Je, ni sahihi mtumishi wa serikali kulipa michango ya kijiji wakati kila mwezi anakatwa kodi?

Tido mtoga

JF-Expert Member
Oct 21, 2015
514
433
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu,

Huku kwetu imekuwa ni lazima hata mtumishi wa serikali kutoa mchango wa kijiji wakati mimi ninavyofahamu mimi nakatwa kodi katika mshahara wangu.

Naomba wataalamu wa haya mambo watujuze watu ambao hawajalipa wanakamatwa na kulipishwa faini elfu hamsini na tano.

Nb:
Sijataja sehemu yanapo fanyika haya kwa ababu natumia real ID nimehofia usalama wangu.
 
Kweli naona hata uniform za shule serikali ya kijiji inunue sababu unakatwa kodi kila mwezi.
 
Taja jina laki full na mawasiliano ya na kijiji ulipo na wahusika ndio operation nianze
Itapendeza
 
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu huku kwetu imekuwa ni lazima hata mtumishi wa serikali kutoa mchango wa kijiji wakati mi navyo fahamu mimi nakatwa kodi katika mshara wangu naomba wataalamu wa haya mambo watujuze watu ambao hawajalipa wanakamatwa na kulipishwa faini elfu hamsini na tano
Nb:
Sijataja sehemu yanapo fanyika haya kwa sababu natumia real name nahofia usalama wangu.
Mkuu usiwe na hofu juu ya usarama wako mimi ndiye niliyekuja kukuchangisha, kumbe upo humu jf? Nmefurahi kukufahamu, nikutakie masomo mema.
 
Hivi na polisi huwa wanachangishwa fedha za ujenzi wa vituo vyao kama walimu wanavyochangia ujenzi wa shule, zahanati na vituo vya afya??!
 
tatizo hamju hata muundo na mfumo wa serikali zilizop[o katika nchi yenu. Serikali ya kijiji ni Mamkala kamili na serikali kamili kama ilivyo serikali kuu. Kodo katika mshahara wako unakatwa kwa mujibu wa sheria ya kodi na serikali kuu inayokulipa mshahara. Serikali ya kijiji au mtaa ni serikali yko pale unapoishi, hivyo unatakiwa kushiriki kila kitu. Mimi mtaani kwangu wote tunachangia maendeleo ya Mtaa wetu. Acha habari ya kuchangia ujenzi wa shule, sisi tunanchangia hadi kujenga barabara zetu za mitaa. Hakuna mwanajeshi wala polisi wala jaji. Wote tunachangia na kushiriki shughuli zote ya mtaa wetu chini ya usimamzi wa serikali ya mtaa wetu.
 
Back
Top Bottom