa mafisadi. Hiyo ndio siri ya mzigo wa nauli ya wanajeshi kubebwa na wamiliki wa madala dala.
 
hapa si cha mshahara mdogo wala nini.askari hana ofisi.popote alipo ni ofisini kwake.kwa hiyo kumwambia alipe nauli ni kwenda Kimyume kabisa. hivi tuseme wakiiniga na zile bunduki zao kama vifaa vyao vya kazi wakawa wanazunguka nazo unaweza hata kuthubutu kufungua mdomo? unajua Tanzania hatujajua thamani na risks walizonazo hawa jamaa kwa hiki kiupepo cha amani kinachotudanganya.ipo siku watu tutawatafuta.
 
naona ni halali walipe nauli na vitu vingine vyote kama watanzania wengine.
wapate unafuu katika mali/ huduma ambazo zinaendeshwa na serikali. Mfano maduka yao, magari yao, nyumba zao nk.
dala dala ni wafanyabiashara tu kama wengine, kuwaonea kunaonyesha kuna siku moja katika biashara zetu za mama lishe tutakuja kuambiwa tuwape watu fulani chakula bure!!! itawezekana?
 
My take: Kwa sababu serikali ilishajitoa kwenye biashara basi wakipanda "private" transport walipe nauli la sivyo serikali iweke ruzuku "subsidy" kufidia gharama zao au iwape hao wanajeshi transport allowance.
 
Hawa ndio maana makonda wanawaita "mawe" kwanza wanapata vitu vingi kwa bei nafuu kuanzia mchele,nyama,nyumba bure mpaka bia pia wana punguzo lao pili wana magari yao meengi tu kwanini yasitumike kama usafiri wao?
huku ni kuumizana tu.....madaktari,walimu na wengineo nao ni wafanyakazi nyeti na wao wasilipe nauli.....kuna jamaa mmoja alisema wanajeshi wanankuza vitambi tu kwa kuwa hawana kazi......walipe hatutaki U kupe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom