Je ni sahihi kuwalaza watoto....

Je ni sahihi kuwalaza watoto....

Mbona mmekuwa na hofu sana...!!?
 
Hamjambojeeee.....

Wanajamvi, je ni sahihi kuwalaza watoto chumba kimoja pamoja na wageni???

Fikiria umepata mgeni, una chumba chako, cha watoto wa kike na wakiume. Mgeni ni mwanaume, je unamruhusu alale pamoja na watoto wa kiume???

Mgeni ni mwanamke je utamruhusu alale na watoto wa kike???

Je unaweza kuhamisha godoro la ziada ukamwekea mgeni sebuleni akalala na watoto wakabaki chumbani?



Je utahamisha godoro la ziada chumbani na kuwawekea watoto
sebuleni wakampisha mgeni akalala chumbani?

Je utafanyeje??

Karibuni kwa maoni....

CL
Kwa Dunia ilivyo na mauzauza ya tabia, ni BORA tena kwa herufi kubwa upishe wanao chumbani kwako ,wewe ulale sitting room au ulale nao..hakuna kuaminiana siku hz...zamani akija mgeni wanampa mtoto mmoja alale nae kama sio kikojozi ...lakini sio sasa aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini mgeni aje bila taarifa?

Mpeleke guest house akalale huko..
 
haaaaa hata kama usingizi umekubana inabidi uwe mpole tu.... usubiri wamalize kuangalia tamthilia ndio ulale
Au kama kuna mtu amedamka asubuhi na mapema (let say Jirani) alafu anakukuta umeangusha sebuleni, unajifunika shuka hakuna kutikisika na akiaga tu unaamka
 
Kwanini mgeni aje bila taarifa?

Mpeleke guest house akalale huko..
Labda wewe ni mgeni katika nchi hii ya extended family hasa those days...sasa hivi at least watu sio wavamizi kwa ndugu lakini zamani mtu anakuja tu vuuuuu alafu anakaa bila issue (amekuja kusalimia ndugu yake)...na mwenye ndugu anampokea tu japokuwa akikaa siku nyingi nae anaanza kuboreka
 
Mgeni anapokuja bila taarifa ya wewe kumuandalia mahali pa kufikia na nafasi haitoshi ataangusha sitting room tu Maana hakuna namna.

Watu wamegeuka wa ajabu siku siku hizi.
usimwamini hata ndugu yako.
Wanalawiti na kuwafundisha vitu vya ajabu watoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KWA MIAKA HII KUFANYA HIVYO NI NGUMU KIDOGO....USIKU MREFU HUWEZI JUA WANAOWATAFANYWA NINI... MUHAMISHE KWA TAHADHARI.
 
Kamwe usilaze wanao na mtu yoyote..awe anaeleweka ai haeleweki.Ubaya hauna sura.Afu watu wanao aminiwa sana ndo huwa waharibifu
 
Kama watoto ni wadogo, nitawalaza chumba kimoja then mgeni atalala pekeye.

Usawa huu kuwalaza watoto na wageni wasioeleweka ni hatari zaidi.
 
Labda wewe ni mgeni katika nchi hii ya extended family hasa those days...sasa hivi at least watu sio wavamizi kwa ndugu lakini zamani mtu anakuja tu vuuuuu alafu anakaa bila issue (amekuja kusalimia ndugu yake)...na mwenye ndugu anampokea tu japokuwa akikaa siku nyingi nae anaanza kuboreka
Anatakiwa alete taarifa kabla hajaja.
Kama kumejaa unamwambia aje wakati mwingine.
 
kama sina vyumba vya kutosha na amekuja bila taarifa akitegemea kulala kwangu... namwambia tu ukweli kua hapatoshi na sipendi mtu alale sehemu yoyote tofauti na chumbani over...
 
Back
Top Bottom