Je Ni Sahihi kwa LHRC Kujitwika jukumu la kutafsiri rasimu ya katiba kwa kiingereza??

Mafuchila

JF-Expert Member
Apr 29, 2006
751
65
Ni Muda sasa nimekuwa nikiziangalia hizi asasi zetu kwa jicho la tatu. Je ni sahihi kwa kila asasi au mdau kutoa tafsiri yake ya katiba? kama jibu ni sawa ni nani anawajibika ikiwa kutatokea upotoshaji wowote wa kimantiki? na je nani mlengwa kwa jitihada hizi za kutafsiri katiba hii kwa kiingereza ni raia wa Tanzania au Wafadhili? Pamoja na maswali hayo naomba kuchokoza mjadala, ukiweka kwenye mizania ni kwa kiasi gani asasi za kiraia zinamtumikia raia/Mtanzania, ni swali ambalo limekuwa likinisumbua kwa muda sasa.
 
Back
Top Bottom