Danny Jully
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 4,416
- 3,860
Huo utukufu wa mahakama ni upi? Tujiepushe kutumia maneno tusiyojua maana yake.View attachment 546312
Hili swali liwaendee wahusika wote wakiwemo wanasheria,Majaji na mahakimu,waandishi wa habari na wanaJF kwa ujumla.
Tundu lissu aliitisha vyombo vya habari katika majengo ya mahakama mjini Dodoma na kuhojiana navyo.
Lissu aliongea na vyombo hivyo na kuanza kuwashutumu polisi wa mkoani Dodoma kuwa wanataka kumkamata jambo ambalo limekanushwa na RPC Dodoma.
Nikijikita kwenye swali...kwa ufahamu wangu Mahakama ni sehemu tukufu na sitegemei kuona inatumika kama jukwaa la kisiasa.Je Hakimu mfawidhi wa mahakama husika aliridhia kwa kutoa kibali cha kumruhusu lissu kutumia vyumba vya mahakama kufanya press?