Je ni sahihi kwa Rais wa nchi kuwa mwenyeji wa waziri wa nchi nyingine?

Mathematic

Member
May 15, 2011
56
2
Wana Jamii, kwa jinsi nijuavyo mimi ni kwamba Rais wa nchi fulani anapotembelea nchi nyingine,protocaly mwenyeji wake anataakiwa awe ni yule Rais mwenzake wa ile nchi anayoitembelea,hivyo hivyo kwa mawaziri ambapo hulakiwa na waziri mwenzake wa nchi anayoitembelea kwa wizara husika. Sasa kilichonishangaza ni kitendo cha Rais wetu kuwa mwenyeji wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani baadala ya kazi hiyo kufanywa na Benard Membe. Au kwa kuwa waziri huyo anatokea nchi tajiri basi akienda nchi kama Tanzania anapewa hadhi ya urais? Nawasilisha.
 
Mahesabu,
Hakuna lililoharibika. Hillary alipokelewa na Membe alipowasili DSM, lakini vivyo hivyo alifanya mazungumzo na rais Kikwete ambalo ni jambo la kawaida kabisa. Kumbuka hata wabunge wa nchi ya kigeni wanapotembelea nchi yako ni protocally correct for a head of state to give them an audience.
 
Ni sawa tu coz hata mi mwenyewe nikiendaga ukweni MAMA MKWE ndiyo ananitandikiaga kitanda, so literally an equation has BALANCED!
 
Protocol ipi kwa nchi maskini kama TZ: Raisi anaruhusiwa kabisa hata kumchezea ngoma WAZIRI wa nchi nyingine endapo kwa kufanya hivyo TZ itajikomboa. Ukipinga hilo na basi tuwe na uwezo wa kujitegemea.

Protocal yetu inaongozwa na wanaotufanya tuwe kama nchi ama wanaochangia bajeti ya serikali ya CCM kwa namna moja ama nyingine - hapo ikiwa ni pamoja na whisani nk.
 
Obama alipokewa na Gordon,Angel Markel na Sarkozi na kupewa heshima kama ya kiongozi wa nchi just akiwa senetor na kama mgombea urais mwaka 2008....so hili la Cliton kuwa hosted na Mr President halina tatizo maadam alipokelewa na conterpart wake Membe
 
Back
Top Bottom